
Transfoma mpya inayofungwa katika kituo cha kupooza umeme cha Kipawa baada ya kuondolewa kwa transfoma iliyoungua na kuchangia mgao wa umeme jijini dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Bw. David K.Jairo akifanya mahojiano na mwandishi wa habari wa BBC juu ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali kukabiliana na tatizo la umeme nchini.kushoto kwake ni Msaidizi wa Katibu Mkuu bwana Elias Kayandabila na Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasialiano Bw.Aloyce Tesha.

Katibu Mkuu wizara ya Nishati na Madini Bw. David K.Jairo akipata maelezo toka kwa Meneja Mwandamizi Udhibiti na Njia kuu za umeme (TANESCO) Eng.Abdullah Fereshi ( kulia kwa KM) juu ya maendeleo ya kazi ya ufungaji wa Transfoma mpya katika kituo cha kupooza umeme cha Kipawa.kushoto kwake ni Msaidizi wa Katibu Mkuu bwana Elias Kayandabila na Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasialiano Bw.Aloyce Tesha. Bw. Jairo ameamuru mafundi wa TANESCO wafanye kazi kwa masaa 24 ili hali ya upatikanaji umeme ilejee kama kawaida katika kipindi kifupi.
Hata mimi ninaweza kusupply mitambo mingi tu inayotengenezwa na General Electric. Nitanunua iliyotumika lakini at least nitahakikisha inafanya kazi. Na commission yangu ni poa tu, asilimia 10. Siyo commission inakuwa kubwa kuliko hata bei ya mitambo yenyewe.
ReplyDeletesasa hiyo kazi itachukua muda gani au huyo mtoa habari hakuwa na nafasi ya kuuliza michuzi wacha kutoa habari nusunusu
ReplyDelete