Salaam,Ankal

Naomba utusaidie kuwafikishia wadau wenzetu ujumbe huu.

Nidhahiri kuwa tunaoumoja wetu tangu mwaka 2007 (Ljs-Phileo) ila muda unavyokwenda tunazidi kurudi nyuma hivyo katika misiba miwili iliyotokea hivi karibuni baadhi ya wanachama waliona nivema kuitana na kujadili baadhi ya mambo.

WAPENDWA wana LJS-Phileo napenda kuwajulisha kuwa kutakuwa na kikao cha pamoja cha umoja wetu
kwa utaratibu ufuatao

SIKU ; IJUMAA

TAREHE; 12 NOVEMBER 2010

MUDA; SAA 11 JIONI

MAHARI; KIJIJI CHA MAKUMBUSHO KIJITONYAMA JIJINI DAR (MAKUMBUSHO)

-- AGENDA KUU: KUJADILI JINSI YA KUBORESHA UMOJA WETU KATIKA
KUWASILIANA,KUSAIDIANA KKT SHIDA NA RAHA.

KUJADILI JUU YA MFUMO WA UWAKILISHI LINAPOTOKEA JAMBO.

NA JAMBO LINGINE LOLOTE KWA RUHUSA YA MWENYEKITI

Tafadhari atakaye pata ujumbe huu awajulishe wengine

Godwill Matayi
Kamati ya Maandalizi.

0715 45 63 43 / 0784 45 63 43 /0784 45 63 43

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Mwalimu alikataza sana haya mambo, wachaga tu hao.

    ReplyDelete
  2. jamani msiba wa nani tena alikuwa mwana ljs ama maana msiba wa mwisho ulikuwa wa Charles maro mungu amlaze mahala pema peponi aminaa

    ReplyDelete
  3. Watu wengine wana hobby ya kupanda mbegu za ukabila lakini bahati mbaya hazioti ktk udongo wetu.

    Godwill si Mchaga na hata angekuwa Mchaga hakuna hoja hapa ya kujadili hilo! Tafadhali sana tuheshimiane.

    Godwill asante sana kwa Tangazo:
    1. Samahani, naomba utujuze hiyo misiba iliyotokea ni ya akina nani.

    2. Tangazo kwa hadhira husika ni waraka unaofuata kanuni za uandishi rasmi hivyo jaribu kuwa unapitia tangazo lako kabla ya kulituma maana kuna makosa kidogo ambayo ungeweza kuyarekebisha; hata hivyo ujumbe umefika.

    ReplyDelete
  4. Jadilini namna ya kuiboresha LJS Morogoro kitaaluma na mengineyo.Mmesoma mnataka tu kujadili mambo ya shida zenu mnaacha kufikiria namna shule hiyo iliyowafungua macho na akili ni namna gani iendelee kuwa chachu ya elimu bora eti mnataka kujadili misiba,hahahahaaaaaa haya jamani ndicho mlichochagua!!

    ReplyDelete
  5. Mmenikumbusha nilivyotembelea Lutheran Junior Seminary miezi michache iliyopita. Napenda kusema mambo mawili.

    Pamoja kuwa na mitandao ya wahitimu, tunahitaji kujenga utamaduni wa kuzichangia shule zilizotusomesha. Nawahimiza kufanya mikakati hiyo.

    Napenda pia kusema kuwa huku ughaibuni, wengi wanaifahamu Lutheran Junior Seminary kutokana na masomo ya ki-Swahili yanayofundishwa hapo. Niliandika kijitaarifa kuhusu hilo. Soma hapa.

    ReplyDelete
  6. HUYU ALIENDIKA NAHISI NI MKURYA

    MAHALI=/= MAHARI
    TAFADHALI=/= TAFADHARI


    CHA MSINGI NI KUZIWEZESHA SHULE ZILIZOKUSAIDIA KUFIKA HAPA ULIPO

    ReplyDelete
  7. na pia ungesema waliosoma hiyo shule na wanaoishi Dar ...ukisema wote halafu mkutano unafanyikia makumbusho na agenda ni misiba huu sio umoja wa wanafuzi wote. mgefungua social groups yenu na kama ni kuunga wanafunzi wote basi agenda ziwe pay back to society na kila almni yeyote na mahali popote. Mnaweza kufanya mkutano on line no matter where you live mnaweza kufanikisha ili . kama madhumuni ni kusaidia shule uliyosoma ili wadogo zako au watoto wako nao wapate elimu bora

    ReplyDelete
  8. nimefurahi kuona umoja wa waseminari basi nami naomba unijuze kikao kingine kitakuwa lini na wapi ili nami nije na wenzangu wengine tuungane pamoja kutoa mawazo yetu kuendelea kuboresha umoja huu asante

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...