Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal kulia, akisalimiana na Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wa Zambia Profesa Geoffrey Ligwangwa wakati Waziri huyo alipokwenda nyumbani kwa Makamu wa Rais Oysterbay Dar es salaam leo kwa ajili ya kumkabidhi Ujumbe Maalum wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kutoka kwa Rais Ruphia Banda wa Zambia.
Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wa Zambia Profesa Geoffrey Ligwangwa kushoto akikabidhi Ujumbe maalum wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kutoka kwa Rais Ruphia Banda wa Zambia kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal, wakati Waziri huyo alipokwenda nyumbani kwa Makamu wa Rais Oysterbay Dar es salaam leo kwa ajili ya kukabidhi Ujumbe huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na ujumbe wa Serikali ya Zambia Ulioongozwa na Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wa Nchi hiyo Profesa Geoffrey Ligwangwa, wakati Waziri huyo alipokwenda nyumbani kwa Makamu wa Rais Oysterbay Dar es salaam leo, kwa ajili ya kumkabidhi Ujumbe maalum wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kutoka kwa Rais Ruphia Banda wa Zambia.Picha na Amour Nassor.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. naona Bilali kapigwa sopsop la nguvu. wakati wa kampeni alikuwa kachoka kama nini sijui. lakini sasa hivi anaonekana vizuri, tena kawiva, kuliko siye wabeba maboksi. kweli madaraka mazuri jamani.

    ReplyDelete
  2. Duuh jamani neema haichagui, mmemuona Bilal!

    ReplyDelete
  3. mdau wa kwanza kumbe umeona hili na wewe kile kipindi cha kampeni nilishindwa kuingia humu manake picha za jamaa zilikuwa siyo kabisa, sasa hivi ana mng'ao kweli, madaraka matamu jamani oneni wenyewe!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...