Globu ya Jamii na Marafiki katika kumsaidia mtoto Abdully imefungua akaunti maalumu kama wadau mlivyoomba ili ikiwezekana asaidiwe yeye na baba yake. Vile vile msaada sio lazima pesa bali hata nguo, viatu na vitu vingine kwa ajili ya mtoto kama Abdully. Kutoa ni Moyo. Akaunti hiyo ni:
ACCOUNT NUMBER 014194
ABDUL MAHMOUD MIRROW
FEDERAL BANK OF MIDDLE EAST LTD
SAMORA BRANCH
DAR ES SALAAM
SWIFT CODE: fbmetztz
Kwa maelezo zaidi piga kwa Auntie Mariam
+255 754 280 495
FEDERAL BANK OF MIDDLE EAST LTD
SAMORA BRANCH
DAR ES SALAAM
SWIFT CODE: fbmetztz
Kwa maelezo zaidi piga kwa Auntie Mariam
+255 754 280 495
Tuombe msaada kuwasaidia wenzetu ambao ni
mtihani kutoka kwa Mwenyezi Mungu...
mtihani kutoka kwa Mwenyezi Mungu...
Ninakuomba kama mtanzania mwenzangu tupeane hamasa ya kupendana na kusaidiana sio katika sherehe za starehe tuu, zaidi siku hizi tuzidishe kusaidiana katika shida maana sasa shida zinazidi siku hadi siku.
Katika pitapita zangu, nimekutana na mtoto huyu Abdully mwenye ulemavu wa viungo huko Kaole, Bagamoyo. Kula kwake kwa taabu, haongei, ingawa anacheka akifurahishwa, na kulia kwa kupiga kelele akiudhiwa au akiwa na maumivu ingawa hawezi kuelekeza maumivi yako wapi.
Cha kusikitisha, mama yake mzazi amemkimbia mtoto na mume, baba nae ameanza kukata tamaa ya mwanae kwa kukosa muelekeo na msaada (support). Baba (Bw. Hamoud) anaishi na mama yake mzazi ambaye ni mtu mzima mwenye matatizo ya kiafya, macho na thyrod eshafanyiwa upasuaji nk... sasa Bw Hamoud ameacha shughuli za kutafuta fedha za kukimu maisha ili aweze kumlea kijana Abdul (4) ananza asubuhi kwa kumuosha, kumlisha kifungua kinywa..... mchana kumlisha anakula kwa taabu maana ulimi hauzunguki sawa sawa kama vile umepooza, na koo halimezi vizuri.... jioni anamsafisha na kumlisha.... maisha yamekuwa duni, kwa hivyo hata malezi ya Abdul yamekuwa magumu mno...
Alishauriwa ampeleke hospitali ya CCBRT, nae baada ya kwenda hapo alishauriwa ampeleke kwa physiotherapy kila wiki, tatizo la Bw Hamoud ni usafiri kutoka Kaole hadi msasani CCBRT ni wa daladala na mtoto mwenye ulemavu wa viuongo si mchezo... mlemavu wa aina hii anaweza kuwa na haja kubwa au ndogo mahali popote wakati wowote hata mkiwa ndani ya daladala huduma yake ngumu hapo ni mtihani...
Hapo CCBRT wanaweza kushinda kutwa kabla ya kupata huduma kipindi hicho cha kusubiri mtoto amebebwa au kupakatwa, chakula hakuna, na pahala pa kumlaza aweze anaglau kunyoosha viuongo hakuna. wahudumu wanapita na kumuangalia hapo katika foleni bila kumpa tamaa au hata nasaha. Jioni usafiri wa wa kubanana ndani ya daladala kurudi Bagamoyo, pikipiki hadi Kaole.... Baba Abdul kaishiwa nguvu ameshindwa. Wapo Kaole wanasubiri hatma ya Mwenyezi Mungu.
Abdul amepewa ki "baiskeli" cha mtoto (push chair) na akiwekwa hapo lazima afungwe na khanga ndio akae kwa usalama na kwa sasa anabanwa hapo....
Hivyo basi Kama kuna wasamaria
wenye huruma na hali hii, wanaomba:
1. Wheelchair ya kawaida Abdul akae
kwa usalama na awe na nafasi viungo viwe huru
kwa usalama na awe na nafasi viungo viwe huru
2. Ushauri kwa kiafya
3. Ushauri wowote, na msaada wowote
utakaoweza kutoa afueni kwa Abdul na baba yake Hamoud
utakaoweza kutoa afueni kwa Abdul na baba yake Hamoud
mpigie simu Hamoud
+255 757 652449 na +255 787 771566
kwa msaada au ushauri. Juhudi za kufungua
akaunti maalumu zinafanywa kwa wenye
kutaka kumsaidia mtoto Abdully
+255 757 652449 na +255 787 771566
kwa msaada au ushauri. Juhudi za kufungua
akaunti maalumu zinafanywa kwa wenye
kutaka kumsaidia mtoto Abdully
Mdau Dar
Mtoto Abdully anaomba msaada wako
Abdully akiwa amebebwa na nyaya yake
Abdully anasimama na kulala kwa shida...





Wadau akaunti ndio hii sasa kama ilikuwa ni nguvu ya soda tutaona, ngoja nianze utaratibu wa kwenda benki wadau shime shimeeeee, michuzi utupe na taarifa kama kinaeleweka ili tujue wadau wa blog ya jamii sio porojo ni vitendo
ReplyDeletemdau canada
Dah imekuwa kutishiana nyau tena mdau mtoa maoni wa kwanza hapo juu.
ReplyDeleteyeah wote tuliokua tukililia account kazi kwetu sasa, tukumbuke leo kwa mtoto wa mwenzetu kesho wa kwa watoto wetu....
ReplyDeleteTuko tayari kabisa kusaidia ila kuna maelezo muhimu yanahitajika.
ReplyDeleteMoja: gharama za baiskeli ni ngapi
Mbili: nani atasimamia hizo fwedha ili haki ya huyo mtoto isipotee.
tatu: Uthibitisho wa Nani Mlezi au Mzazi wa huyu mtoto
NNe: Nani atasimamia na kuhakikisha kuwa kitakachotolewa kitamfikia mtoto.
Hivyo ingekuwa vizuri sio tu kuomba msaada bali kuwe na kautaratibu chenye kueleweka ili kila mtoaji aridhike kuwa hela au msaada utafika kwa mlengwa.Niko tayari kabisa kutoa £50ya maboksi kuchangia mfuko huo kwa utakuwa unaeleweka.
Mzawa
DAAH! TUNASHUKURU KWA KUFUNGULIWA AKAUNTI HIYO....LAKINI HII AKAUNTI NI YA UBAGUZI KWA SISI WA MIKOANI NA WILAYANI, HIYO BENKI MLIKOFUNGUA AKAUNTI NETWORK YAKE SIO KUBWA HIVYO KUTUKWAZA SISI TUNAOTAKA HELA YETU IINGIE MOJA KWA MOJA KTK AKAUNTI YA ABDUL. KUNA BENKI MBILI TU HAPA TANZANIA AMBAZO ANGALAU UNAWEZA KUIKUTA KILA SEHEMU NA SISI WA MIKOANI TULITEGEMEA MNGEFIKIRIA HILO ILI KUPATA MICHANGO ZAIDI...(NI NMB NA CRDB BANK).
ReplyDeleteUSHAURI: SIKU NYINGINE KAMA KUNA TATIZO KAMA HILI TWAOMBA AKAUNTI IFUNGULIWE KTKT MOJA YA HIZO BENKI MBILI NA HASA NMB SABABU MTU WAWEZA TUMA HELA KWA KUTUMIA SIMU YA MKONONI POPOTE ULIPO (NMB MOBILE) NA KUONDOKANA NA KUTUMIA MUDA MWINGI KWENDA BENKI KUTUMA HELA NDOGO AMBAYO PENGINE INAWEZA KUKUTIA UVIVU KWENDA KUTUMA UKICHUKULIA TIME LIMIT KWA WA DSM NA NON AVAIILABILITY OF THE BANK BRANCH KWA SISI WA WILAYANI.
NILIAHIDI TSHS.50,000.00 NA NATAKA KUTOA KWA DHATI HELA HIYO TATIZO NIKO WILAYANI NA SIJUI NITAFANYAJE KUWEZA KUINGIZA HELA HIYO KATIKA AKAUNTI HIYO YA FBME AMBAYO BRANCH NETWORK YAKE IS SO LIMITED....MSAADA TUTANI PLEASE.
MDAU 0767528272/0655528272
Dah,
ReplyDeleteSi mchezo ukisikia Mungu anakupa mitihani ndio kama hivi, sio eti unakosa pesa ya bia unaanza kumlaani M/mungu kuwa eti akupendi kwakuwa sikuhizi akupi pesa ya bia. mitihani ya maisha ni kama ya babayake Abdul hapo M/mungu anampima kuona kama ataweza kumlea mtoto u na yeye atakimbia kama mama yake. Inshah Allah shime shime jamani tumchangie mwenzetu kwenye ili. Mimi sina pesa ila nitaanza na 50,000 tu kwa leo na Inshah Allah kadri M/mungu atakavyoniwezesha siku za mbeleni nitakuwa naongeza na kuziweka ktk account hii.
Muddy Nice
Mzee mzima Michuzi
ReplyDeleteSababu swala zima ni kukusanya faranga na ilhali si kila mtu yupo Dar au ana ana muda/access na hiyo bank, nashauri yafuatayo:
(1) Ikiwezekana pia aweke namba kwaajili ya wadau wa kutuma hela kwe M-Pesa, Z-Pesa au M-Pesa.
(2) Kuna watu tuko huku madongo kuinama, ni NMB tu ina branch na CRDB had wilayani (atumie hata za nduguze). Ikiwezekana aweke account hiyo. Akidiposit mtu, atume sms kwa mhusika ili hela iweze fuatiliwa.
(3)Money Gram/Western Union inaweza tumika, kwa wadau walio ughaibuni.
(4)Ripoti ya fedha iwekwe wazi baada ya mtoto kutibiwa.
Suleman,
Kilwamasoko
Kama kawaida yao waswahili doma kaya wameanza.mara nini sijui nini. wewe toa pesa kama kweli mtoaji. kama ni kwa M-Pesa namba ya simu ya baba mtoto unaiona hapo. mpigie kisha muulize utume lini. mara ohh sijui nini. mwisho mtaanza kusema ankal sijui nini. hadi hapo sijaona mtoaji. wamatumbi utawajua tu wanapotaka kuchomoa. hamna hata haya. mie nshatuma 20$ za boksi najisikia roho swafiiiiiii. hata mtu akiila hiyo itakula kwake kwa Mungu. Dah! Waswahili bwana. Ankal akifanya hivi oooo sijui nini. asipofanya mnamsumbua ah! bahati yenu kaka watu hana nongwa. ningekuwa mimi nisingejisumbua na jambo la mtu kha!
ReplyDeleteMdau Dada Kachiki
UK
Kwanza nimpe pole kwa kuuguza mtoto wake asife moyo mungu atamsaidia tu.
ReplyDeleteMimi nijaribu kumpa ushauri yeye na watu wengine wengi tu ambao wana watoto kama hawa wako wengi wengine wanawaficha ili wasionekane.
Ugonjwa huo unatibika kwa mazoezi daktari yeyote atakushauri mazoezi huko Muhimbili au CCBRT ambao wana vitengo maalumu kwa ajili ya watoto kama hawa...ILA SASA mtoto anajikuta hapati mazoezi ya kutosha kwakuwa wale wataalamu pale ni wachahce na wagonjwa(watoto) wanakuwa wengi hivyo nao huchoka(kwa mtazamo wangu)
Naomba niwashauri ndugu hawa kuna kituo kiko DODOMA sehemu inaitwa MLALI wao wantoa huduma kama hiyo ya mazoezi na gharama zake si kubwa sana..Hapa mtoto anapata mazoezi kila siku na wanavifaa vya kutosha..Kinaendeshwa na KANISA KATOLIKI...Hapa anaweza pata nafuu au kupona kabisa...
Pia hapa dar es salaam kuna Daktari pale Magomeni Mikumi yeye anatibu magonjwa ya MIFUPA hata hili anadawa za kuzuia kukakamaa kwa misuli kunakofanya mtoto anajivuta na kujipindisha kama huyu hana bei kwa watoto..Pia atakuelekeza kwa kina mama wanatoa dawa za watoto....Natumaini unaweza ona mabadiliko makubwa sana kwa mwanao hata kama hatarudi kama kwaida but tofauti itakuwa kubwa sana....
MWAKA JANA NILIWAHI MPA USHAURI MAMA WA TABATA ALIJITOKEZA HUMU KAMA HUYU LAKINI ALINISIKITISHA PAMOJA NA JUHUDI ZANGU KUOMBA NAMBA KWA MICHUZI NA KUTAFUTA POST YA HABARI YAKE MWISHO WA SIKU NAMFUATA ILI NIMWELEKEZE YOTE HAYA aliingia mitini iliwia tabu kumuelewa.Unapokuwa na mgonjwa kama huyu ni unatakiwa kila mlango salama upige hodii ili kuzuia mtoto asipate madhara zaidi.....
....NINAYAZUNGUMZA HAYA KWANI NINA CASE KAMA HII ILA NAMSHUKURU MOLA NI MWAKA WA TATU HUU NA DOGO ANAONYEHSA MATUMAINI MAKUBWA SANA ...ndugu usikate tamaa ....NITAMTWANGIA KUMPA MAELEKEZO ZAIDI
kwakuwa wengi tumejitokeza kutaka kutoa misaada lakini swala la benki linazorotesha vitando vyetu. Tunaomba ifunguliwe akaunti yenye jina la mtoto kwanza likifuatiwa na jina la mzazi au madhamini kwenye benki ambayo ina matawi mpaka wilayani kama CRDB au NBC ili iwe rahisi hata kudhibiti matumizi ya pesa zitakazo wekwa huko hata kama zitakuwa ni pesa za chakula au nini lakini zisichanganyike na pesa nyingine za mzazi au za mlezi. Kutuma pesa toka nje ya nchi inakuja moja kwa moja mpaka hizi benki kama CRDB, NBC , lakini ukituma kwenye hii bank watazungusha kwenye hayo mabenki makubwa mpaka zifike huko hata huo msaada wa haraka hautakuwa na maana. Simu nazo hazipatikani na nyingine haipokelewi. Patrick +4741629677
ReplyDeleteNASHAURI PIA HUYO MLEZI WAKE AMPELEKE CCBRT, KWANI PALE WATOTO KAMA HAO WA CP WANAHUDUMIWA NA PIA MLEZI ATAPEWA MAFUNZO YA KUMHUDUMIA AKIWA NAE NYUMBANI, NA PIA VIUNGO VYAKE VITAFANYIWA MATIBABU YANAYOSTAHILI.WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO WANATIBIWA BURE.
ReplyDeleteDADA KACHICHI USITAKE KUCHAFUA HALI YA HEWA NA WEWE UNAONYESHA ULIVYO MMATUMBI ASILIA. INAPOITISHWA HARAMBEE NA AKAUNTI KUFUNGULIWA INAKUWA RAHISI BAADAYE TULIOCHANGIA KUPEWA TAARIFA ZIMEPATIKANA NGAPI BADO NINI LABDA TUENDELEE KUCHANGA AU ZIMETOSHA. SASA HIYO M-PESA INAINGIA KTK SIMU YA MTU TUTAWEZAJE KUMONITA/KURATIBU NA KUWEZA KUPEWA TAARIFA SAHIHI YA HELA KIASI GANI ZIMEPATIKANA.
ReplyDeleteKWAHIYO TUNAVYOSEMA KUWA SISI WA WILAYANI HIYO BENKI MLIKOFUNGUA INATUKWAZA USIFIKIRI HATUTAKI KUCHANGA WALA TUSINGEJISUMBUA KUOMBA AKAUNTI SI TUNGENYAMAZA KIMYA TU ILA TUNATOA MAONI ILI SIKU ZA MBELE KUKIWA NA TUKIO KAMA HILI IWE RAHISI KILA MTU ANAYEJISIKIA KUCHANGA APATE URAHISI KUCHANGIA KUPITIA BENKI YENYE BRANCH NETWORK KUBWA NA NI RAHISI KUPATA TAARIFA KILICHOCHANGWA KWA WARATIBU WA ZOEZI KUOMBA BANK STATEMENT NA KUWAPA TAARIFA WACHANGIAJI, LKN M-PESA INAKUWA SIO RAHISI SANA KUPATA TAARIFA ZA MICHANGO YOTE NA IMEFANYA KAZI GANI. HUU NI USHAURI YAKITOKEA MATUKIO MENGINE SABABU TUNAPOCHANGIA TUNA SABABU YA KUCHANGIA.
MDAU