Mshambuliaji wa Kilimanjaro Stars, Stephano Mwasika akimtoka beki wa Rwanda, Clement Mutunzi katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Chalenji uliofanyika kwenye Uwanjawa Taifa. Kili Stars ilishinda 1-0.
Golikipa wa timu ya Rwanda,Ndaishimie akiokoa moja ya hatari zilizokuja langoni mwake katika mchezo uliopigwa jana jioni uwanja wa Taifa,jijini Dar.Kilimanjaro Stars ilishinda 1-0.
Moja ya mabao ya penati ya uganda likitinga
kwenye wavu wa Zanzibar Heroes. Picha na John Bukuku

TIMU ya soka ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ jana ilitinga nusu fainali ya michuano ya Kombe la Chalenji baada ya kuifunga Rwanda ‘Amavubi’ bao 1-0.

Mchezo huo ulifanyika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, huku wawakilishi wengine wa Tanzania, timu ya Taifa ya Zanzibar ikitupwa nje ya michuano baada ya kufungwa kwa penalti 5-3 na Uganda ‘The Cranes’.

Matokeo hayo ni zawadi kwa Watanzania ambao leo wanasherehekea miaka 49 tangu Tanzania Bara ipate Uhuru wake mwaka 1961.

Mashabiki waliojazana kwenye uwanja huo ilibidi wasubiri mpaka dakika ya 62 kwa bao la mkwaju wa penalti lililofungwa na nahodha wa Kilimanjaro Stars, Shadrack Nsajigwa baada ya John Bocco kuangushwa alipokuwa akielekea kufunga.

Kutokana na ushindi huo, Stars sasa itacheza nusu fainali kesho na Uganda ambayo jana iliitoa timu ya Taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’.

Timu hizo zilifungana mabao 2-2 katika mchezo wa kwanza wa robo fainali uliofanyika uwanjani hapo.

Watanzania waliokuwepo uwanjani hapo ilibidi wasubiri mpaka dakika ya 87, ambapo Aggrey Morris alisawazisha bao kwa kichwa na kufanya ubao usomeke mabao 2-2.

Lakini Morris ndiye aliyewaliza mashabiki baada ya kukosa penalti ya kwanza, wakati wa upigaji huo kutokana na matokeo ya sare hiyo.

Katika upigaji huo Waganda walitumbukiza wavuni penalti zao zote tano, huku Zanzibar ikifunga tatu, ambapo penalti ya mwisho haikupigwa kwa vile tayari Waganda walishafunga penalti zao.

Wafungaji wa penalti Zanzibar walikuwa Abdulhalim Humoud, Nadir Haroub na Waziri Salum, wakati kwa Uganda ni Isinde Issack, Sadam Juma, Danny Walusimbi, Tonny Maweje na Emmanuel Okwi.

Katika dakika 90 za kawaida, mabao ya Uganda yalifungwa na Mike Sserumanga na Okwi ambaye alifunga kwa penalti mapema kipindi cha pili, huku ya Zanzibar yakifungwa na Mcha Khamis na Morris.

PS: Kunradhi kwa kuchelewesha matokeo.
Hii imesababishwa na kwikwi ya ghafla ya mtandao.
-Michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Kaka japo Kilimanjaro tumeshinda 1- 0 wale Rwanda walikuwa very cinsistency na sisi tunabahatisha zaidi.PIA NINGEPENDA KAKA TIMU YETU IHAMISHWE PALE ATRIUMS HOTEL KWANI PALE NI OPPOSITE NA AMBIANCY CLUB NA UTAONA USIKU MZIMA WACHEZAJI WANAHANGAIKA NA MACHANGUZ NA MASATOZ!!!!

    ReplyDelete
  2. matokeo ya visiwani please????? mbona wavivu nyie kutupa habari za nyumbani?

    ReplyDelete
  3. Kaka Michu, sisi tulioko Ughaibuni tunasubiri update kwa hanu. Najua hapo Bongo mida hii ni saa moja na mpira utakuwa umeisha. Pia naomba utuletee matokeo ya ndugu zetu wa Zanzibar pia

    ReplyDelete
  4. KAKA WATU WENGI TUNAPENDA SANA BLOG YAKO BUT WENGI WETU HASA MIMI NINAPATA SANA SHIDA JINSI YA KUTUMA HABARI,COMMENT AU HATA PICHA!!

    ReplyDelete
  5. Tumeshinda kwa sababu ya juhudi binafsi za wachezaji, hakuna mpangilio maalum wa uchezaji kama wenzetu walivyokuwa wanacheza. Kama tungeweza kuchanganya hizi juhudi na mfumo wa uchezaji tuliokuwa nao wakati wa Moximo hii timu ingetisha!!!!
    MDAU HOUSTON.

    ReplyDelete
  6. Kaka huyo jamaa wa jamaa wa juu ni muwongo sana mimi mqwenyewe nipo hapa...kocha wao anawakataza hata kutoka nje hapo walipo ni sehemu safe kabisa

    ReplyDelete
  7. sasa wewe undendi hotel wanayo kaa , walipie basi hiyo unayo itaka. kwani machangu wanamatatizo gani. ukiwa mtaje wao hata uwe wapi watakufata tu

    mdau paris

    ReplyDelete
  8. Mr Blog owner, najua kabisa kabla ya kurusha hizi comments zetu huwa unazipitia ku-approve kabla ya kuzirusha. Tunaamini unazisoma ndio uzirushe. Tuko Ughaibuni na tumeandika utupe matokeo ya mwisho na pia ya Zanzibar.Kwa nini hutuletei? Otherwise, hamna haja ya sisi kutuma comments. Tafadhali, ukishaisoma hii ili kui-approve, tuma matokeo tuliyoomba

    ReplyDelete
  9. Wale wa Ughaibuni

    Zanzibar imefungwa 7-5 ni baada ya kudraw 2-2 normal time na kukosa penati 2 wenzao wakipata zote 5

    ReplyDelete
  10. Kwa wanaotaka matokea ya Zanzibar ni kuwa Zanzibar wametolewa kwa Penalti kwa magoli 5 kwa 3 baada ya kutoka sare ya 2-2 kwenye muda wa kawaida. kwa hiyo Uganda itacheza semifainal na Tanzania Bara. wakati Ethiopia itacheza na Ivory Coast.
    mdau Paka la Jikoni.

    ReplyDelete
  11. wewe mdau wa ugaibuni unaye lia lia kuusu kutowekewa matokeo ya zanzibar kwani lazima kila kitu uwekewe humu. kama wewe mkereketwa wa mpira kwa nini usiwatumie nduguzako znz wakuambie kuusu hiyo match . ama huna
    pesa ya kutuma msg .

    mdau China

    ReplyDelete
  12. Zanzibar imetolewa kwa matuta-walifungana 2-2 na baadae ikawa matuta. Ambapo Zanzibar tumepokea taarifa ilipata 3 ikakosa 2 kati ya 5. Hivyo imetolewa lakini imekufa kiume. Waganda walipata zote 5.

    Kampuni
    Norway

    ReplyDelete
  13. Zanzibar imetoka nje? Da! Walikuwa wetu hao Watanganyika, sasa Uganda itatufunga 2-0.

    ReplyDelete
  14. Wewe mdau kutoka China huna tofauti na madawa ya kichina yanayoweza kuongeza sehemu fulani ya mwili. Pia huna tofauti na bidhaa za china. Mwenzako anataka hii blog iwe updated wewe unaleta longolongo. Hivi unaona ni sahihi saa sita usiku huu bado blog inaonesha kwamba ni dkk ya 35 kipindi cha pili. Hata ukiwa China jitahidi usiwe kama bidhaa za huko

    ReplyDelete
  15. hihihihi MADE IN CHINA HAYA visiwani wametolewa MUNGU IBARIKI TANZANIA kama inavojulikana kimataifa timu ya taifa ya tanzania ishinde world cup hii

    ReplyDelete
  16. Jamani hii Chalenji vipi?

    Mbona Tanzania inaingiza timu mbili? Eti Tanzania Bara na Zanzibar!!

    ReplyDelete
  17. HIVI INAWEZEKANA KUPATA LIVE STREAMING YA HIZI GAME? MSAADA PLEASE ANAYEJUA. ASANTE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...