Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama Cha Demokrasia na Maendeo (CHADEMA),Mama Leticia Ghati Mosore akizungumza na waandishi wa habari waliofika leo katika Makao Makuu ya Chama cha NCCR - Mageuzi kumsikiliza akitangaza nia yake ya kukihama chama cha CHADEMA na kujiunga na NCCR - Mageuzi.Mama Leticia ameamua kujitoa katika chama cha CHADEMA na kujiunga NCCR Mageuzi kwa madai kwamba amechoshwa na taratibu nzima za uongozi wa juu wa Chama hicho na kutopewa umuhimu wa cheo chake katika shughuli mbali mbali za kichama zikiwemo za Baraza la Wanawake ambalo yeye ndio Mwenyekiti wake.
Mwenyekiti wa NCCR - Mageuzi Taifa,James Mbatia akisisitiza jambo mbele ya wamahabari waliofika leo katika Makao Makuu ya Chama hicho wakati wa kumkaribisha mwanachama mpya katika chama chake ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama Cha Demokrasia na Maendeo (CHADEMA),Mama Leticia Ghati Mosore(kushoto).
Mwenyekiti wa NCCR - Mageuzi Taifa,James Mbatia akimkabidhi kadi ya uanachama aliekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama Cha Demokrasia na Maendeo (CHADEMA),Mama Leticia Ghati Mosore (katikati).anaeangalia kushoto ni Mjumbe wa NEC wa NCCR -Mageuzi,Danda Juju.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Usanii mtupu!

    ReplyDelete
  2. mama sema mama, wamekunyima viti maalum nini? ungeingia kwa mlango wa jimbo.

    ReplyDelete
  3. hata akiondoka haitutishi kitu, chadema tupo pale pale mwendo mdundo mpaka kieleweke , mtu mzima hatishiwi nyau....

    ReplyDelete
  4. Sasa sijui Bi mkubwa unakihama chama labda hujachaguliwa kuwa mbunge viti Maalum au ERABORATE BI MKUBWA

    ReplyDelete
  5. Mmeshaanza mlitaka mpewe ubunge wa viti maalum mmekosa sasa mnaanza kuhaha. Wakati wa uchaguzi hamkuonekana popote kukisaidia chama leo kwenye matunda mnasogea.ASIYE FANYA KAZI NA ASILE!!!!

    ReplyDelete
  6. Huyu mama alikuwa anatafuta Ubunge wa vita maalum kakosa ndo maana ameondoka kwa hasira na kusingizia vitu vingine. Mama pole sana hizi ndo siasa sio kila kitu lazima upate vitu vingine vinahitaji uvumilivu.

    ReplyDelete
  7. Pole mama Leticia! Hukujua kama sio mwenyeji wa nanihii hutapata keki ya Chadema?

    ReplyDelete
  8. Mzee wa BusaraNovember 22, 2010

    Mama kweli bora uhame, yaani ubunge umepita machoni pako hivi hivi.... Kweli hata mimi sikutegemea uendelee kuwa mwanachama wa hicho chama tena..

    ReplyDelete
  9. Watu kama hawa sio wa kuaminika kabisa na wala hawajui maana ya vyama vingi. Ukiwa mwanachama wa chama fulani ni kwa ajili unaamini sera zao sio kwa sababu ya wadhifa ulio nao wala nini? Wee unataka watu wakutafunie kabisa wewe umeze tu. Na huko tukupe miaka mingapi?

    ReplyDelete
  10. Ukitaka kujua kasoro kubwa za chadema...wape nguvu. Yani kupata nguvu kidogo mambo kibao yanajitokeza.

    Timu ya upinzani hawajausisha vyama vingine !!

    Mara Slaa hamtambui raisi lakini Mbowe anamtambua...

    Eti wote walikubaliana kutoka nje raisi akianza kuutubia, mara Zito anasema hapana wengine walikataa....

    eehe Chadema utawala wa juu ni mbovu na wengi wao wako kwa maslahi binafsi....Hakuna cha ajabu hapo

    Viti maalum hawakufata demokrasia ya kweli kama wanavyojiita...matokeo yake ndio haya.

    ReplyDelete
  11. WEE MAMA UKABILA UMEUONA JANA? SIKU ZOTE ULIKUWA NA MAKENGEZA ILA BAADA YA KUUKOSA UBUNGE VITI MAALUM NDIPO UMEUONA UKABILA/ SIJUI NA WEWE NI MCHAGA? HIVI MBOWE, ZITO, SLAA HAWA WOTE NI WAMACHAME AU WAROMBO AU WAMARANGU? ANADAI PIA KUWA UMEDHARALISHWA NA MBOWE KWA VIPI MAMA USIJE UKAJIPA KESI KWANI MAHAKAMANI UTAKUWA PEKE YAKO NCCR HAITAKUTETEA. NINAMSHAURI MBOWE UKUFUNGULIE KESI YA MADAI ILI UKATUTHIBITISHIE MAHAKAMANI NI JINSI GANI ALIKUDHALALISHA,KWANI MADAI YAKO YANATULETEA HISIA MBOVU JUU YA MBOWE.

    ReplyDelete
  12. Njaa hiyo inakusumbua mama, kwa mwendo huo utahama sana, nenda hatuhitaji watu wenye uchu wa madaraka kwenye chama chetu...

    ReplyDelete
  13. Mama ninakuelewa ingawa japo hapa kuna kasoro kidogo. Inabidi tujiulize mambo kama haya:
    1. kweli wote hawezi kupata ubunge kwani viti maalumu viko limited!
    2. Si rahisi kumuridhisha kila mmoja. Na ifahamike chama kinahitaji watu wengine ambao si wabunge ili waweze kukijenga. Kuna kazi za utawala nk. Kwa nafasi yako ilitakiwa uendelee kusaidia kukijenga chama. Kama ni ubunge basi ni baada ya muda fulani wakati tumewapata watu wenye sifa kama zako ili washike nafasi yako ili wewe utafute ubunge.
    3. Inabidi tuelewe process ya kujenga chama kikawa imara ni ndefu na wakati mwingine kwa watu wanaotaka vyeo inakatisha tamaa. nafikiri hapa ni rahisi kuona nani anataka kujenga chama kwa kujituma na wala siyo kufizia vyeo. Kwa mwendo kama huu hatufiki mbali.
    4. Kama ni kuhama basi hata chama tawala wangehama wengi. angalia uchaguzi wa kwanza wa ccm. watu wangapi wameachwa lakini wanaendelea kubaki na kufanya kazi zingine za utawala.
    5. Kuwa mchapakazi wa chama siyo lazima uwe mbunge. Kama watu hodari wakiwa wabunge nani atajenga chama?
    6. Kuhama chama kwa sababu kama huzi nafikiri kwa hapo baadae hata CHADEMA haitawapokea watu kama hawa!!
    7. Anagalia mifano ya wenzetu kama ujerumani, uswiss, uingereza nk. Chama wakati mwingine kinachukua zaidi ya miaka 10 ili kujijenga ili kurudi na kuchukua serikali. Ni wakati huo wanachama wanashikamana na kutafuta makosa ya serikali ili kuweza kuyatumia ili kujijenga.
    8. Watu wengi wanaopenda kuhama vyama kama mama Cecilia nafikiri wana kasoro fulani. Ni kweli makosa yanaweza kutokea katika uteuzi wa nafasi fulani lakini hiyo isiwe sababu ya kukata tamaa na ktoa siri za chama kwa manufaa ya vyama vingine. Je huko unapokwenda unajua wapi kama matatizo kama hayo hayawezi kutokea?

    USHAURI WANGU KWA CHADEMA NA VYAMA VINGINE:
    Kwa wanachama wanao hama hama nafikiri kabla ya kuwapokea ni lazima kuwaangalia kwa kipindi fulani kabla ya kupata uanachama kamili. Wengine ni kama hawajaiva kisiasa na wanatumia vyama vya siasa kama njia ya kutafuta ajira ya haraka! Ni sawa ajira ni muhimu kwa kila binadamu lakini ajira katika vyama vya siasa ina utaratibu wake. Sioni kweli mtu mwenye kukubali sera za chama chake pamoja na kuwa amejituma ahame chama kutokana na sababu kama alizozitoa mama Cecilia. Nakuomba urudi tena kwa Chadema kwani milango yako bado imefunguliwa.

    Ahsanteni, na Mungu ibarike Tanzania.

    ReplyDelete
  14. Hata mimi natoka chadema na kumfuata mama Leticia NCCR Mageuzi. Viva NCCR MAGEUZI!!!! VIVA!!!!!!!!Tesha79.

    ReplyDelete
  15. Heeeee!!!!! mbona wanakyadema mmekuwa mbogo hivi. Watu walipokuwa wanatoka vyama vingine kuingia kyadema mlikuwa mnawasifia. Sasa watu wameanza kutoka kyadema kwenda vyama vingine mnawatukana na kuwakashifu. What is good for the gander is good for the goose. Anzeni kuzoea hali hii. Free advice: chadema wacheni matusi, kwa sababu mtatukana sana na hamtawazuia watu kutoka chadema kwenda vyama vingine!!! Hiyo ni demokrasia. Just get used to it!!!!

    ReplyDelete
  16. Chadema nawashauri muache matusi na muanze kutazama mapungufu yenu, hasa jinsi mlivyovunja muafaka mlioufikia May 2010 na vyama vingine vya upinzani na ukorofi wenu unaoanza kuwaboa hata wanachama wenu wengi. Kikulacho ki nguoni mwako.

    ReplyDelete
  17. Huu ni mwanzo tu! Laiza.

    ReplyDelete
  18. Karibu mama yetu NCCR, chama pekee cha upinzani chenye principles. nccr4lyfe.

    ReplyDelete
  19. UTAMALIZA MABUCHA SHOSTI.....NYAMA NI ILEILE.......Lol umechemsha!!!

    ReplyDelete
  20. hata hututishi, kwani tunajua miaka si mingi tutakuona tena unazungumza na waandishi wa habari ukitangaza kuhama NCCR ukikosa viti maalum.uchu wa madaraka utawaponza wengi, kama huna vigezo hata huko hutapeawa hivyo viti maalum othrwise jitose jimboni usingojee vya kuteuliwa, ala?!

    ReplyDelete
  21. Dalili za Malaria huanza na Homa, au kutapika au kuha... na dalili ya kuishiwa mafuta mlimani utazijua tu gari itakapokuwa imeanza kuinama, sasa nyinyi Kyandema mmeishiwa mafuta na breki hakuna, maana kila mlipopita mlitaka kushinda jamaa wengine wakichukua mnaona wamechakachua, sasa inakula kwenu mdogomdogo... mtakuwa kama NCCR kipindi kileee sasa kikafulia na nyinyi hamtimizi 2yrs mtakuwa mnaanika, watabaki wabunge vimeo ukitoa Zitto na yule aliyetoka CHICHIEM...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...