Kocha mkuu wa timu ya Taifa,Jan Poulsen akitangaza kikosi ya timu ya Kilimanjaro Stars leo katika ukumbi wa mikutano wa shirikisho la soka nchini (TFF). Kikosi hicho ndicho kitakacho shiriki katika mashindano ya Cecafa Tusker Cup yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 27 mpaka Desemba 10,2010.katikati ni Meneja wa bia ya Tusker,Nandi Mwiyombella na kushoto ni Afisa Uhusiano wa SBL, Imani Lwinga.
Na Mwandishi Wetu
KOCHA wa timu ya taifa Jan Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 22 uku akimrudisha kundini mshambuliaji Gaudence Mwaikimba na Juma Nyosso ambao walitemwa kwa kipindi kirefu katika kikosi cha Mbrazil Marcio Maximo.
Mwaikimba mshambuliaji wa zamani wa Yanga alikuwa mmoja wa washambuliaji tegemeo wa Stars chini ya Kocha, Marcio Maximo raia wa Brazil, hata hivyo baadaye alimuacha mshambuliaji huyo kutokana na kushuka kiwango na baadae kufungashiwa virago na Yanga.
Hata hivyo mchezaji huyo ambaye awali alikuwa kipenzi cha Maximo kutokana na umbile lake amekuwa lulu kwenye timu ya Kagera anayochezea hivi sasa na aliweza kumshawishi Poulsen amrudishe kundini baada ya kuonyesha kiwango kizuri kwenye mzunguko wa kwanza wa Ligi uliomalizika mwishoni mwa wiki.
Wachezaji wengine walioitwa kwenye kikosi cha Kilimanjaro Stars ambacho kitashiriki michuano ya Chalenji iliyopangwa kuanza Novemba 27 hapa nchini ni mlinda mlango Juma Kaseja (Simba), Shaban Kado (Mtibwa) na Said Mohamed wa Majimaji. Wengine ni Shedrack Nsajigwa, Erasto Nyoni, Stephano Mwasika, Haruna Shamte (Simba), Idrisa Rajabu, Shaban Nditi, Henry Joseph (Kongsvinger- Norway), Nurdin Bakari, Jabir Aziz, Nizar Khalfan (Vancouver Whitecapes -Canada), Salum Machaku, Mohamed Banka na Kiggi Makasi.Wengine ni Dan Mrwanda (DT Long - Vertinam), Mrisho Ngasa, John Boko, na Thomsa Ulimwengu anayesaka soka la kulipwa nchini Sweden.
Akitangaza kikosi hicho Poulsen alisema baadhi ya wachezaji hao pia wataunda kikosi cha timu ya taifa Taifa Stars kitakachocheza mechi ya taifa ya kirafiki Novemba 17 kujiandaa na michuano ya kufuzu fainali za mataifa ya Afrika baadae mwakani itakayofanyika Gunea.
===== ===== =====

Kilimanjaro stars Coach Jan Poulsen today announced a squad which will represent the Tanzania Mainland team during the CECAFA TUSKER CUP.

The press conference was attended by the Acting Secretary General Mr Sunday Kayuni, Serengeti Breweries Limited (SBL) TUSKER Brand Manager Nandi Mwiyombella and SBL Corporate Relations Senior Executive Imani Lwinga, amongst others.

Speaking at the press conference today in Dar es salaam, the SBL Brand Manager Ms Nandi Mwiyombella said, we are committed to raise the football standard for East and Central Africa, and we would like to see the East and Central African Teams (Countries) be presented in the next World Cup 2014 in Brazil and would like to see TUSKER at the heart of that journey.

As the title sponsors we will be making effort to ensure that this competition will be the best ever in CECAFA history, we have a very good engagement from CECAFA and TFF. She added.
The 12 teams who have confirmed for the competition are the host Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Somalia, Zanzibar, Ethiopia, Sudan. Invited Guest teams are from Ivory Coast, Zambia and Malawi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Beki ya stars Bila Cannavaro....Nurdin Haroub wa Yanga!!!!!!!!hii inawezekanaje?au kuna sababu?
    asilete masiala huyu!!!!!watu tuna hasira!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. Cannavaro wa yanga yupo ktk timu ya Zanzibar ndio maana hakuitwa. Ingawa sikusikia timu ikitajwa ila ninahisi Shamte aliyetajwa ni Juma Shamte wa Simba sio Shamte Ally wa Yanga kama Michuzi ulivyoandika kwa kuwa Shamte wa yanga kocha hajamuona ni majeruhi siku nyingi na hajapona.

    ReplyDelete
  3. Hongera kwa kutupa habari lakini list yako ina mapungufu kwani kuna baadhi ya wachezaji umeandika na timu wanazo chezea na baadhi hujaandika,sasa sijui ni vigezo gani umetumia kwa hilo.
    Pili mimi nina amini kuwa kocha wetu kutokana na ugeni wake hawajui wachezaji wote hivyo hiyo list anapangiwa na baadhi ya watu.
    Kwani hapati muda wa kuwaona wote,je anawachaguaje katika orodha yake?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...