MATOKEO RASMI YA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO BAADA YA UCHAGUZI MKUU YANATARAJIWA KUTANGAZWA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA KATIKA VIWANJA VYA KARIMJEE JIJINI DAR.
WAGOMBEA WOTE ISIPOKUWA DK. WILBROAD SLAA WA CHADEMA BADO HAJAINGIA HADI SASA WAKATI SHUGHULI INAANZA SASA.

WALIOWASILI TAYARI NI WAH. KUGA PETER MZIRAY/ APPT - MAENDELEO, KIKWETE JAKAYA MRISHO/CCM, LIPUMBA IBRAHIM HARUNA/CUF, RUNGWE HASHIM SPUNDA/ NCCR-MAGEUZI, MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT/ TLP NA DOVUTWA YAHMI NASSORO DOVUTWA/UPDP

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. UKISUSA WENZIO TWALA

    ReplyDelete
  2. Ulikuwa uchaguzi wa chama kimoja?

    ReplyDelete
  3. Itafahamika2

    ReplyDelete
  4. Hata kama kajafika huyo slaa rais lazima atangazwe akisusa lakin habari ndio hiyo hongera sana rais jakaya mrisho kikwete kwa kuwapuruza wapinzani

    ReplyDelete
  5. Labda kawa mhehe, sasa angoje Mheshimiwa aapishwe kisha alete zake za kuleta, kumbukeni hiki ni kipindi cha lala salama hiki. Mtu anakosa hata ustaarabu? Hata kama ukisusia matokeo ndiyo hatatangazwa? Vijana wanakudanganya hao shauri yako, hakuna Mtanzania mwenye kupenda amani atakuunga mkono upuuzi wako, unataka ushinde hata mahali hukuweka wagombea?

    Mimi wasi wasi wangu mkubwa ni kuwa huyu mtu amewaahidi nini watu waliogharamia kampeni yake? Sasa wanashurutisha lazima aende Ikulu kwa nguvu huko Ikulu anataka kwenda kufanya biashara gani?

    ReplyDelete
  6. WEWE MASANGU MATONDO UNAPATA WASIWASI GANI WAKATI AMESEMA BAYANA KUWA CHADEMA HAITAYATAMBUA HAYO MATOKEO.

    ReplyDelete
  7. J.k Congraduation but you need to work hard 61 % iS (D-) ????

    ReplyDelete
  8. Hongera Kikwete kwa kuwa raisi wetu na ombi langu kwa mheshimiwa raisi ni kwamba miaka mitano ilyopita hatujaona chochote cha msingi sana toka kwake lakini kwa sababu watanzania wanaamini kwamba unaweza ukafanya zaidi ya hapo jipange kutuletea baraza lenye tija na la watu wawajibikaji.
    Kwa upande mwingine, Slaa amenisikitisha. nasema hivyo kwa sababu kwa mtu yeyote mwenye uelewa wa kawaida na asiye shabiki wa vyama anajua kwamba Slaa asingeshinda hata kama angepewa kula zote ahesabu yeye na mkewe.Kutuletea kiburi cha kijinga namna hii na kutoka kwa mtu ambaye anahisi anajua democrasia is absolutely non sense.Democrasia inamaanisha yeye kuwa raisi at any cost?hata ikiwa ni kumwaga damu?je pamoja na matatizo yote tuliyonayo mtu anayehubiri maendeleo na huduma zote bure, is it feasible kurudia uchaguzi kama anavyotaka yeye?na akishindwa tena we need to do it again?
    na pia kwake yeye kama anafikiri vizuri, then ni kitu ambacho kiko wazi kwamba hata katika majimbo mengi ambayo upinzani imechukua, sio kwa sababu upinzani au chadema kina nguvu au kimekua sana, ni kwa sababu ccm wamewaboa watu katika majimbo hayo thats why he was still not peoples choice.
    guys we can talk, but only if we talk the reality.
    ciao

    ReplyDelete
  9. SO kama chadema hawatayatambua matokeo so what? Ndio nchi italala usingizi? Kwa miaka mingapi CUF ilikuwa haiyatambui matokeo je ilizuia serikali kuundwa? Tena afadhali hata hao CUF walikuwa na tofauti ndogo ya 1 au 2% seuze nyie gap kubwa utafikiri uwanja wa mpira?

    Mlichotabiriwa na hata wachunguzi wa siasa wa kutoka nje ndicho mlichokipata hakuna mtu huko nje atawasikiliza kwanza wenyewe wako taabani wanahangaika na hali ngumu za uchumi kwenye nchi zao.

    Grow up and stop sulking!

    "SAUTI YA WATU SAUTI YA MUNGU IMEONGEA"

    ReplyDelete
  10. Kwa ufupi Watanzania walio wengi bado wako kwenye enzi ya mawe.Vyama vya upinzani vina kazi kubwa sana ya kuwatengeneza akili zao na kuwaleta kwenye ulimwengu huu mpya.Tuko karne ya21 lakini badala ya kwenda mbele tunaendelea kurudi nyuma. mambo ya ajabu leo hii ni miaka 49 tangu tupate Uhuru lakini kuna mtanzania ambaye anaishi mjini tena Dar hajawahikufungua maji kwenye bomba.hawezi kutumia umeme maana ni wa mgao.Naamini 95%ya Watanzania hawana uhakika wa maisha.Lakini Serikali haiwajali wananchi wake. lakini cha ajabu na kushangaza haohao wenye shida ndiyo wa kwanza kuipigia kura CCM Nahao wanaopinga CCm ukiangalia wengi wao hawana maisha mabaya. Hivyo basi, lazima CCM itashinda.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...