leo kipofu kaona mwezi. ankal kapata noti mpya alipokwenda ATM kudroo hela ya weekend. anasema tunoti tuzuri kweli hata kutumia anaona kama atatuonea. amefurahi kweli maana alipata kusikia redio mbao kwamba noti mpya zimechakachuliwa. Wamatumbi bwana! saizi yake ni sawa na ya dola ya kimarekani ama jero la kitanzania. hizo juu ni buku tano tano na kwenye pochi zinafiti uzuri kweli tofauti na minoti ya zamani mipana kama gazeti daily news.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. hahahhahhahah,nimeipend aulivyoiandika hii habari!! za zaman kama gazet la daily news??
    nawe angalia ucjeruh hisia za watu ankal

    ReplyDelete
  2. pesa nzuri lakini inafaa sasa jamii ifundishwe matunzi mazuri ya pesa,
    kwamfano makonda, wafanya bishara ndogo ndogo kama mkaa,sokoni,baharini,machimboni,n.k ni waharibifu wa kubwa wa pesa.
    Matumizi kama ya Pochi hapo kwetu ni kwa wachache tu,wenye uhakika wao.

    ReplyDelete
  3. TATIZO KUBWA LA WATANZANIA BADO HATUJUI KUHIFADHI PESA, UNAKUTA MTU ANAIKUNJA PESA MARA 10 NDIO ANAIWEKA MFUKONI, KINA MAMA WANAZIFUNGA KWENYE MAFUNDO YA KANGA, NAKAZALIKA, BASI MUDA MFUPI TU UNAKUTA PESA ZIMESHACHOKA, MFANO BAADA YA TOLEO LA MSIMBAZI NAKUMBUKA NILIPATA BAADA YA WIKI 2, ILA ZILIKUWA KAMA ZIMETUMIKA MWAKA 1. HIZI MPYA PIA MTAONA BAADA YA MWEZI 1, TUTAANZA KUZIPOKEA ZIKIWA ZIMECHAKAA TAYARI. SASA BASI WATANZANIA KWA UJUMLA TUJITAHIDI KUTUNZA PESA VIZURI ILI ZISIWAHI KUCHAKAA.

    ReplyDelete
  4. ngoja niwatume watoto wakuchomolee

    ReplyDelete
  5. Wewe ankal wewe kulisema gazeti la Daily News ndio nini?.Angalia waheshimiwa Six na Dairecta na BBC_TZ wako wapi na wewe yasijekukuta huko Daily News.Tunakuonea huruma

    ReplyDelete
  6. mimi napendekeza sheria juu ya utunzaji wa pesa, na je mnajua hakuna kitu kichafu kama pesa hizo, wengine wanafutia jasho na kupengea makamasi. Ukishika pesa lazima unawe mikono kabla hujala chakula vinginevyo unakula uchafu mtupu Kazi bado tunayo wabongo. Mungu tusaidie

    ReplyDelete
  7. Anonymous said...
    kuhusu namna ya kutunza pesa..wala tusiwalaumu watanzania...lawama iende kwa watu wenye mamlaka ya kuleta maendeleo kwa wananchi...watu wengi wa hali ya chini hawawezi kuweka pesa vizuri kutokana na hai halisi..huwezi kuniambia tumfundishe muuza mkaa namna ya kukunja pesa, wakati yeye hata asipoikunja tayari inachafuka...angalia watu wanaohifadhi pesa vizuri, wengi wao wana kazi nzuri au kipato cha afadhali...nchi ikiwa na maendeleo automatically hata namna ya kuhifadhi pesa itakua nzuri bila hata ya kuwapa watu elimu ya kuhifadhi pesa...

    ReplyDelete
  8. Hhahahahahah! Kweli ankal umenifurahisha sana jioni hii....jinsi ulivyoandika:)

    ReplyDelete
  9. JAMANI MIMI NINAOMBA KUELIMISHWA Haya yafuatayo:-
    1.Kwa nini tunatoa/tunachapa matoleo mengine ya hela?
    2.Babu yangu kule kijijini Berega anafaidikaje na hili zoezi?
    3.Kwanini wanaondoa elfu 5 na kuleta elfu 5 tena?
    4.Kama zimechakaa kwa nini wasichapishe toleo lile lile?
    5.Kuna muda maalumu wa kutumika toleo fulani, yani kila baada ya miaka kadhaa mfano 15 tunatakiwa kutoa toleo jipya?
    6.Je hili zoezi linasaidiaje kushusha au kupandisha thamani ya pesa yetu?
    7. Anaye "DIZAINI" ni nani?

    NB: Niliku kwenye bar moja nikasikia MFANYAKAZI MMOJA WA SILIKALI WIZARA NYETI AKIWA KALEWA NA KULOPOKA "walibadilisha sehemu ya kuzichapia baada ya kuahidiwa 10% kwani kule ubora utakua mdogo kiasi" sijui lina ukweli kiasi gani maana cku hizi bwana....


    Aksante natanguliza shukurani kwa majibu mtayonipa. YOYOTE YALE.
    Mlala hoi

    ReplyDelete
  10. Wabongo ni lini mtashukuru kwa kidogo mnachofanyiwa na Govt.yenu???Kila siku kulalamika na lawama kibao kila mtu fisadi ...Je kwenu aliye msafi ni nani???Tujifunze kutoa pongezi inapotakiwa mweeeeh.
    nawakilisha.
    Mdau wa Ukerewe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...