Hello Ankal Michuzi,
Ni jana tu ambapo niliomba uniwekee tangazo langu juu ya kumtafuta rafiki yangu Lucas Alfred niliyepotezana nae takribani miaka kumi iliyopita na kujaribu kumtafuta bila mafanikio yoyote.
Sasa basi naomba kuchukua fursa hii kwanza kukushukuru kwa kuitikia wito wangu na kuniwekea tangazo langu na pia wadau wote walio husika kwa namna moja au nyingine ktk kunisaidia kumtafuta rafiki yangu huyu kwani nimempata na sas nina mwasiliano nae tena baada ya mda mrefu kupita. Mwenyezi Mungu na awabariki kwa ushirikiano wenu mliyo uonyesha kwangu na iwe hivyo na kwa wengine.
Asanteni sana.
Mdau UK
Mdau UK
Ahsante Mdau wa UK karibu tena. Hii ni blog ya jamii na ipo kwa ajili ya jamii!!
ReplyDelete