Mojawapo ya mabasi ya Sumry

Habari za uhakika zilizotua punde kutoka mtandao dada wa Globu ya Jamii wa Iringa www.francisgodwin.blogspot.com zinaeleza kuwa watu wanane wamekufa papo hapo na wengine zaidi ya 22 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la kampuni ya Sumry ambalo walikuwa wakisafiria kutoka Dar es Salaam kwenda Iringa kugongana na lori eneo la Mikumi mkoani Morogoro.

Habari zinasema ajali hiyo imetokea majira ya saa 9 Alasirileo wakati basi hilo likitokea Dar e Salaam na kuvamiana na Lori hilo lililokuwa likitokea mkoani Iringa, ikisadikiwa kuwa kutokana na mwendo kasi lori lilishindwa kupishana vyema na basi hilo na kuishia kugongana na basi hilo.

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Morogoro Afande Ibrahim Mwanakurwa ameuthibitishia mtandao huo kutokea kwa ajali hiyo na kuwa madereva wote wawili wamekamatwa .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...