President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete inspects a welcoming parade mounted by members of the Malawian armed forces shortly after he arrived in Blantyre’s Chileka International Airport for one day working visit.
A Malawian girl Kiki Mbilizi pins a fresh Red Rose on President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete’s coat shortly after he arrived in Blantyre for a one day working visit yesterday.
Malawi’s President Bingu wa Mutharika welcomes President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete shortly after he arrived in Blantyre for a one day working visit.
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete lays a wreath on the tomb of the former Malawi First Lady Madame Ethel Zvauya Mutharika who died on 2007 and buried at Mpumulo wa Bata Mausoleum.President Kikwete was in Malawi for a one day working visit where he held talks with his host President Bingu wa Mutharika who is also the current chairman of the African Union AU.
Malawi’s Foreign Minister Etta Banda(on her knees, right) welcomes in style, President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete shortly after he arrived in Blantyre for one day working visit yesterday. On the left is Malawi’s Minister of transport and public infrastructure. President Kikwete later held talks with President Bingu wa Mutharika of Malawi who is also the current chairman of African Union AU. The President returned to Dar es Salaam yesterday evening.President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete in talks with President Bingu wa Mutharika of Malawi in Blantyre yesterday during a one day working visit. President Dr.Kikwete returned to Dar es Salaam yesterday evening.(photos by Freddy Maro).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. HIYO NDIYO AFRICA AMBAYO HAKI ZA BINADAMU HAZIZINGATIWI. NILIFIKIRI KIKWETE ANGEMWAMBIA MAMA SIMAMA HAKUNA HAKI YA WEWE KUPIGA MAGOTI NA KUTAMBAA...WASUKUMA MPO? DESTURI ZA KIAFRIKA ZA NDIYO MZEE,..NDIYO MZEE ZINATURUDISHA KARNE YA 18 NA KUTUKUMBUSHA UTUMWA.

    ReplyDelete
  2. Halafu watu wa Malawi wanategemea huyo mama (Foreign Minister) awe effective...bullshit.

    ReplyDelete
  3. Hivi kaka Michuzi, unapomuandika huyu Raisi Kikwete, ni lazima utangulize na hiyo hadhi ya Dr? Kweli bongo watu tunajua kuwakweza viongozi. Mbona akina Obama wanamadigrii ya ukweli ya Phd na bado anatambulishwa tu kama President Obama? Au mnataka kutuletea mambo ya Iddi Amin aliyejiita Field Marshal, Dokta, Sir, Conqurer of British Empire na upupu mwingine mwingi wa vyeo. Acha kasumba kaka Michuzi!!

    ReplyDelete
  4. Hilo ni tatizo ambalo wengi linawakumba, yeye anafuata desturi za kiafrica na bado hajawa brain washed na "western culture" kupiga kwake magoti hakumfanyi ashindwe kufanya kazi zake kama waziri. Mlioendelea mbona hata huo uwaziri hamjapewa???? Acheni kuiga mira na desturi za wenyewe na kuona zenu hazifai.

    ReplyDelete
  5. Actually, nothing wrong. Kuna nini kinapungua kama mama akipiga magoti? Hivi waafrika hatujui kama kuna majukumu ambayo kwa mila zetu, yanafanywa na baba tu na ni makubwa? Pamoja kuwa mama na baba wote ni wazazi na wakuu wa familia, Maandiko yote yanaonyesha kuwa anapewa mamlaka na wajibu mkubwa zaidi katika jamii. Ndiyo maana likiharibika jambo, watu hawaanzi kumlaumu mama kwanza. Wanamtupia baba lawana, mama anaulizwa kama mtu wa pili. Mfano wa majukumu makubwa ambayo wanaume wanayachukua kwanza ni kama kazi ngumu za ujenzi, kwenda vitani, nk, kwasababu tu za kimila na pia kimaumbile, na utamaduni pia.

    Nafikiri tusiige sana mambo ya wazungu tukadhani kila wanachotukosoa tunakosea.

    Ukiangalia familia za wazungu, hamna heshima kubwa sana ya watoto kwa wazazi wao, kisa ni huko kujiona wako sawa nao sababu nao ni binadamu. Mzazi anambembeleza mtoto kama yai. Hata kumkemea anaogopa, mtoto wake wa kumzaa.

    Huyu mama anawakumbusha waafrika kuwa tuna mila zetu, tusizisahau.

    ReplyDelete
  6. WEWE ULIYEKOSOA KITENDO CHA HUYO MAMA KUMPIGIA MAGOTI RAIS KIKWETE HIVI UNAWAZIMU? ALIYEKWAMBIA HUYO MAMA KAMPIGIA MAGOTI RAIS WETU KWA SABABU NI HAKI YAKE KUMPIGIA MAGOTI NI NANI? HUYO MAMA KAMPIGIA MAGOTI RAIS WETU KWA SABABU TU YA KUMUHESHIMU NA SIYO UTUMWA KAMA UNAVYODAI. wewe si BURE BALI UNAKABILIWA NA TATIZO LIITWALO "PSYCHOLOGICAL DISORDER".

    ReplyDelete
  7. Hii kitu siyo kabisaa, anayepaswa kupigiwa magoti ni mwenyezi Mungu peke yake, hata ingekuwa ni mila yangu nisingempigia mwanaume goti bora wanitenge lol, huo ni utumwa wa hali ya juuuuu sana!!

    ReplyDelete
  8. Nyie wote wawili naona upeo wenu sio mkubwa kihivyo. Ebu angalia Japan..mwanamke anavyomsimamia mmeo, mbona wameendelea? Mzungu kweli hana haja ya kufanya kazi yake, maana ana kina nyie mliosoma mko wakutosha..

    ReplyDelete
  9. Jamani. hii ni stayle ya heshima tu, na heshima ni kitu cha bure, kaonyesha heshima yake ni ishara ya upendo kwa viongozi wetu wa bara la Africa, na viongozi waweza onyesha heshima hata kwa wanachi wao ni upendo tu, mbona hata nchi zilizendelea wanawake waliowengi wafalme wao wakipita kuwasalimia na kuwapa mikono uwa wanapiga magoti hata kama sio mapaka chini, lakini wanapiga magoti kwa wafalme wao.

    ReplyDelete
  10. sare za jeshi ni sawa, tuungane

    ReplyDelete
  11. Jamani, kweli si lazima kumwita J.K doctor kila mahali. Uncle Michuzi umejisahau kidogo. Huyo Bingu wa Mutharika ni doctor wa ukweli, ana Ph.D. Hivyo anaitwa Dr. Bingu wa Mutharika au Bingu wa Mutharika, Ph.D. Lakini uncle amemtaja tu kama raia wa kawaida (lay person).

    Mdau uliyesema Obama ana Ph.D ni mwongo. Mimi sijaona mahali popote inapoonesha alipata Ph.D. Najua tu alifundisha sheria chuo kikuu na si lazima awe na Ph.D.

    Nawasilisha.
    Mdau,
    States

    ReplyDelete
  12. Jamani mimi sioni kosa alilofanya huyo mheshimiwa kupiga magoti, hii inaonyesha hata ukiwa na cheo gani usisahau mila na desturi za kwenu kama mtu unaona azifai basi achana nazo nyinyi mnaoshutumu inaelekea mnaweza kumwambia mzai wako, babu, bibi kwamba wasifanye mambo yaliyowakuza kisa wazungu wanasema yamepitwa na wakati. Lazima tukubali kwamba hii ni mila na desturi za Waafrika.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...