NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
JUMLA ya Watanzania wapatao zaidi ya 500 wanatarajiwa kupatiwa matibabu mbalimbali ya huduma za afya yatakayotolewa kuanzia leo hapa nchini na madaktari 13 bingwa kutoka katika hospitali za Apollo za India.
Hayo yalisemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Mama Blandina Nyoni alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio wa madaktari hao, ambao watakaa hapa nchini kwa muda wa siku saba, ambapo alisema utaratibu huo wakuwaleta utakuwa ni endelevu kila baada ya miezi mitatu.
Alisema madaktari hao, watatoa matibabu hayo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Taasisi ya Mifupa ya Binadamu (MOI) na Taasisi ya Sartani ya Ocean Road. .
“Madaktari hao ni wa magonjwa ya saratani ,moyo, figo na mishipa ya fahamu, mifupa na viungo na watatoa matibabu bure kuanzia Jumanne kwa wagonjwa waliwahi kutibiwa India, waliopewa rufaa za wizara na waliotayarishwa kuona na hospitali hizo,” alisema Mama Nyoni.
Naye Kiongozi wa msafara wa huo, Bw. Radhey Mohan , ambao uliwasili jana jumapili alisema ujio wao utasaidia kubadilishana uzoefu na utaalamu kati yao na madaktari watakaofanya nao kazi wa hapa nchini. “ Ujio huu utasaidia kuboresha ushirikiano,” alisema Radhey.
Madaktari hao wanatoka katika hospitali za Apollo za Chennai, Bangalore, Delhi, Ahmedabad na Hyderabad. Hii ni mara ya pili kwa madaktari kutoka nchi hiyo kuwasili nchini kwa ajili ya kutoa matibabu ya afya kwa Watanzania.
mhhhh????!!!!!
ReplyDelete