Home
Unlabelled
TAMASHA LA VODACOM XXL AFTER SKUL BASH FUNIKA BOVU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Jamani wenzetu katika tamasha hili mlitumia kigezo gani kupata washindi? Nauliza hivi maana msijekuitwa washamba kama tulivyoitwa WASHAMBA na Master J kwenye mashindano ya BSS kwa ajili ya kumshabikia mzungu Joseph Pyne.
ReplyDeleteNiliumia sana kitendo cha Master J kukashifu watu au naweza kusema kutukana watu (pengine watanzania) kwa ajili ya kumpigia kura mzungu Joseph Pyne; na si kumpigia kura tu, hata kule kumshabikia alipoimba jukwaani.
Mimi nauliza kwa Master J, ni kigezo kipi cha ushamba alichokiona? Ni nani alimchagua mzungu Joseph Pyne kuingia kwenye BSS? KAMA NI USHAMBA, BASI MASTER J NA MAJAJI WENGINE NDIWO WASHAMBA MAANA WAO NDIWO WALIMCHAGUA PYNE KATIKA MSULULU WA WAIMBAJI WENGI WALIOJITOKEZA KUWANIA NAFASI.
Nilikuwa nafuatilia sana mchakato wa kuteua washindani, hata mikoani mlikokwenda, nilikuwa nafatilia, maana mlikuwa mnaonyesha kwenye runinga
Joseph Pyne alianza kwenye foleni kama wengine walivyoanza. Nakumbuka Joseph Pyne siku moja aliingia na gita katika usaili (interview) ya BSS. Miongoni mwenu mlimsisitizia sana NA KUMSHAURI Joseph aimbe kiswahili. Nadhani ushauri ule mlimpa kwa kuwa mliona ana kipaji hata mkampa nafasi. Nauliza, walikuwa watu wangapi kutoka Dar, lakini Pyne mliona anakipaji hata mkamchagua. Kwa kipaji hicho hicho mlichokiona Watanzania na watu wengine walikiona na ndiyo maana walikuwa wanampigia kura na pia kumshabikia. Haikuwa ni kwa sababu ya uzungu wake, bali ni kwa vitu alivyokuwa anafanya. Sasa iweje kutuita WASHAMBA?
Master J, pengine njia mliyochagua ya kumpata mshindi huenda mmekosea. Kama kutuma SMS tu ndiyo kura zenyewe za kupa mshindi, basi hakuna haja ya kuwatukana watu na kuwaita washamba.
MKURUGENZI WA BENCHMARKER, MADAM RITA, ULIUONA UDHAIFU HUU? HATA KAMA MASTER J ALIKUWA NA MTU WAKE ALIYETAKA ASHINDE, HAIKUWA NA SABABU YA KUKASHIFU WATU NA KUWAITA WASHAMBA. TENA LIVE, MOJA KWA MOJA, HADHARANI.
WENYE BUSARA ZETU TULISIKITIKA SANA. KITENDO KILE NAOMBA KILAANIWE. HUKU NI KUPUNGUKIWA NA BUSARA.
Hitimisho. KAMA MASTER J AMEKOMAA KIMAADILI, ANAPASWA KUWAOMBA RADHI WATU (MASHABIKI) KWA KUWAKASHIFU KUWAITA WASHAMBA.
Ni mimi Busara si Mvi
Naunga mkono hoja hii. Nakuomba Ankel Michuzi, ikiwezekana peleka ujumbe huu kwa Master J, na Madam Rita Paulsen wajirekebishe. Vinginevyo, wasituhamasishe mashabiki kutuma msg kuwapigia kura wale tuwapendao. Wapigieni wenyewe sasa ninyi mlio werevu. Au lengo lenu ni kutaka tuwachangie kupitia sms zetu tu halafu mnaishia kutukashfu?
ReplyDeleteHongera mdoa duku duku, kumbe uliguswa kama mimi.
hamkudhalilishwa chochote ila mmeambiwa ukweli. wabongo au waafrica kwa ujumla acheni kushobokea wazungu..huku kwao hufiki hata second round hata kama una sauti ya kumtoa nyoka pangoni..kama mnabisha waulizeni watu wa UK walivyoona jinsi watu weusi walivyobaguliwa kwenye mchakato mzima wa X-Factor!!! nimefurahi mshindi ni mzawa at least mtu mmoja au tuseme familia moja ishajitoa katika umaskini...Big up Madam Rita na Master J.
ReplyDeleteNoma sana
ReplyDelete