Meza kuu wakiitikia dua, kutoka kulia mwenye miwani ni mwenyekiti wa madrasa sheirk Amran Rashid, akifuatiwa na mgeni rasmi ustaadh Suphian Masasi, anayefuata kulia kwa mgeni rasmi ni mratibu mkuu wa madrasa \Mufti Haji (mwenye bargashia) na anesoma dua mwisho kushoto ni mwalim mkuu wa madrasa ustaadh Hakim
Wa kwanza kulia mwenye shati ya mistari ni ustaadh Mudhuhir akiwa na baadhi ya wazazi wa wanafunzi wakiitikia dua maalum
Wanafunzi wa madrasa wakifuatilia kwa mazingatio mawaidha maalum yaliyotolewa na mwalim mkuu wa madrasa ustaadh Hakim
Wanafunzi wa ngazi ya masahafu kuanzia juzuu ya tatu (3) hadi juzuu ya kumi (10) wakidurusu na kutafsili baadhi ya Aya kulingana na sura aliyofikia kila mmoja wao. mbele ya wazazi na wageni waalikwa.


Asalaam aleykum kaka Michuzi na wasomaji wote wa Globo hii,

Tuanze kwa kumshukuru Allah Subhana wataalah kwa kutujaalia, afya na uhai kufikia hapa tulipo leo hii. Pili Allah aijalie globo hii maendeleo yenye kukuza upendo, amani, ushirikiano na furaha kwa wasomaji wote wa globo hii "INSHAALAH"

Sisi ndugu zenu wa Madrasat Muhamad ya hapa LEEDS tuliandaa sherehe maalum ya kuwapongeza na kuwazawadia wanafunzi wote waliomaliza juzuu Amaa katika muhula huu, na kwamba kuanzia tarehe 05.01.2011 mwanzo wa muhula mpya ujao, wanafunzi hawa wataanza kusoma Masahafu.

Sherehe ziliandaliwa katika ukumbi wa madrasa wa Ebbo Garden Leeds Mjini zilianza saa 3.30 Asubuhi mpaka saa 6.30 mchana, Sherehe ziliadhimishwa kwa usomaji wa kuraan wa aina mbalimbali kwa wanafunzi wahitimu na wanafunzi wakongwe. Mawaidha kutoka kwa mufti Haji na ustaadh Hakim yalikuwa ni sehemu kuu ya msingi na muelekeo wa sherehe yenyeweri wa .

Na mwisho kabisa wahitimu hawa wadogo wenye wastani wa umri wa miaka 7 walizawadi bahasha maalum kila mwanafunzi. Mgeni rasmi katika sherehe hii alikuwa Ustaadh Suphian kutoka chuo kikuu cha Leeds.

Tunawaombea dua vijana wote waliofanikiwa kufikia hatua hii. INSHALLAH , waendelee na masomo zaidi na waje kuwa mwanga wa amani na taa ya umoja, furaha na upendo katika jamii. Na wewe neema kwa wazazi wao na jamii yote kwa ujumla.

Afya njema, Amani, furaha na upendo kwako wewe Issa wa Michuzi na wasomaji wote wa globo hii

Asalaam Aleykum
Amran Rashid (mwenyekiti)
na
Sheirk Khasim Mintonde (Katibu).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Hii safi saana!!!

    Jitahidini zaidi ya hapo tuisimamishe Dini kwa vizazi vyetu vyote!!!!! Inshalaah Allah atatia uwezo wake kwa kila hatua!!!

    Hamis, (Norway)

    ReplyDelete
  2. Hadj Drogba "mwana chelsea"December 20, 2010

    Nimefurahi sana kuona wenzetu walioko ughaibuni dini hawaiachi nyuma na wamechukua jitihada za makusudi kuwajengea vijana wao wadogo misingi ya kuijua dini yao,wengi huwa tunajisahau hasa tunapokua katika kilele cha mafanikio ya kidunia ilhali tumeambiwa tuyakazanie yote;
    "SHUGHULIKA KWA AJILI YA DUNIA YAKO KANA KWAMBA UTAISHI MILELE LAKINI PIA SHUGHULIKA KWA AJILI YA AKHERA KANA KWAMBA UTAKUFA KESHO"hili ni agizo toka kwa kiongozi wetu MTUME MUHAMMAD (SAW).

    ReplyDelete
  3. Assalaam Alaykum,

    NAwaombea kila la KHERi watoto wote waloshiriki ALLAh SWt awazidishie Elimu ya Dunia na Akhera na iwe manufaa kwa Umma wa Dunia Nzima ... na nawaombea wote walioshiriki kwa pamoja kufanikisha haya na ALLAh awajaalie mfanye makubwa zaidi ya haya kwa uwezo wake SWT...

    Kaka michuzi na wewe tunakuombea Afya njema na Swiha njema wakati wote na ALLAh SWT akulinde na MAhasidi Allahumma Amin

    Kila laKheri

    ReplyDelete
  4. inapendeza sana WALLAHI Mwenyezi Mungu awafanyie wepesi wote walioshiriki kulifanikisha Hili
    Jumanne (India)

    ReplyDelete
  5. tumefurahishwa na juhudi za walimu na wanafunzi lakini jee CHUO CHENU HAKINA MIKWAJU? MAANA ISIJE KUWA TUNALETA WANAFUNZI WANAPATA BAKORA,NA MAISHA YA HAPA YANAJULIKANA KWA WAZAZI MARA LEO UNAFANYAO KAZI MARA HUFANYI KWA HIYO INAATHIRI MWENENDO WA MTOTO KUHUDHURRIA SHULE AU JE KUNA UTARATIBU GANI? maasalam

    ReplyDelete
  6. mashAllah, keep up with the great job. Mmbarikiwe

    ReplyDelete
  7. Nimefurahishwa sana na hili. Huwa nafikiri kuwa tukitangulia mbele za haki watoto wetu hawatajua cha kufanya huku nyuma, maana siku hizi tumekazania sana elimu ya kiwestern ( sipingani na western Education, najua tunaihitaji) na kupuuzia sana elimu ya dini. Nimefurahi saaana, kuona kuwa vijana wanafundishwa dini yao.

    ReplyDelete
  8. Nzuri sana Vijana Mungu awabariki pamoja na wazazi wenu na walimu wenu nasi sote tulio katika njia kama hiyo yenu ya kujifunza jitahidini sana kuisoma Qur-an kwani ndio Muongozo Mkuu wa Maisha kwa asiyetaka Potea.
    Ghalib
    Al-azhar University(Cairo)

    ReplyDelete
  9. Allaah awalipe kheri awali (hapa duniani) na huko akhera (siku ya hukumu/mwisho)

    ReplyDelete
  10. asa mbona wamevaa viatu?

    ReplyDelete
  11. Hİİ İNATUFUNDİSHA SİO KILA ALIYEKUWA UGHAIBUNİ Nİ WAKUJİLUSHA WAPO AMBAO WANAOTAFAKARİ JUU YA AKHERA YAO.mdau İSTANBUL.. UBATANİ.

    ReplyDelete
  12. Mashallah mwenyezi mungu awaongoze na awaongezee kila lililo na kheri na wao, yaani hii inatia moyo sana, inshallah mungu azidi kutupa wazazi moyo wa kuwapa elimu ya dini wanetu popote pale tulipo


    Mdau Amsterdam

    ReplyDelete
  13. MASHALLAH MASHALLAH MASHALLAH.MWENYEZI MUNGU AWAZIDISHIE WANAFUNZI WALIMU NA WAZAZI WAO KWA KAZI NZURI MUIFANYAYO.WATU WA LEEDS MNAONYESHA MFANO MZURI KWA MIJI MINGINE HUKU UK KUIGA,NIMEFURAHI SANA KUONA MAMBO MAZURI,MAANA UKIFUNGUA INTERNET SIKU HIZI MIFANO YA WAISLAMU WA UK NI YAKUSIKITISHA.MUNGU ATATUONGOZA SOTE INSHALLAH.
    MDAU UK

    ReplyDelete
  14. Ni ishara nzuri katika muongozo na maadili ya vijana wetu,inshaallah itasambaa ughaibuni yote.
    NA WEWE ANONY Mon Dec 20, 09:54:00 PM UNAYEJIITA MDAU WA ISTANBUL,UMETOKA WAPI TENA KUDANDIA MAJINA YA WATU?MDAU WA ISTANBUL ANAYEJULIKNANA NI MMOJA TU,KWA HESHMA YA MBULI TAFADHALI USITUMIE TENA HILO JINA
    MDAU HALISI WA ISTANBUL

    ReplyDelete
  15. Swali zuri na takujibu kwa kama ulivouliza viatu ni vinakatazwa msikitini tu, wala havijakatazwa popote au wakati unasoma Qur an au vinginevo hata kusali unaweza kusali navo kama ni dharura kwani salaa ni muhimu hata ukiwa safarini au mgonjwa unatakiwa usali kadri unavoweza na viatu au kibla unachoweza hivo viatu si haram.

    ReplyDelete
  16. Mungu awape moyo wa fahamu zaidi na kuweza kuisimamisha dini, najuwa ni ngumu sana hasa katika nchi zisizoongozwa na dola ya kiisilam ila Allah yupo pamoja na kila mwenye kufanya juhudi katika Dini

    ReplyDelete
  17. Aslm Alkm!Ma'ansha'Allah!ahiyo iko Bomba!Big up vijana wa kiislam!Insha'Allah Mola atakuwezesheni kwa kila hali Uislam Usonge mbele!Atainusuru Tu Dini yake Insha'Allah>Hi Mdau wa Tue Dec 21,05:17.00 am,,,Mimi sikutegemea kama Waislam wa UK wanajali Dini nimeona nilivyofika huku,Jaman ya Kaizali tumpe Kaizal!Hata vijana wa Kiislam walokuwa wakiipuuza Dini yao naona walivyofika huku utafikiri ndo wameelezwa maana kamili ya Uislam.wamekuwa Wacha Mungu Hamssa Salawath mpaka nashangaa sikutegemea,,,Hiyo Uk ulosema ni IPI HIYO?Hata wazubgu wanaoslim hao ndo usiseme,,Jamani Inafurahisha mno,si UK hiyo ya Zamani maana nilisikia Ulaya hakuna Dini.Ni Mejionea Kweli Mwenyezi Mungu ndi Mola wetu na,Uislam ndio Dini Yetu na Muhammad ndio Mtume wetu!Ma'assaallaam!

    ReplyDelete
  18. Manshaalah mola Awajaalie wazazi woote kwa kuhimiza watoto wao kusoma dini pia wote waanzilishi na wanaowezesha mashindano hayo kufanyika kwa imani na kuipenda dini yao.

    Allahwakbar! Allah karim!!

    Chef Issa

    ReplyDelete
  19. Amazing,hii inathibitisha kuwa uislam unaweza kuwa adopted by people of different cultures bila kuharibu utamaduni wao.bravo wanafunzi wote NOORDIN NSUBUGA Tanzania

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...