Mfungaji wa mabao mawili ya Zanzibar Heroes, Salum Shiboli akishangili bao la pili la timu yake.
Beki wa Zanzibar Heroes, Rashid Faki (kulia) akichuana na mshambuliaji wa Sudan, Ramadan Shareif ferein katika mechi iliyochezwa leo katika uwanja wa Taifa.Zanzibar Heroes imeibuka kidedea kwa kuichapa Sudan bao 2-0.
Nahodha wa timu ya taifa ya Rwanda (kushoto) akiwa na mwenzake wa Ivory Coast kabla ya kipute kuanza kupigwa.
Kipa wa Rwanda, jean Ndayishimiyei akiokoa moja ya hatari langoni mwake katika mchezo uliopigwa leo ndani ya dimba la Taifa.mpaka mwisho wa mchezo Rwanda waliibuka kidedea kwa kuichapa Ivory Coast 2-1.
Wachezaji wa Zanzibar wakishangilia baada ya kumalizika kwa mchezo wao.
Brass Band ya Polisi ikipiga nyimbo za Taifa wakati wa mchezo wa Rwanda na Ivory Coast. Picha na Francis Dande wa Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Kumbe Tanzania watu hawapendi mpira, yani kiwanjani hakuna kabisa mashabiki, au waliweka kiingilia kikubwa sana.

    Hongereni Zanzibar kwa kushinda.

    ReplyDelete
  2. Haya wale wanaosema zanzibar mdebwedo mambo ndo hayo hapo sisi hatuongei sana ila vitendo tu. hao wamedhaminiwa milioni tisa tu.Nyie mnadhaminiwa na viwanda vya pombe ufisadi mtupu

    Hongera wazanzibari

    ReplyDelete
  3. hongera ndugu zetu wa zanzibar lakini cha kusikitisha uwanja mtupu.

    ReplyDelete
  4. Katika nchi nyengine bei za viingilio hupunguzwa sana ili uwanja ujae na hata huwapa tiketi za bure wanafunzi wa mashule ili kuwepo na shamra shamra uwanjani kuliko kuwepo na viti vitupu.

    Alieuliza kama tanzania hatupendi mpira, jawabu ni kuwa tunapenda lakini bei zinatushinda ndugu yetu!!!!

    ReplyDelete
  5. kama wa zenchi wanaweza kufundishika kwa nini sio wa bara? wa zenchi wanaumoja sana , wabara fitina nyingi.

    mdau paris

    ReplyDelete
  6. kuna mtu mwenye majibu ya kwa nini uwanja mtupu?

    ReplyDelete
  7. Nilisema ndugu zetu wa bara si kwa mpira koment zangu zikafutwa. Nasema tena bara ni kwa kuimeza Zanzibar tu si kwa kitu chengine ngojeni wazenji wakuonesheni mpira.

    ReplyDelete
  8. Mbona uwanja mtupu ama tunahitaji 'muafaka' kwenye michezo ndio mambo yakae sawa.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  9. mdau wa Mon Nov 29, 12:00:00 AM jawabu ni tumbo joto. Bei ni ghali mno kwa mlala hoi, plus haikuwa brazil uwanjani kwa hivyo vigogo na wakurugenzi hawakupanga foleni kudemand tiketi za bure,

    ReplyDelete
  10. Duuh! Uwanja huo enzi zetu ulikuwa unajaa kama nini. Naongelea miaka ya 90's. Tenga and Co inabid ku hire marketing guru awasaidie.

    ReplyDelete
  11. Kwa kweli CECAFA inabidi mjiulize kwa nini viwanja viwe tupu wakati wa mechi. Ni bora kuweka hata viingilio vya jero na buku angalau sura za watu zionekane humo. Mechi ina mashabiki wachache kuliko hata ashanti ikicheza na opeki hapo temeke.

    ReplyDelete
  12. hongera saana amavubi club jitaidini vijana hilo kombe mlipeleke home rwanda maana zamani lilikua linaitwa kagame cup kama sikosei.. rwanda juu juuu zaidi.

    mdau kigali makazi boksini kusaka chake

    ReplyDelete
  13. Jamani uwanja kuwa mtupu hivi inatia huzuni sana. Yaani ndiyo ile tukiita challenge kapu hii?! Au Tenga kasahau tulinyokuwa tukijazana miaka ile kumuone yeye na wenzie wacheza challenge kapu pale neshno? Mafisadi kweli hawa.

    ReplyDelete
  14. mdau wa Mon Nov 29, 04:55:00 AM, hapana kombe hili huko nyuma tena nyuma kweli lilikuwa likijulikna kama challenge cup na likishindaniwa na timu za east africa ya kikweli, yaani zanzibar, tanzania bara, kenya na unganda peke yao.

    Mpiga boksi makini uk

    ReplyDelete
  15. UWANJA KUWA MTUPU WALA HAITAKI KUJIUMIZA KICHWA. TUJIULIZE KUNA TANGAZO LOLOTE LA MECHI KAMA HII ZIKIKARIBIA WANA PROMOTE KWENYE VYOMBO VYA HABARI??
    HII YOTE INATAKA SHULE ILI WAFAHAMU IMPACT YA PROMOTION KWENYE VYOMBO VYA HABARI. NA HII NDIO ITAPELEKEA KUINUA STANDARD YA MPIRA TZ. MTU ANAWEZA AKAULLIZA PROMOTION NA KIWANGO CHA MPIRA INA LINK GANI? HILO NI JIBU UKAE LITAFUTWE.

    ReplyDelete
  16. "...kuna mtu mwenye majibu ya kwa nini uwanja mtupu?"

    Jibu: Kwa sababu uwanja ni mtupu!

    ReplyDelete
  17. MTOA MAONI Mon Nov 29, 02:06:00 PM, Naona huna data hili kombe zamani liliitwa Gossage na lilishirikisha Tz, zenji, kenya, ug, malawi Zambia pia na Sudan mpaka Somalia, badaye chalenji mpaka miaka ya 90 zambia na malawi zikajitoa na kwenda COSAFA, SIKU ZA KARIBUNI KUMEKUWA NATABIA YA KUAALIKA TIMU TOKA NJE YA CECAFA KAMA ZAMBIA NA IVORY COAST MIAKA YA MWISHONI MWA 90 NDIO RWANDA NA BURUNDI ZILIJIUNGA NA BADAYE KOMBE KUITWA KAGAME CUP, HONGERENI ZENJI INGAWA MIMI MBARA WAKOME HAWA NA WANAFUNDISHWA NA KOCHA WA MUUNGANO LAKINI OOOOVYOOOOO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...