Mdau:mbona kama magumashi hivi.??!!

Ndugu

Tukumbuke kwamba wakati huu ni wakati wa kuandikisha watoto kwenda darasa la kwanza. na Serikali ya Tanzania inasema au tuseme sera ya elimu inasema kwamba elimu ya msingi ni bure. lakini sasa hivi inajitokeza kuwa kila mzazi anayekwenda kumwandikisha mtoto hasa katika shule ya Msingi Bryceson huko Mburahati jijini Dar es salaam kila mzazi/mlezi anayekwenda kuandikisha mtoto anadaiwa apeleke shilingi 22,400 ikiwa ni mchango wa madawati, mlinzi, na mengineyo lakini cha ajabu risiti hazitolewi.

Je uhalali uko wapi? Halafu hili suala la kutochangia kwa maana ya elimu ya msingi bure likoje mbona kama magumashi hivi????????

Najua tukifuatilia kuna mengi mno ambayo tunaweza kuibua. Kazi kwetu!!!

Mdau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. MDAU SIO SIRI UMENIKUMBUSHA MBALISANA KWA SWALA ZIMA LA"MAGUMASHI!!!!!"
    ILA UKWELI NAFIKIRI KAMA KUNA KUWA NA MALIPO YOYOTE KUNA UMUHIMU WA KUTOA RISIT,PIA SWALA LA ELIMU BURE NAFIKIRI HAWAKUMAANISHA KUWA BAADHI YA MICHANGO MIDOGO MIDOGO HAITAKUWEPO.ILA KAMA HAWATOI RISIT INAKUWA NI TATIZO.ILA HATA KAMA ITAKUWA NI BURE BADO KUTAKUWA NA KITU KAMA UCHAKAVU NA KADHALIKA ILA HII NI MAGUMASHI KWELI.-dako

    ReplyDelete
  2. haya ndio yenyewe mlioyataka

    ReplyDelete
  3. Kinyerezi 25,000

    ReplyDelete
  4. Watz mmeyataka wenyewe........mkiambiwa hamsikii. Hamna cha kukushauri, mlipewa nafasi hamkuitumia, mliambiwa elimu bure mkakejeli kuwa haiwezekani, sasa cc tutoe ushauri gani.aaaaaaaaaghhhhhhhhhhhhh

    ReplyDelete
  5. yaani hivi kila mkuu wa shule anajipangia mwenyewe kiasi ndio hivyo samaki mkubwa anamla mdogo na bado mtalimanya jiji shule zingine 275oo.

    ReplyDelete
  6. Nakumbuka tangu 1985 nilipoanza dalasa kwanza tulikuwa tunapeleka ela ya madawati kila mwaka mpya. Kwani bado hayajatosha tu!

    ReplyDelete
  7. HAHAHHAA...hahaha mdau wa mwaka 1985 umeniacha hoi sana...hahahahah..hehehe...kweli duniani kuna watu wanavituko sana..!!

    ReplyDelete
  8. TZ kila mtu anajaribu kuiba kwa nafasi yake.
    Wenye shule zao wanapandisha bei na hawafundishai wanafunzi kila siku kulipia masomo ya ziada,

    wasio na shule michango ya uwongo na kweli kila kukicha.

    Mzee wetu yeye hana watoto wanaosoma, hii shida haimgusi ndiomaana elimu bure ilikataliwa. Tusubirineema ya Mungu tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...