Mh. Kate Kamba akichukua fomu za kuwania
Uspika toka kwa katibu mkuu wa CCM Mh. Yusuf Makamba
Wengine waliochukua fomu za kuwania kiti cha Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Mbunge mteule wa Jimbo la Bariadi Magharibi, Shinyanga Andrew Chenge, yumo pia Mbunge mteule wa Jimbo la Kongwa Dodoma Job Ndugai na vile vile Mbunge wa Jumuhiya ya Afrika Mashariki Bi. Kate Kamba. Zoezi hilo limekamilika leo Ijumaa, 5 Novemba 2010 saa 10 jioni.
Mh. Job Ndugai akichukua fomu toka kwa Mh. Yusuf Makamba

Mh. Andrew Chenge akichukua fomu za kuwania Uspika



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Bongo tambarare sana...Speechless...

    ReplyDelete
  2. Michuzi nafikiri unaelewa vizuri kiswahili. Sijui kwanini unatumia neno mteule. Nifuatia sehemu kibao unatumia neno mteule kwa wabunge na rais walioshinda kwenye uchaguzi. Mteule ni mtu aliyeteuliwa na watu na kunakuwa hakuna ushindani wala hakuna kupiga kura unateuliwa. Kwa mfano wakuu wa wilaya na mikoa unaweza ukawaita wateule kwasababu hawachaguliwi. Sasa sijui jamani huu undishi wa kipambe usiofuata maadili ndio unaowajaza watanzania ujinga na kukosa dira. Michuzi unatumia nguvu yako vibaya. Hata ukiweka kapuni maoni haya ni sawa tu kwasababu ujumbe ni wakwako.

    ReplyDelete
  3. KWA UJUMLA HUU MCHAKATO UTAKUA NI MKALI SANA MAANA WAMEAMUA KWELI KUCHUKUA FORM ZA KUTAKA NA KUONESHA NIA...KWA UJUMLA NAWATAKIA KILA LAHERI....ATAKAESHINDA BASI NA SISI WATANZANIA WOTE TUTAMPONGEZA

    ReplyDelete
  4. .....Tehe...tehe...tihii!...kuna mtu hapo atakula kibano, mpambano mboni kunaga!!

    ReplyDelete
  5. unaesema michuzi kakosea kuandika raisi mteule au mbunge mteule wewe ndio umeingia chaka. ni sahihi kuitwa rais mteule (president elect) hadi hapo atakapo apishwa rasmi kwa mujibu wa katiba ya nchi.

    hata mataifa mengine Duniani wana utaratibu huo mfano hata Baraka Obama wa marekani alikua anitwa president elect nearly 2 months hadi alipoapishwa.

    ReplyDelete
  6. HAPO NDO CHAMA CHANGU CHA MAPINDUZI KINAPOPOTEZA DIRA...INAUMA SANA
    HIVI MTU UNA TUHUMA KIBAO MGONGONI MWAKO KWA NINI USISUBIRI ZIISHE THEN UWANIE VITI VIKUBWA.
    KWA UJINGA CCM WATAMPA MTUHUMIWA NAFASI HALAFU WATASHINDWA AU KUPIGWA CHINI,THEN WATAANZA KUMTAFUTA MCHAWI.
    TUMEPOTEZA VITI 59 KWA UZEMBE NA KUBEBANA.
    IMEFIKA WAKATI KAMA MTU KWA WAKATI HUO HUFAI SUBIRI JISAFISHE KISHERIA THEN GOMBEA.
    KWA JINSI NINAVYOONA NAFASI YA USPIKA NAYO INAENDA UPINZANI.
    wagombea tukionee chama chetu huruma..tunataka kurudisha heshima iliyokuwepo......KIDUMU

    ReplyDelete
  7. Naomba mnieleweshe labda sijui.
    Kwani kugombea Uspika watu wanachukua forms kupitia chama cha CCM kama hapa?
    Au ni ofisi za bunge?
    Kwani navyoelewa Spika atakuwa ni Spika wa Bunge na si CCM.
    Naomba elimu ndugu zangu.

    ReplyDelete
  8. JK keshaingia Ikulu, tumpe na Chenge uspika ili tuwe na wazoefu wawili kwenye mihimili miwili.

    ReplyDelete
  9. wewe unayesema elected ni mteule unatakiwa urudi shule...appointed ndio mteule elected ni kuchakulliwa kama huyo hapo juu alivyosema..sas kama hawjawa official sowrn to the office kiswahili kachukue dictionary lakini si sahiii kusema mteule nimtu aliyechaguliwa..

    ReplyDelete
  10. Jamani hivi watanzania tunajia lugha gani? Mbona hili liko wazi sana!
    Kipindi toka mgombea kuchaguliwa mpaka kupishwa anakua ‘mteule’ au elect kwa kiingereza ambacho wengi wetu huwa tunavunga kwamba tunakijua tofauti na ‘wa kuteuliwa’ ambaye ni appointed . Na ndio maana tunakua na wabunge wateule na wakishaapishwa wanakua ‘wabunge’ bile kutumia neno mteule. Muulizeni mbunge mteule Prof. Kahigi atakusaidieni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...