Ndugu Ankal!

Tunashukuru kwa kuweka kwenye mtandao wetu huu wa jamii ile jumatatu Kero ya jinsi uchafu ulivyokuwa umeachwa majumbani kwetu Sinza kwa zaidi ya mwezi na wiki kadhaa. Hatimae, nadhani wahusika walisikia kilio chetu kwa kupitia Globu hii ya Jamii. Jana matakataka yamezolewa na saa hizi tunafurahi kuwa tunaingia mwaka mpya na harufu safi. Tunaomba adhabu ya kuachiwa matakata isirudie tena kwa mwaka huu mpya wa 2011.

Tunamshukuru Mungu kero hii imetoka na tunaomba isirudie tena. Nadhani kuna uongozi wa juu uliliona hili na wahusika wakalifanyia kazi. Katika maoni kulikuwa na malumbano makubwa ,lakini yote yalilenga katika kujenga na sio kubomoa.

Wana Sinza kwa Wajanja Hoyeee!!! Mungu atubariki sote tuanze mwaka mpya 2011 kwa furaha na Shange na Mafanikio mengi. Harufu Mbaya MWIKO!

Libeneke Oye!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. watanzania huwa hawana moyo wa kujitolea,baada ya kuona taka haziondolewi mlitakiwa kila jumapili kufanya harambee ya kuzitoa hizo takataka hata kwa mikokoteni na kuzifukia sehemu nyinyi wenyewe hapo mtaani, ina maana hizo taka zisingezolewa mngeishi nazo milele majumbani kwenu? tanzania kila mtu anataka "white collar jobs"

    ReplyDelete
  2. Blog ya jamii hoyeeeeeeeee..............!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...