maoneo ya Bahi
Dodoma inanukia...
kilomita kama 2 kuingia Dodoma.
Chuo kikuu cha University of Dodoma kileeeee... kule juu.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. alafu kuna wapumbavu wakishashiba maharage yao wanasema JK hajafanya kitu,JK amejenga barabara nyingi mno,na kama akiendelea hivi mpaka 2015 atakuwa amejenga barabara mara 3 ya mkapa

    ReplyDelete
  2. “Tayari mchakato wa kumtafuta Rais mpya baada ya Kikwete 2015 umeanza na ujue Bunge hili litakuwapo hadi uchaguzi ujao na hivyo lazima wanasiasa wanaowania nafasi hiyo wahakikishe wanamsimika Spika atakayerahisisha malengo yao kutimia,”

    ReplyDelete
  3. Mi ni mmoja wa wapumbavu ambaye nasema JK hajafanya kitu. Shida sijashiba maharage manake kwa Mkapa yalikuwa 500 kilo sasa hivi duu! Labda ndio mambo ya kuongezeka pengo la maskini na tajiri, wengine tunaona mambo ni magumu zaidi.

    ReplyDelete
  4. zitto-kiaratuNovember 14, 2010

    wengine tukishiba maharage ndio akili inafanya kazi, imagine vijisenti vinavyoibiwa kila siku vingetumika kusaidia wenye inchi katika kuboresha ahali zao, nadhani ungeshiba maharagwe ungejipunguza migrane.

    ReplyDelete
  5. Yaani natamani kuja Bongo na kusafiri kuona nchi maana sijafika Mwanza, Moshi, Arusha hata Bukoba ningekwenda..na vile vile kutumia hivi vijisenti tunavyopata kwa kupiga boxi. Lakini hapo bwana mara tu anatoka mtoto wa tajiri anaendesha lori anaua watu.. Maana barabara za bongo hata tukiwa tunakuja huko, wanatuonya kuwa tukae chonjo barabara zinaua.. basi mtakosa dolari zetu maana hatutamani kufa jamani.. jifunzeni kuendesha kwanza, looh!! Barabara zinaua kama ukimwi!!
    Mdau, Ughaibuni.

    ReplyDelete
  6. Hakika ukishiba maharage unakuwa na fikra tunduizi na unang'amua kuwa barabara hii haikujengwa na JK bali Mkapa. Mradi wa barabara hii ulianzishwa na kusimamiwa kikamilifu na Magufuli enzi za Mkapa na ni sehemu ya barabara ya kutoka Mtwara hadi Mwanza. Maharage yanasaidia kutambua haya. Pole kwa wewe usiyeshiba maharage.

    ReplyDelete
  7. Wahamiaji haramu wana shida sana. Pamoja na kubaguliwa kote bado wanadiriki kudharau nyumbani kwao. Taabu kwelikweli.

    ReplyDelete
  8. Takwimu za ujenzi wa barabara Tanzania zinaonyesha kuwa urefu wa barabara zilizojengwa kati ya 2005 na June 2010 ulikuwa mkubwa kuliko kati ya 1995 na 2004. Tafadhalini check na Tanroads data zote ziko wazi. Ifikapo June 2011, barabara za Arusha to Namanga na Tanga to Horohoro zitakuwa zimekamilika na chadema bado wataendelea na kampeni zao za uongo na chuki. Chuo Kikuu cha Dodoma kitaanza kutoa maelfu ya graduates wenye BA (Ed) na BSC (Ed) baada ya miaka miwili ambao wataajiriwa katika shule zaidi ya 2,000 za sekondari zilizojengwa katika miaka mitano ya kwanza ya uraisi wa mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete lakini wanachuki bado watakuwa na upofu wao wa giza la chuki. Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki Rais Kikwete. Amen.

    ReplyDelete
  9. Huo ni mwanzo tu, wajasiriamali jipangeni PRIDE (mkopo wa riba nafuu chini ya 5% kwa mwaka) imepewa shingi BILIONI KUMI na srikali ya JK kuendeleza wajasiriamali wanaojituma kuboresha maisha yao. Wavivu siku zote wataendelea kutafuta mtu wa kumlaumu kwa uvivu na uzembe wao. JK juu zaidi!!!!!!! (Mimi Dua za kuku hazimpati mwewe).

    ReplyDelete
  10. JK ametekeleza 83% ya ahadi zake kati ya 2005 na 2010. Sababu iliyompa mafanikio hayo ni kutoa ahadi zinazotekelezeka. Kuna wanasiasa wengine wanatoa ahdi bomu kama yule mzee fulani bin fulani aliyesema eti "ohh sijui ndani ya miaka mitatu nitafuta kodi na kila mtu katika kila kijiji atakuwa na maji na umeme na ohh Tz itakuwa nchi peke duniani yenye 100 percent elimu na afya bure, saruji na mabati yatauzwa bei ambayo ni chini ya gharama za uzalishaji wake na alnach lukuki". Naona kwa kuwa uchumi wa dunia unatarajiwa kuimarika baada ya miaka miwili safari hii JK anaweza kutekeleza zaidi ya 95% ya malengo wake. WATZ tuko naye. Mangelepaa.

    ReplyDelete
  11. duh barabara nshakatiza sana hii enzi hizo za mivumbi,sasa mkekahuu mtuy unapata hata hjamu ya kusafiri.itabidi nikitua lazima nizue ki tripu nikawasalimie wajomba.

    ReplyDelete
  12. 1.sijui kama ni mimi ila kusema ukweli bongo mambo ni magumu sana.wachumi wameshindwa kuhandle mfumuko pesa inaelekea kuwa zimbabwe.nadhani walioko pale hawaoni ila mimi nilikuja juzi juzi baada ya miaka minne tu niliona hali ni ngumu hata kwa kutumia fungu la box.
    soda mia tano?? mara mbili tangu nikimbie.laki moja mfukoni is nothing na subirini kima cha chini kiwe sijui laki tano.

    jamani kukamata pesa mbona ni easy.kumbukeni mkapa pamoja na kuibuka mafisadi nyangumi aliweza kutangaza mikanda kufungwa na kweli pesa ilisound kwa kiwango fulani.

    Tanzania inahitaji jamani uongozi thabiti wenye kuwa very efficient ,transparent ,commited,na kuwa strict katika kusimamia mambo yake na si kuendesha vichwa vya mafisadi kama familia.

    Tanzania inahitaji msimamo kama wa kagame na nchi inaweza kutake off dunia ikashangaa.sichafui hali ya hewa ila sisi tuna siasa za chuki kukomoana kutaka utajiri kirahisi rahisi kutokuwa na huruma na kizazi kijacho wala umaskini wa jamii.

    mkuu wetu wa kaya anakuwa na vision na machungu ila ajue kuwa anahitaji kusimama bila kuona haya na si yeye anaetakiwa kufanya kila jambo ila wafuasi wake waweze kuogopa na kuheshimu pale anapokemea wakati umefika kila mtu awe na uchungu na nchi yetu .

    ReplyDelete
  13. Mie Nimeshiba kunde ila kiukweli hii barabara ni kwaajili ya kuwarahisishia wao tu kuwahi dar dom kila siku na kuongeza marupurupu ya vikao hakina lolote( michuzi kada wa ccm nibanie bana)

    ReplyDelete
  14. We Anon wa kwanza kabisa nafikiri ndo umeshiba maharage...kwa maana ya kwamba ukishashiba unaona kila kila kinaenda sawa.
    Ebu angalia shilling inavyopolomoka kama maji.. Hata kama JK angekuwa amejenga barabara mpaka kijijini kwetu Mpanda bado hali ya mwananchi wa kawaida ni ngumu sana.
    Ukweli ni kwamba serikali zetu bado haziwezi kupanga na kutekeleza sera za umma au nisema hawajui zinafanyaje kazi, ukiweka na rushwa ndo basi.

    ReplyDelete
  15. Michuzi ee labda wewe ndo umeshiba mabeans.Bongo hali ni ngumu mno.kujenga vyuo hakutoshi bila kuhudumia wanaovitumia mwenye mtoto chuo ataniunga mkono.watoto wanaahidiwa pesa asilimia 80 wakifika chuo wanapewa vi hela wanashindwa hata kujua wanadai nini au wamepewa nini.hali ni ngumu jamani vyuoni.hasa mzumbe watoto hawaruhusiwi kudai chao.hiyo hela ni mkopo watarudisha hivyo lazima wapewe ili wajiandae vema. watoto wa kike wana hali ngumu pocket money wanategemea toka kwa wazazi.mzumbe wakidai wanaambiwa wao wanafuata kanuni huku wao wamelala njaa wenye watoto mzumbe tumechoka kwani mtoto huanza chuo akiwa na uhakika ila mzigo unarudi kwa mzazi.

    ReplyDelete
  16. Hivi Dodoma kuna University? Ilianza lini?

    ReplyDelete
  17. Dodoma miji mkuu wa Tanzania ambao mpaka leo halijawa jiji, umezidiwa mpaka hata na Mbeya!!! Ama kweli wanasiasa wabaya, wanakula (wanafanya ufisadi) kwa jina la kustawisha makao makuu miaka yote hiyo!!! Mtajahukumiwa baadaye!!!

    ReplyDelete
  18. Dodoma imekuwa sana ukilinganisha na enzi za mwalimu, dom is beautiful, reli ya kati inapita kati-kati ya mji. Tunahitaji miradi ya kuwapa wakazi kazi, kama hawa wabunge wangeachana na kuendesha hizi cruiser ghali labda wenye inchi tungeambulia makombo ya kutoka juu/serikalini, pia mwenye hela kama ukijenga ki guest-house cha maana unaweza ukashiba pesa, kiwanda cha matofali ya kuchoma zuzu kinahitaji ujasirimali kidogo. msomali wa dom

    ReplyDelete
  19. university of dodoma ni mafanikio ya JK,graduate kibaaaaao kwa mwaka ukilinganish na UD mbayo haitaweza kukifikia,yaan kitafunika east africa,.bravo JK nadhan baada ya 2015 tukupe tena 10yrs ujenge nchi

    ReplyDelete
  20. Tunawakaribisha Dodoma Watanzania wote. Siusifii Dodoma kwa kuwa ni mji wangu tu, lakini kwa kweli katika miaka mitano hii miundombinu ya Dodoma imeboreshwa sana. Ukitaka kujua ukweli njoo mwenyewe ujionee, si kuambiwa na watu ambao hawajawahi kufika hapa hivi karibuni. Kama wanavyosema Waingereza "Seeing is believing". Saulo Boma.

    ReplyDelete
  21. Tukumbuke kuwa ifikapo March 2011, barabara ya Dar es Salaam -Bujumbura itakuwa lami tupu, kwa hivyo Warundi wa Dar hamtakuwa na haja ya kulipa US$ 450 kwenda Bujumbura, gharama itakuwa mara kumi nafuu na ndani ya masaa 36 baada ya kutoka Dar utakuwa unatafuna ndagala (dagaa) Bujumbura town huku ukitazama jua linatua Ziwa Tanganyika. Yego!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...