Mdau Bachalla akiwa na Bob Farell jijini Amsterdam
BOFYA HAPA

Na mdau Ughaibuni

Bobby Farrell (61) ambaye alikuwa mwanamziki mashuhuri katika miaka ya 1970s kutoka kundi maarufu enzi hizo Boney M, Mr.Bobby Farrell amekutwa amefariki dunia katika chumba cha hotel aliyofikia mjini St.Petersburg,nchini Urusi.

Mwanamziki huyo alikuwa katika ziara ya kimziki nchini urusi,maiti yake iligunduliwa katika chumba cha hotel aliyofikia baada ya kumaliza show zake.idara ya usalama ya mji wa St.Petersburg umeunda kamati maalumu kuchunguza chanzo
cha kifo cha Bobby farrell.

Marehem Bobby Farrell (61) alikuwa mwanamziki anayeongoza safu ya mbele ya iliyokuwa bendi maarufu duniani Boney M,ambapo alifanyakazi na wanamziki Maisie Williams,Liz Mitchel na Marcia Barret.

Kundi la Boney M lilijizolea umaarufu kila kona duniani kutokana na umahili wa nyimbo zake kutingisha katika madisco na redio za kimataifa, Kundi hilo lilikuwa na maskani yake nchini Ujerumani na kuweza kupiga tour katika kila kona duniani.

Baada ya kundi la Boney M kusambaratika marehem Bobby Farrell alihamishia makazi mjini Amsterdam,nchini uholanzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Rest in peace bobby

    ReplyDelete
  2. urusi nako kuna umafia sana, isiwe jamaa wamemuua,anyway rest in peace bobby farry umeturusha sana na bonny m enzi zako...

    ReplyDelete
  3. RIP Bobby!
    @ Thomas: Bobby alikuwa na matatizo ya moyo. Usiku wa kuamkia kifo, alikuwa ktk kazi (GAZPROM Cooperative Party) na alitumbuiza vizuri ila baada ya kazi akasema kuwa anajisikia vibaya. Malipo yake yalikuwa 15000Eur + cost (transport, accomodation etc) ambazo alilipwa mapema kabla hajafika Urusi. Hivyo sioni sababu ya kumuua.
    Blackmpingo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...