Wafanyakazi wa TBC One wakimpongeza Mh. Juma Nkamia, Mbunge wa Kondoa Kusini walipokutana viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo
Mbunge wa Kilosa Mh. Mustafa Mkullo akipiga stori na wabunge wa viti maalumu Mh. Angela Kariuki (shoto) na Mh. Zarina Madabida leo mjini Dodoma

Mbunge wa Bumbuli Mh. January Makamba na
Mbunge wa Singida mjini Mh. Mohamed Dewji wakibadilishana mawazo leo

Mbunge wa Njombe Kusini ambaye pia ameteuliwa kuwania nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anna Makinda akisalimia na Mbunge wa jimbo la Muleba kusini (CCM) Prof. Anna Tibaijuka leo katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma. Waziri Mkuu wa serikali iliyopita Mh. Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya wabunge mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma.Kutoka kulia ni Mbunge wa jimbo la Mtera Livingstone Lusinde,John Magufuli jimbo la Chato na Dk. Emmanuel Nchimbi wa jimbo la Songea mjini. Mwenyekiti wa TLP na mbunge wa Jimbo la Vunjo Mh. Augustino Mrema akijaza fomu za usajili wa wabunge mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Bunge mjini Dodoma leo.


Mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini Steven Ngonyani a.k.a Profesa Mji Marefu, akisalimiana na Mh. Vita Kawawa mbunge wa jimbo la Namtumbo na Mh. Zainabu Kawawa, mbunge wa CCM Viti maalum (wafanyakazi) nje ya Bunge mjini Dodoma leo.


Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini kupitia CHADEMA Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu ama Mr II akitaniana na waandishi wa habari alipowasili kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo.


Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ) Dkt. Willbroad Slaa akisalimiana na baadhi ya wabunge mara baada ya kuwasili katika viwanja vya bunge mjini Dodoma kwa shughuli za Chama hicho.



Juu na chini ni Wah. Wabunge wa CCM wakiwasili ndani ya Ukumbi wa Pius Msekwa kwa ajili ya kuchagua jina moja la mgombea atakayeingia katika kinyag’anyiro cha nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo asubuhi mjini Dodoma


Picha na Anna Itenda na Aaron Msigwa - MAELEZO na John Bukuku












Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Hahahahaha Sugu maswala ya Tai kufunga yanamtia chenga hahaha. MZ

    ReplyDelete
  2. mamie Anna tuko nyuma yako. Hongera sana.

    ReplyDelete
  3. Ushauri nasaha kwa wabunge wote-nendeni kuongelea maswala ya maendeleo ya nchi msilete uvyama vyama wenu huko.

    ReplyDelete
  4. Mdau/anon. wa kwanza,hiyo ni style tu mwana. Usiogope wala nini. Ndo mambo hayo silazima ujikabe kama ujuavyo wewe!

    ReplyDelete
  5. Kama tunavyoona kwenye picha tayari CCM imeanza uvyama ndani ya bunge, haya sasa sijui mpinzani gani safari hii atafukuzwa bungeni. Hivi hakuna kanuni inayokataza uvaaji wa jezi za vyama ndani ya bunge?

    ReplyDelete
  6. KIBONDE, ULIYEMBEZA HUYOOOO NAJUA KWAKUWA SI MWANACCM KWAKO UNAMUONA HAFAI LAKINI YUMO SIJUI UTAGOMA KUMUITA MHESHIMIWA KWA SABABU YUKO CHADEMA AU VIPI! DUA LA KUKU HALIMPATI MWEWE.

    ReplyDelete
  7. mdau wa Nov 12 saa 08:34 AM hao wana CCM walikuwa kwenye kikao chao cha chama hizo ni taratibu za Bunge ktk kutafuta mgombea Uspika. Kila chama kilipewa nafasi ya kukutana kuchagua mgombea wao. Na huo ukumbi ni wa Bunge lakini ni ukumbi wa zamani si huu wa sasa unaotumiwa kwa shughuli za Bunge.

    ReplyDelete
  8. Hujaweka comment yangu kwasababu na wewe ni mmoja wao. Nikija Tanzania naanza na wewe. Nikufundishe adabu

    ReplyDelete
  9. hahahaha Mdau nimekupata sawa nitaanza kuregeza Tai au kwaujumla nitaanza kuvaa tai na kuregeza sababu mie si mvaaji Tai. Nishazoea Shati langu na suruali.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...