
1:kila eneo liwe linajitegemea kwa kila kitu..kwa huduma zote ikiwa,za afya,chakula,hoteli.
Mfano..itakuwa safi sana kama kwa wanaokaa kinondoni wakawa na bank zote.wakawa. supermarket zote. Na wanaokaa magomeni nao wakawa na za kwao.ilala nao za kwao..kwa wanokaa manzese…nao wanakuwa na kila kitu..hivyo basi itakuwa hailazimiki mtu kwenda town kwa kuwa huduma zote zinapatikana hapo..nimetoa mfani huo kwa kuwa mm nipo hapa London..(uk) toka nimefika hapa sijawahi kuona traffic akiongoza magari.. na hawa..jamaa wanahuduma zote..kwa kila eneo..hata distance ni ya kilomita 2 basi huduma zote unapata hapo ulazimiki kwenda mbali…
2:ingewekwa malipo ya magari kuwa yakiingia town yawe yanalipa..kama hapa London..kuingia na gari town centre..una lipia congestion charges..kwa kuwa watu waona ni gharama basi wanapanda train..wabishi wenye hela zao ndio wanaingia nayo mjini..
3:kingine ni kuwa ujio wa automatic umefanya magari kuwa mengi…n ass pale dar hakuna ukaguzi wa leseni huku wenzetu kila aina ya gari unayoendesha ina leseni yake..kama unaendesha automatic..basi unakuwa na leseni ya automatic..au kama unaendesha manual unakuwa na manual ambayo inakuwezesha kuendesha automatic lkn mwenye automatic haruhusiwi kuendesha manual..gear..
4:fly over ni muhimu…zikiwekwa sehemu zifuatazo..basi..kila kitu itakuwa hakuna foleni milelel magomeni. Ubungo.tazara, mwenge. Morocco. Faya. Uwt/mr road.ilala boma.. buguruni. Njia ya panda kwenda tabata. Na kuweka matoleo..sio kila mtu anekwenda mbezi ya kimara basilazima apite ubungo..
5: idadi ya madereva kwa gari.: hapa uk kila gari na dereva 1 au 2. Wakizidi 3.na system yao iko hv..first driver anaweza kuendesha gari ya mtu mwingine kama insurance yake in cover 2nd driver haruhusiwi kuendesha gari nyingine.. na hata 3rd driver..lakini ss home pale gari 1 tunaendesha familia nzima..hata kama tuko 10..kwa hilo hilo gari 1..
6: barabara za uswahili zote ziwekwe lami ili waatuwengine wapiti huko baada ya kujazana barabarini..
Yangu hayo tu kwa leo..
Mdau
15 spring pond road.
Dagenham
Essex
Rm9 5dp
UK
ushauri wako ni mzuri tena sana,lakini hayo yote mpaka yatimizwe mimi na wewe tutakuwa tumeshazeeka!!!!!viongozi wa bongo ni wazuri sana kwa kutoa ushauri na kuweka malengo lakini huwa hawafuatilii....ushauri wako huo kwa bongo ni kama "ndoto ya mwendawazimu!!!!!"
ReplyDeleteWATOA USHAURI NAWAPONGEZENI KWA MAONI NA USHAURI WENU. ILA WAHUSIKA NADHANI HAWATAKI KUFANYA KAZI ZAO, WANAYAJUA YOOOTE HAYA, SIJUI TATIZO NI NINI?!!!!
ReplyDeleteKila nchi ina sheria zake na uwezo wake katika kufanya na kutekeleza mambo.
ReplyDeleteuwezo wa kuweka mabenki na masupermarket kila sehemu sisi bado. hilo la fly over lenyewe tunalisubiria kwa hamu tuone kama litafanyika.
asante kwa mawazo.
imetolewa na:
katibu mkuu wizara ya maendeleo blog ya jamii.
Mapendekezo yako yanafaa mji mwingine Ulaya Mashariki, lakini sio Tanzania.
ReplyDelete1.Huduma hata ikiwa zitawekwa kila sehemu hilo haliwezi kupinguza msafara wa kuelekea mjini kati. Je unataka kutuambia na ofisi za Ikulu nazo ziwepo Mazese, Mwembe yanga? Feri nayo iwepo Mazese? Kuna vitu vitabaki kama vilivyo.
2.Ulaya watu walio wengi huduma nyingi wanazipata kupitia mtandao kama shughuli za kiofisi, maduka, benki na nk. Bongo hilo bado na sio la leo wala kesho. Ulaya hilo ndio limechangia kwa kiasi kikubwa kupinguza unnecessary movements.
3. Serikali zetu hazina uwezo wa kujenga barabara za kuunganisha na mipaka ya nchi jirani ili tufanye biashara na majirani, tunashindwa kukarabati huduma za reli ili tuingize pesa kutoka kwa majirani. Je kipaumbele cha barabara za mataani Dar kitawezekana?
Mdau,una mawazo mazuri kimsingi hata binafsi naliona ila tatizo la baadhi ya wakwetu sijui ni kasumba au nini hata sielewi utakuta dada amezoea saloon ya posta nayeye anakaa tegeta usije shangaa anawasha gari anazipita saloon zoote anaenda huko ukiuliza anakwambia aah wale nimewazoea pia kaka vivo hivyo haya anaacha maduka au masoko bunju anakwenda mwenge hilo ndo tatizo ndugu yangu
ReplyDeleteMawazo mazuri sana mdau, lakini hakuna kipya yote hayo uliyoyataja, wataalamu wetu na wanasiasa wanayajua SAANA, shida ni kujua mchawi aliyeturoga mpaka tunakataa kufanya hivyo,bado tuaagua, tukimpata atashugulikiwa, then tutatekeleza, naitakia familia yako XMAS njema.
ReplyDeleteMdau wa Tanganyika Masagati
Mtoa mada, nafikiri kuna mambo uliyosema lakini hayajazingatia hali halisi ya Dar. Oni no 2 lingewezekana tu endapo kutakuwa na usafiri wa uhakika wa public transport. Kwa sasa ni vigumu sana kupanda daladala ukiwa umevaa suti kisha ukaenda katika mkutano unaokutana na wadau wa mataifa mbalimbali. Kwa kweli utakuwa unanuka jasho sana
ReplyDeleteJamani ni mawazo mazuri ila kwa kwetu ni ngumu na msilinganishe tz na uk nyie mnalinganisha tz na nchi tajili wakati nyinyi ni nchi ya 3 kwa umasiki duniani mawazo kama ayo wanaweza kuwa nao nchi ka india thailand au nchi zozote zile zenye angarau kidogo kwenye uchumi . nyinyin yana kushindeni hata maji au umeme alafu mnataka muyapitishe magai yenu juu nani kakwambia iyo kitu inawezekana kwa tz nyie angalieni leo hii wenzetu wana jenga viwanja vya ndege nnje ya mji sisi ndio kwanza huu ulio ktk ya mmji tuna upanua . msisikilize zile ahadi za uchagu yale mambo yamesha pita hata ukimfata kiongozi leo ukamuuliza ahadi alizo zitoa kwenye uchaguzi atakwambia mi siku sema kitu chochote na wara sijaaidi mimi kama nikiingia madarakani ntajenga train ya kutoka ubungo hadi tegata . jamani mi nafikili kwanza tuzungumzie ma swara ya maji na umeme matibabu elimu tukiweza kuvifanikisha hivyo basi tunaweza kufanya chochote.
ReplyDeletekila la mzungu ndio zuri na sahihi enh?
ReplyDeleteUNASHANGAA KUONA KAMA TANZANIA NI NCHI ILIYOLOGWA LAKINI NAFIKIRI KUNAMAPUNGUFU MAKUBWA YA VIONGOZI WETU KWANZA HUWA NAJIULIZA JE HAWAONI NCHI NYINGINE WANAFANYAJE AU HAWAONI WENZETU WANAISHIJE WANAPLAN VITU VYAO NAMNA GANI,UNASHANGAA TANZANIA TUNAONGELEA BARABARA ZA JUU WAKATI TATIZO NI DOGO SANA TUNAHITAJI "BY PASS" AU RING ROAD,HIZI NI MUHIMU SANA UGANDA WAMEJENGA NA KENYA SASA WANAJENGA SISI TUNAONGELEA HABARI ZA ABUNUWASI,HUWEZI MTU WA TEGETA UNAFANYA KAZI AIRPORT KUKWEPA FOLENI KAMA HAKUTAKUWA NA BARABARA ZA PEMBENI,TUNAJISUMBUA
ReplyDeleteMtoa mada hongera sana kwa kuona utofauti uliopo viongozi wetu wanasafiri kila mara lakini wakifika airport yanayeyuka wazo langu tujenge mji mwingine (New DSM)nje ya mji na uwe na hayo yote uliosema
ReplyDeleteVIONGOZI WANAWAZA KUPELEKA WATOTO WAO MAULAYA!! UNATEGEMEA WATAJENGA HAPO? TUMESHAUZWA JAMA!! HAKUNA MABADILIKO HAPO, WE JUST HAVE TO DEAL WITH IT.
ReplyDeleteMtoa mada tumekuelewa ila kwa hali ya Tanzania kwa sasa haingekuwa busara kutoza magari yanayoingia mjini kama hiyo public transport network iko hoi. Ichube
ReplyDeleteMie watu wa Ulaya huwa wananishangaza sana kwakweli. Sasa hayo yote Ulaya yapo lakini jiji la London foleni yake ikifika wakati wa peak hours unaweza kulia na hapo pia kuna usafiri wa public wa kuaminika mpaka imefikia kuwa magari yanaingia kati kati ya mji kwa malipo maalum.
ReplyDeleteTusidanganyane hapa kama matawi ya benki yako kila wilaya mpaka Mbagala utayakuta.
Tatizo la Dar ambalo wengi wetu bado hatujalikubali ni hili, mji huu hauwezi kukidhi matakwa ya wamazi wake wanaoongezeka kila kukicha. Barabara ni zile zile wakati Dar ikiitwa Mzizima na zilizoongezeka ni chache na za zamani haziwezi kupanuka inabidi watu wahame Dar wahamie kwingine kama Dodoma ili kupunguza huo msongamano wa watu. Na pia wanaotaka kwenda mjini na magari walipe fees ili kuongeza idadi ya watu wanaotumia public transport nayo iwe ya uhakika hata trani na bahari pia tuitumie.
Dah, kaka huu ushauri wako ni mzuri sana hususan kwa sisi wakazi wa hapa Dar. Mimi nadhani mkuu wa nchi huwa hatoi kipa umbele katika hayo mambo kwani yeye huwa ana aanza kwa kupiga vingóra magari yote yanakaa pembeni then huyo anachomoka zake dkk 5 ameshatoka Ikulu na amefika Mbagala.....sasa ss wenzangu na mie kutoka posta ya zamani hadi mnazi mmoja masaa matatu............... Bora tungempa uraisi mzee Hashim Rungwe wa NCCR mageuzi labda angeliona hil1
ReplyDeleteMama Tibaijuka ingia kazini please uifanye kazi ya makazi kama ulivyoifanya HABITAT mpaka sasa hivi umeacha jina kubwa tena liko juu sana in the international community hakuna asiyekujua ndio mana Mhishimiwa Rais alikuachia hiyo kazi kwa kukuamini so hiyo Dar kwako ni cha mtoto I beleive, as long as ukipata ushirikiano wa MEya wa Jiji na Mkuu wa Mkoa na sisi wananchi ndani na nje tuko nyuma yenu ...together we can !!
ReplyDeleteahsante kwa ushauri wako ndugu,na mimi nipo london.back to relevancy,ushauri wako si mpya sana miongoni mwa watz wengi.mfano:UDSM kuna prof mmoja wa c.enginrn yeye ameshagombana na sumatra.cha kushangaza eti anaitwa marekani kutoa ushauri wa barabara na madaraja.TZ imelaanika kwa kuto kuthamini ushauri wa kielimu na kiufundi toka kwa watu wake...mwe!
ReplyDeleteflyovers are not as expensive as we over imagine! sudsidiary and muunicipal laws are been disregarded.licensing authority is not serious.municipal council doesnt knw its powers vested by the law,traf jams are nt a bunge matter as it was 2007 rather it was for the local authority mentioned above.where is the rule of law,until magufuli intervines?who polices the local gvts rough spendings?LORD...it doesnt take a genius for this which is common to all gvments...i humbly submit
Sisi hapo bongo tunataka kupiga roundi zetu pale maoffisi za ndugu zetu.Htu kubali hiyo .
ReplyDeleteDuh!wazo zuri sana,too bad tanzania hatuko kama ulaya kivitendo na fikra.
ReplyDeletemawazo yako viongozi wanayo siku nyingi ila hali halisi hairuhusu,
hata wewe ukirudi bongo na kupewa madaraka utakuwa kama viongozi wailiopo,thats the nature of African mind and Tanzania in particular.
in 2099 labda tutakuwa kama ulaya by then wao wanaenda mars and jupita for holidays
Ndugu mtoa maoni
ReplyDeleteNaafikiana na wewe baadhi ya point, ila point nr 5, sikubaliani na wewe kwani hio ya huko uk kuwa gari moja inawezekana watu 3 tu na hapa ndani ya dar ...tunaweza kuendesha hata watu 10 hii haijawa sababu kwenye suala la foleni hata kidogo, kwani unapokuwa na kila mtu ana gari ndio misongomano inaanza ni bora hio kuwa gari moja kuendeshwa na familia mzima
Isitoshe ni hapo uk tu, ila ukiangalia nchi jirani za ulaya ambazo wameendelea hata hapo uk wako na mfumo kama wa hapa bongo, na kama hujui hilo tembelea Germany,na Holland utajuwa hasa kwamba sasa uko ulaya ukiachana na hapo UK
Ukiangalia bara bara zao hizi nchi utapenda binafsi nimekuwa hizi nchi na siku zote naazima gari za watu na wako sheria kama za hapa kwetu gari moja endesha hata watu 20 kama kisheria unakubalika yaani uwe na leseni tu na utakuta mambo yanakwenda vizuri sana, kama ukitembelea germany ndio nchi pekee ulaya wanaruhusu kuendesha gari HIGH WAY mpaka 130 KM/HR, hii inatokana na kuwa na barabara mzuri na gari zao zote takribani zinamudu hio speed kutokana na umadhubuti wake, ila sio suala la kuwa gari moja tunaruhusika watu 10 hapa dar hili nakataa na ukitaka kuyajuwa haya jaribu kuzitembelea hizi nchi utakuja kuona kuwa hapo UK ni jina kubwa na kwa vile tulitawaliwa na hio nchi ila ukitakakuifaidi ulaya nenda Germany na Holland, na wameweka hata njia za wapanda baskeli ambazo unauhakika wa usalama wako unapokuwa barabarani, leo hii hapa dar sio baskeli tu ukiwa na pikipiki basi ni mtu maskini kwa vile hakuna mipangilio tu.....
Mdau ndani ya mikocheni B
Maarifa na waalamu tunavyo vingi, haswa kwenye mtandao. Tatizo ni uwezo, taifa letu lina mahitaji kuliko kipato.
ReplyDeleteNani ana mawazo ya kutuwezesha kugharamia malengo yetu?
Hapo utakuta kuna watu wanatoka kimara kwenda posta mpya kununua stamp, wengine kupost barua zao na wengine kuchukua barua kwenye masanduku yao ya posta.Kama wangewekewa ka-posta kadogo pale kimara magari yao yasingekuwepo kwenye foleni.Sasa wandugu na hili nalo serikali haina uwezo? Mbona tunao mawaziri wawili wa uchukuzi, ma naibu waziri wawili na wakurugenzi wa wizara wawili.Sijui Dr.Kikwete angekuwa rais wa Marekani wizara yake ya uchukuzi ingekuwa na mawaziri wangapi ili waweze ku-handle viwanja vya ndege karibu laki moja,1500 flights in the air per minnute more than Europe and Asia combine.Hata hivyo Marekani kuna waziri mmoja tu wa uchukuzi lakini mwendo mdundo.Naelewa kuwa si vizuri kulinganisha nchi tajiri sana na maskini sana, lakini nivizuri pia tujifunze kutoka kwa wenzetu kama tunahitaji mabadiliko.
ReplyDeletemi nadhani swala la muhumu ni kuhamisha baadhi ya ofisi katikati ya jiji...kwa sababu asubuhu watu wote wanaenda posta/kkoo...jioni wote watoka posta/kkoo..ofisi zote za bank, wizara, hazina, immigration, ikulu, makao makuu polisi, jeshi, hospitali kubwa kama muhumbili, agakhan e.t.c zote ziko katikati ya jiji...sasa unadhani foleni kwnda mjini itapunguaje?
ReplyDeletemi naona hila za mijitu iliozeeka wanaona hawatafaidi wao ila wataacha kwa vizazi vipya ka hiyo kufatilia suala inakuwa wazito sana ila ingekuwa kununua magari ya kifahali ungeiona serikali ilivo shapu.
ReplyDeleteMdau una wazo zuri lakini hamna big city ambalo halina foleni we call rush hours nimeishi london na miji usa na yote same asubuhi na jioni
ReplyDeleteMdau wa Essex, hata huko kwenu nje ya London, watu hawategemei usafiri wa magari madogo au viji- coaster.
ReplyDeleteHivyo kwa nyongeza ziwepo reli ya abiri wa mijini zipitazo juu ya ardhi toka Kongowe(Kilwa Road) kwenda Wazo Hill na pia toka Mnazi Mmoja Garden reli ikiambaa na Morogoro Road hadi Kibaha Mjini.
Tukipata usafiri-ziada (alternative transport) na kuondoa kabisa vipanya na coaster visiguse maeneo ambayo yanahudumiwa za barabara zifuatazo za Kilwa Road/Morocco/Bagamoyo/Upanga/Mandela/Shekilango/Sam Nujoma basi adhaa hii itatoweka. Usafiri ndani ya maeneo ya barabara hizo mabasi makubwa (Abiria zaidi ya 75 waliokaa vitini)yaruhusiwe.
Mdau
Kimanzichana.
Nice contribution, well explained and to the point. k, sasa kunamijitu mingine wao hawana kitu positive kuweka mezani zaidi ya kuponda na kuongea pumba. Sasa wewe annony 12:13:00pm nani kakwambia presidential convoy na ferry ndio chanzo kikubwa cha foleni dar labda unamatatizo ya ubongo.point ni kwamba kama mjini pangeachwa kwajili ya maofice na hizi biashara nyingine kusambazwa foleni lazima ingepungua.Mbona watu kibao waliamishwa toka imalaseko mpaka mlimani city.
ReplyDeleteMbona Hayati JKN aliishaliona hilo hata kabla ya ujio wa msongamano wenyewe na iliamuliwa makao makuu ya serikali yahamie Dodoma ( imo kwenye Katiba) - miaka zaidi ya 30 iliyopita - lakini hadi kesho serikali hiyo hiyo imegoma kuhamia Dodoma!!!!! Mashangingi mangapi ungeyaondoa katika barabara za Dar? Bongoland iache ilivyo tu!!!
ReplyDeletemi ushauri wangu ni kwamba kungejengwa vituo vya kupaki magari, mfano watu wanaendesha kutoka majumbani kwao mpaka kwenye vituo hivyo then wanaacha magari yao hapo na kupanda mabasi special ya serikali masafi A/C andni na kila kitu hakuna kusimama mpaka mjini kwenye vtuo karibu na makzi yao kisha mabasi hayo yanawarudisha vituoni na kuchua magarao.serikali ingetengeneza pesa kwenye parking na nauli za bussue hizo au hata train ni poa tuu.
ReplyDeleteKusema hakuta kuwa na foleni sio kweli, ila hayo uliyopendekeza yakifanyika , kutapunguza foleni. Peak/rush foleni itabaki kama miji mingine mikubwa duniani .
ReplyDeleteKinachonichanganya mimi ni hawa watoa maoni ambao wanatafuta neno baya la kusema kwa mtoa maoni. Yeye hayo ni maoni yake, kama una la kuongeza andika, badala ya kujifanya unashangaa walio ulaya.
Ikulu toka lini inatoa huduma za jamii hata tuihamishe ???
Viongozi hawawezi kutekeleza hili kwa sababu nao wako negative kama baadhi yetu hapa. Umaskini tunao, lakini ipo room ya improvement, taratiibu tutafika.
wacha ncheke..mbavu zangu mie!!!! yaani watu wanaongelea kuboresha kwa kutia lami barabara za pembezoni wa mji pamoja na kujenga bypass annoy mmoja hapo juu eti anaongelea "zijenjwe train zipitazo juu ya barabara" nafikiri huyu mdau anaishi tokyo au new york!!!!
ReplyDeleteusituzingue ndugu. kama hutaki foleni hamia Tanga au Unguja. Nchi yetu imeendelea na hayo moja ya vigezo vya maendeleo. Kwani huko London kwenu hakuna hayo maflaiova na bado kuna foleni? Wabongo mkienda ulaya mnajisahau saana - usikute umetokea mbalali halafu ulaya kwenyewe umekwenda mwaka huu. kula krismas na familia yako. hawa mawaziri na viongozi wote wamefika huko London kwako na hawaoni haja ya hayo maflaiova. Krismas Njema Mtanzania!
ReplyDeletemim nafikiri unaongea kitu ambacho hukifaham,miji mikubwa yote inatatizo la foleni,jaribu kutembelea miji mikubwa mingine na sio London tu,
ReplyDeleteDar supermarket,mabank yapo kila kona,wezetu walikuwa na plan ya miaka mingi mbele tofauti na sisi,tunahitaji kubomoa maghorofa mengi sana ktk upanuzi barabara
Majuzi nilitembelea katikati ya jiji la Dar es Salaam, na nilitishwa na kasi kubwa ya ujenzi wa majengo marefu inayoendelea katika eneo hilo. Nilihesabu si chini ya majengo matano yenye ghorofa zilizopungua kumi yaliyokuwa yakijengwa. Hii inamaanisha kuwa katika kipindi cha miaka takriban mitano ijayo hali itazidi kuwa mbaya katikati ya jiji la Dar es Salaam kwa kuwa idadi ya watu watakaokuwa wakifanya kazi na kutembelea eneo hilo itaongezeka kwa kiasi kikubwa.
ReplyDeleteMtindo huu wa kubomoa majengo madogo na nafasi yake kujengwa majengo marefu (skyscrapers) katikati ya jiji utatupeleka pabaya na nina wasiwasi tutafikia mahala ambapo katikati ya jiji hakutaingilika. Huu ni mfano mzuri wa mipango mibovu katika kupangilia miji.
Dar kwa sasa inatakiwa kupanuka kuelekea pembezoni. Hakuna haja ya kuendelea kuweka maghorofa marefu katikati ya jiji. Sehemu hiyo ilishajaa zamani. Kinachotakiwa ni kuboresha barabara na miundombinu mingine inayounganisha sehemu kama Bunju, Boko, Tegeta, Ukonga, Kiluvya na maeneo mengine ya jiji. Taasisi kama Tanesco na TCRA zinapaswa kupongezwa kwa kuweka makao yake makuu pembezoni mwa jiji.
Uwezo wa Kuendeleza barabara tunao na upo na wa uhakika kuliko nchi jirani. Ufisadi umezidi kwa hivyo hakuna anaefikiria kingine zaidi ya matumbo yao. Subirini Wazungu wachukuwe nchi wakishashiba tu mtaona barabra zinatengenezwa za kila mtaa, Lakini wakati huo wajukuu zetu watakuwa wameshachapwa viboko vya kutosha. Wewe endesha gari yako kwenye follen kwani hiyo starehe ya barabra nzuri ni ndoto za bunuasi hutaiona kwa leo au kesho ukiamka. Na hakuna suluhisho mapka mafisadi wote na viongozi wanochumia matumbo yao waondoke. Michuzi usibanie hii. Kuna wataalamu wa barabra Watanzania wametunikiwa pongezi nyingi kwa kazi nzuri wanzozifanya lakini hawan nafasi kwenye nchi yao ya kuendelza miradi kama hiyo, kwa sababu hiyo hongo hawaiwezi.
ReplyDeleteMtau umetoa ushauri mzuri sana na watanzania tunakushukuru kwa hilo. Tatizo linakuja pale pale kwenye utekelezaji serikali yetu imekuwa ikitoa ahadi lukuki kuhusu uboreshaji wa miundo mbinu ila mpaka leo imekuwa porojo tu. Swala la congestion charge kwa sasa Dar nadhani lingefaa kuna watu hawana shughuli za msingi mjini wanakuja na magari ilimradi tu kwa sababu wanayo. Sijaelewa kwa nini mpaka sasa Dala dala bado zinajazana kati kati ya jiji, kwani si tuambiwa uda inachukuliwa na wa sauzi imekuaje? ingesaidia kuweka usafiri wa mabasi ya kistaarabu na dala dala zisiondolewe ila zipige kazi nje ya mjini.
ReplyDeleteKuhusu swala la leseni ni la msingi mno serikali inauwezo wa kukusanya mapato ya hali ya juu kwa faini itakazopiga wavunja sheria za barabarani nina uhakika 60% ya madereva wa dar hawana leseni. kuna mdau hapo juu kapinga swala la huduma vitongojini...mbona hili swala limeshaanza kufanyika?sasa hivi kuna cashpoints kila kona mabank, masoko makubwa supermarkets hilo bado kidogo ila cha msingi hili swala limeshaanza kufanyika..kweli itatuchukua muda kufikia level ya ulaya ila na sisi wa-daslam turidhike na hizi huduma za vitongojini sio mpaka tuende mjini basi ndo tuonekane babu kubwa....
Asante na Xmass njema!
Mdau CV1.
very wise ideas, viongozi ndio wanaoiua tanzania. wakati nchi yetu nitajiri na ina kila kitu cha kujivunia. me ningeomba waweke pia BUS LANE. madaladala na maroli yote yapite line moja na magari madogo yapite line yake kwisha. then waanze kukamata magari yanayopita njia sio zake na faini wapewe risiti ya kulipia kwenye agency wakukusanya mapato hayo then pesa itumike kuboresha hizo hizo barabara. but kama wazo hili halifai Basi watu wasiruhusiwe tena kuja kuishi dar es salaam tena. waambiwe mji umejaa. nawale ambao hawakuzaliwa hapo wakafanye kazi na kuishi kwenye miji yao mikoani. tena ndio watapeleka maendeleo huko. hata baba zetu warudi makwao . tubakie tuliozaliwa na ushahidi uwe nao kwamba uezaliwa na kusoma dar. maana mijitu kila kukicha inakuja dar dar dar. waje na VISA sasa yakutembea tu na sio kuishi. hahahahahahahaaha. ndio ukweli wenyewe
ReplyDelete