Rais Jakaya Kikwete akiwa katika gari maalum na mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Jenerali Davis Mwamunyange wakati akiwasili ndani ya Uwanja wa Uhuru jijini Dar leo.
Amir Jeshi Mkuu,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua Gwaride leo katika maadhimisho ya miaka 49 ya Uhuru ndani ya Uwanja Uhuru,Jijini Dar leo.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mama Salma Kikwete wakati alipokuwa akiwasili katika jukwaa kuu.wengine ni Rais wa Zanzibar,Dr. Ali Mohamed Shein (wapili kulia) na Waziri Mkuu,Mizengo Pinda (wapili kushoto).

kwa habari na picha zaidi

BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. RAIS WETU JAKAYA MRISHO KIKWETE
    AMIRI WA JESHI LETU LA WANANCHI,
    MWENYEKITI WA MAPINDUZI YA WANANCHI

    HONGERA KWA KUPOKEA NA KUENDELEZA UHURU NA UTAWALA BORA.

    MWL JK NYERERE ALIWEZESHWA NA WANANCHI AKAPAMBANA NA WAKOLONI AKALETA UHURU WA KUJITAWALA KITAIFA.

    KWA MISINGI YA UHURU HUO MZEE A.H MWINYI HAKUONA HAYA KUCHUKUA UAMUZI WA HEKIMA NA MGUMU KUUWEZESHA UCHUMI WETU UENDANE NA SOKO LA WAKATI.

    KWA NGUVU ZA UHURU WETU MSTAHIKI BEN MKAPA AKALETA NIDHAMU YA UCHUMI WA SOKO.

    WEWE UMEKUWA JEMEDARI WA KWANZA:

    1.KUWAWEZESHA WANANCHI WA KIPATO CHA CHINI KUJIENDELEZA KIUCHUMI NCHINI KOTE BILA UBAGUZI.

    2.UMEJENGA NA KUPANUA KWA MAKUSUDI UWANJA WA DEMOKRASIA YA WAZI KWA WATU WA IMANI, RANGI NA ITIKADI ZA SIASA NDANI NA NJE YA VYAMA VYAO LAKINI KWA KUZINGATIA UTAIFA NA UHURU WETU.

    3.WEWE NI MWASISI WA HOJA YA KUWATAMBUA,KUWASHIRIKISHA NA KUWASAIDIA WATANZANIA WANAOISHI NJE YA NCHI(DIASPORA) ILI WAYAVUNE MATUNDA YA UHURU WA TANZANIA KWA USAWA.

    4.UMEONGEZA KIWANGO KUWA CHA JUU CHA KUWATAMBUA KWA UFANISI WAO WANAWAKE WA TAIFA LETU ILI WASHIRIKI KATIKA SIASA ZA UWAKILISHI NA UTAWALA; KUENDESHA TAASISI ZAO ZA KIUCHUMI mf BENKI NA ASASI ZA KUPUNGUZA UMASIKINI.

    5.UMEWAJALI WALEMAVU WA AINA ZOTE NA KUWEKA MPANGO MADHUBUTI WA KUWAKWAMUA KIUCHUMI,KIUSALAMA NA UWAKILISHI WA UPENDELEO.

    6.UMEWEZA KUWEKA TARATIBU MADHUBUTI ZA KUPUNGUZA CHANGAMOTO ZINAZOJITOKEZA KUTOKANA NA MAENDELEO UNAYOYASIMAMIA NA KUYAONGOZA NDANI YA CCM NA SERIKALI YAKE mf. kuongeza waalimu; watendaji wa huduma za afya za jamii,wauguzi na waganga;idara ya usalama wa raia na mali zao;maafisa kilimo, mifugo na uvuvi n.k

    NI JUKUMU LETU SASA SISI WANANCHI KUACHA KULAUMU BALI KUTEKELEZA SEHEMU YA MAJUKUMU YETU ILI HAKI NA USAWA VISHAMIRI NA VISHABIHIANE NA UHURU WETU.

    MUNGU IBARIKI TANZANIA.
    MAPINDUZI DAIMA.

    MAINA ANG'IELA OWINO
    CCM UK

    ReplyDelete
  2. Sasa Uhuru wa kitu gani unasheherekewa? HAPA SIJAFAHAMU,Kwani TANGANYIKA INA EXIST HADI LEO? INA MAANA VYOMBO VYA HABARI VITARIPOTIVIPI MFANO"habari kamili DODOMA,TANGANYIKA leo imesherehekea miaka 49 ya uhuru" au TANZANIA IMESHEREHEKEA MIAKA 49 YA UHURU? SASA CELEBRATION OF NONE EXISTING COUNTRY HII SIJAPATA KUONA,INA MAANA TANGANYIKA BADI IPO NA INA SERIKALI

    ReplyDelete
  3. Nawapongeza watz wote kwasiku hii kwan ndotulipata uhuru.
    LAKINI NAOMBA KUTOA USHAURI KWAMBA TUACHE KUPOTEZA MUDA KWAKUKAA NA KUSHEREKEA TU KWAN SIKU KAMA HII TUTUMIE KUCHANGIA UJENZI WA HOSPITALI, MAHABARA ZA SHULE NA KUWAFUNDISHA VIJANA KWAMBA UZALENDO UNAITAJIKA HILI TUTOKOMEZE UFISADI NA RUSHWA. SIKU HII INABIDI HIWE NIYAKUWAKUMBUKA WAPIGANIA UHURU WOTE NASIO KUKAA KWENYE VIWANJA NA KUMBI ZA STAREHE KWA WAISHIO ULAYA NA ASIA KAMA WANAVYOFANYA. iNAITAJIKA MABADILIKO MAKUBWA SANA TANZANIA. NAONA KUNA HAJA YAKUWA NAUONGOZI MADHUBUTI KAMA WAKKINA SOKOINE, NYERERE, NAWENGINE WALIOKUWAPO KIPINDI HICHO WAKATI TUMEPATA UHURU.
    TUACHE KUPPOTEZA MUDA NA KUDANGANYA WANANCHI KWAKUSEMA "NATOA PESA KIASI HIKI KWA KUCHANGIA UJENZI WA...."

    MUNGU IBARIKI TZ NA WATU WAKE.
    MAPINDUZI DAIMA.

    MDAU FRANCE

    ReplyDelete
  4. Hivi ukiwa ndani ya Uniform za jeshi na Crown kichwani si hautakiwi kucheka wala kulia??

    Au picha imeongezea mbwembwe kwa Mheshimiwa Mjeshi wetu??

    ReplyDelete
  5. Tunamshukuru mungu nchi yetu kufikisha miaka yote hiyo ya uhuru lakini bado hali zetu watanzania ni tete, maradhi,umaskini bado ni tishio.Tuchukulie mfano hapo dar tu, sasa hivi maji hakuna, maana yake watu wanatumia maji machafu,hivyo basi,baada ya miezi au wiki, mlipuko wa magonjwa ya tumbo yatatokea kwa wananchi, mwananchi huyo atakapokwenda hospitalini atatakiwa kununua dawa,pesa hana,atakunywa panado.Umeme ndo usiseme, Uchafu jiji linanuka, na hizi mvua vyoo vinatapika hovyo,watoto wanachezea maji hayo yenye vinyesi.Sijajua bado ni nani wa kulaumiwa.Tupo ndani ya shimo ambamo hatujui atakaetutoa ni nani.

    ReplyDelete
  6. HIVI LILE GARI LA NYUMBU MBONA HALITUMIKI?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...