Haya ni mahafali ya kwanza ya Chuo kikuu cha Sebastian Kolowa University Collage (SEKUCO) yaliyofanyika tarehe 4 Desemba 2010. SEKUKO ni chuo kishiriki cha TUMAINI UNIVERSITY; Kipo katika eneo palipokuwa shule ya Sekondari Magamba, huko Lushoto. Mgeni rasmi katika mahafali hayo alikuwa Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa.

Wadau wa Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa University Collage (SEKUCO) wakielekea kula nondozzz zao tarehe 4 Desemba 2010.

Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa, akihutubia mahafali hayo.

Mgeni rasmi katika mahafali hayo Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa akiwa na viongozi wa kanisa la KKKKT na wahitimu wa chuo hicho baada ya kula nondozzzz

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Collage??? Hizi elimu za kupeana na kufungua vyuo kuendeleza ukabila ni hatari kwa watanzania. Kuna ripoti inayosema wanafunzi wa mkoa wa Pwani karibu wote wamefaulu kwenda sekondari? Je wamefaulu kweli au ni kwa sababu JK anatoka huko?

    ReplyDelete
  2. huu ni wakati ambao mtu anayetaka kuishia la saba achague mwenyewe. Kufaulu haitakiwi kuwa dili na kunatakiwa kufutwe. Kila mwanafunzi anatakiwa apate elimu ya sekondari.

    Hivyo usishangae watu woote kufaulu, maana yake kila mtu asome secondari.

    ReplyDelete
  3. K moja imezidi bro!

    ReplyDelete
  4. Wajemeni, msaada kwenye tuta...ni nini maana ya university college? Kwanini hivi vyuo vinaitwa University college? Na siyo tu University au college tu. Natumaini nitasaidiwa wajameni.

    ReplyDelete
  5. Swala ni upendeleo sio wanafunzi kufaulishwa mkoa mmoja wakati mikoa yote inatoa kodi ya kuendeleza nchi. Elimu ni muhimu! Kwa utaratibu unaotaka ni bora elimu iwe ya kulipia kusudi serikali isionekane inapendelea mikoa fulani.

    ReplyDelete
  6. He!SEKUCO?Kumbe Tz siku hizi kuna vyuo vikuu vingi,ndiyo nakisikia leo hiki,kinafundisha Theology pekee au?

    ReplyDelete
  7. Ankal Salaam,

    Hawa waliokula Nondozzzz hawajui kuwa baada ya kula nondozzz huu uzi unatakiwa uelekee kulia???? badalaya shoto? maana kabla ya kutunukiwa uzi unakuwa shoto! na baada ya hapo ukivaa kofia baada ya kutunukiwa uzi unatakiwa uelekee kulia KAMA SIKOSEI AU WADAU MNASEMAJE???

    ReplyDelete
  8. Some ceremonies no longer include the tradition of placing the tassel on one side or the other, but, historically, the tassel was placed on the right side of the student's cap before he or she was awarded a diploma and then moved to the left side after the student received his or her degree. At some university ceremonies, graduate students wear their tassels on the left side of their caps, while undergrads tassels are placed on the right side.

    ReplyDelete
  9. Mdau hapo juu, "University College" maana yake ni moja wapo ya vyuo katika college kubwa. Tumaini University ni campus mama na vyuo vingine ambavyo vinatoa taaluma moja au chache ni 'University College"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...