Kwa kutambua mchango unaotolewa na wasanii wetu katika tasnia ya filamu mtandao huu umeguswa na kazi za wasanii hawa na kuwatambua kwa kuwatangaza kulingana zoezi tulilokuwa tunaliendesha la BORA ZA 2010, wadau hawa wamechaguliwa na wapenzi wa filamu hapa nchini ambao pia ni wapenzi filamucentral ambao kila siku wanatembelea mtandao huu kwa habari za filamu za Swahiliwood. Gonga HAPA kuona matokeoTunawapongeza wale wote walioshinda na kuibuka washindi katika nafasi walizoshiriki, kila aliyeingia katika mtanange huu alikuwa ni bora lakini siku ya siku tuliitaji mshindi mmoja ambaye ndiye tunamtngaza leo hii, tumefarijika sana kwa ushirikiano mlioonyesha wadau wa tasnia hii toka mwazo wa zoezi hili hadi mwisho, tunapenda kuwatambua waliotikisa mwaka 2010 na kusema Hongera.
BORA ZA 2010
1. Msanii chipukizi bora za 2010 – HANIFA DAUDI (Jenifer)
2. Muigizaji bora wa kike — YVONNE CHERRYL (Monalisa)
3. Muigizaji bora wa kiume — STEVEN KANUMBA (Kanumba The Great)
4. Mwandishi bora wa mswaada – ALI YAKUTI
5. Mchekeshaji bora – ATHUMAN MUSSA ( KING MWALUBADU)
6. Filamu yenye kava bora – DANGER ZONE
7. Mtayarishaji bora wa filamu – STEVEN KANUMBA
8. Kampuni bora ya utengenezaji filamu – RJ Company
9. Msambazaji bora – Game 1st Quality
10. Muongozaji bora – VICENT KIGOSI (Ray The Greatest)
Matokeo haya ni kwa mujibu wa watembeleaji wa mtandao
wa
http://www.filamucentral.co.tz


hongereni washindi..ila kinachohitajika mwaka 2011 mfanye mapinduzi ya kuleta more quality movies pia na story zenye akili acheni kutoa movie ka njugu af quality ya kishamba...big ups all
ReplyDeleteMIMI NIMEWAHI KUSEMA KWAMBA WASOMI WA MUZUMBE CHUO KIKUU CH AUNIVESITI CHA KULE MOLOGOLO NDIO WATU MAKINI KURIKO WOTE KWENYE HII NCHI NA TASNIA YA FIRAMU. MUNAONA KANUMBA ZE GLET ALIVYONYAKUA TUZO ZA HESHIMA? MAANA YAKE NI KWAMBA AMESOMA UCHUMI NA ECONOMY KATIKA CHUO KIKUU CHA MUZUMBE AMBAKO ANKAL MISUPU, KAMAU,NA WEMA SEPETU HATA DR.JK AMEPATA DIGILII YAKE YA PHD YA UCHUMI NA ECONOMY. BIG UP KANUMBA BWANA. KILICHOBANI NI MIMI KUJA KUWA STELINGI KWENYE SENEMA ZAKO BWANA TUPIGIANE TAFU
ReplyDeleteKanumba juu
ReplyDeleteAnonymous wa 10:54:00 PM, usinichekeshe mie....
ReplyDeleteKwanza unatudhihirishia kuwa wasomi wa Mzumbe hawajui kuandika kwa kishwahili....au sio? sasa spati picha ungeandika kwa "kidhungu"..Eti Uchumi na Economy...haha
Ndugu yangu, hawa watu wameshinda hizi tuzo na kuyamudu maisha kwa juhudi zao binafsi, kwa taarifa yako Kanumba kaanza kuigiza tangu enzi za Jitegemee...hapo vipi?
Acha sifa za kijinga, wasifie wenzio kwa kushinda tuzo hizi na kuwa na malengo katika maisha yao, usituletee sisi hapa mambo ya university, kaandike kwenye notice board ya chuo chenu,
Kwa taarifa yako namfagilia sana Kanumba, He z got talent, and it has nothing to do with Economics..
Thumbs up to all the winners..keep it up guys...
monalisa?how??i strongly believe waigizaji wengi wa kike wamemwacha mbali huyu.
ReplyDeletewalioaachwa hawafikii kiwango cha Monalisa huyu binti anatisha na kweli ana act, hasomi ngonjera na anajua kuvaa uhalisia, kidogo kwa nyuma yake Riyama wengine wauza sura na kujishebedua.
ReplyDelete