Kampuni ya Dowans leo imewasilisha rasmi maombi ya madai ya usajili wa TUZO katika Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam na kusajiliwa kwa kupewa namba ya usajili nane ya mwaka huu.

Kampuni ya Dowans ilishinda kesi ya madai dhidi ya TANESCO katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) na kuamuliwa TANESCO kumlipa Dowans Sh Bilioni 94.

Naibu msajili mwandamizi wa mahakama hiyo Mh. Salvatory Mwongole,ameiambia Globu ya Jamii kwamba maombi hayo yameifikia mahakama hiyo januari 25 mwaka huu na yamewasilishwa na wakili wa kampuni hiyo hapa nchini kutoka kampuni ya uwakili ya Kennedy Fungamtama.

Mh. Mwongole amesema maombi hayo yamekwishapangiwa jaji lakini kulingana na unyeti wa suala hilo jina la jaji linahifadhiwa kwa sababu ndio kwanza ameteuliwa kushughulikia maombi ya usajili huo na jalada halijamfikia.

Alisema maombi hayo ya usajili yameombwa na kampuni ya Dowans Holdings S.A na Dowans Tanzania dhidi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Kwa mujibu wa sheria TUZO hiyo haitasajiliwa hadi mahakama itoe nafasi kwa mdaiwa kuwasilisha pingamizi kupinga usajili wa Tuzo hiyo kama anaona haifai kusajiliwa, na kama hana pingamizi itasajiliwa kama imekidhi sheria na mdaiwa kulazimika kulipa fedha hizo.

Wadau wengine pia wana nafasi ya kuwasilisha maombi yao kama wanadhani usajili wa TUZO hiyo haustahili nayo pia yatapokelewa, Mahakama ikishasikiliza kama kuna mapingamizi itatoa maamuzi kama ni kuisajili au la.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Wakilipwa machafuko yatatokea...huu ni ujambazi wa mchana. Duh Maskini najuta kuzaliwa bongo.

    ReplyDelete
  2. Wasitutanie hawa Dowans. Wakitushinda mahakamani tunaiga Tunisia na Misri. Hii ni new generation bwana

    ReplyDelete
  3. Mi sijaelewa. Mwenye kujua taratibu za kisheria, atueleweshe zaidi maana ya 'KUSAJILI TUZO'. Naona nyota tu hapa

    ReplyDelete
  4. Hizi lugha za ajabu ajabu ndizo zinazotupelekea kutapeliwa miaka yoote !!Inabidi tueleweshwe hii "KUSAJILI TUZO"ina maana gani???au ndiyo njia ya kutafuta Dowans kulipwa kwa urahisi??Tuangalie sana sisi Watanzania naona tunakoelekea ni kwenye yale yale ya Tunisia na Misri !!!Vugu vugu hili linazidi tu kuteremke kuelekea kusini mwa bara la Africa,na si muda mrefu lityafika "Bongo"Tumechoka kuonewa na lugha mpya la kilaghai,na huu ndio mwisho wa "AFRICAN DICTATORS"Wimbi hili litawakumba wengi,majina tunayahifadhi !!!
    Mdau Usa.

    ReplyDelete
  5. Hata mimi sielewi hapo jamani.Hebu tusaidieni Wadau juu hiyo Tuzo ina maana gani. Wengine ni mbumbumbu kuelewa hizo Sheria za Kimahakama. Au DOWANS wameingia kwenye shindano la kupewa ZAWADI KWA UBORA? mbona itakuwa vichekesho.

    ReplyDelete
  6. Pengine makala iliyomo kwenye link hii inaweza kuwa na majibu yaliyoulizwa hapo ju:

    http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/99647-mahakama-kuu-ya-tanzania-kuzuia-malipo-kwa-dowans-3.html

    ReplyDelete
  7. kama mahakama imeshatoa hukumu kuwa walipwe waacheni wavute chao. sisi tunaotakiwa kuwalalamikia ni watanzania wenzetu waliosaini. lakini hela yao wachukue ili kuepusha adhabu kubwa zinazoweza kutokea endapo hawatalipwa kwa wakati. ujanja kupata!

    ReplyDelete
  8. KUSAJILIWA KWA TUZO: Ninavyoelewa ni kwamba, kwa kuwa kesi hii iliamuliwa nje ya nchi ya Tanzania(ICC-Mahakama ya Biashara kimataifa), uamuzi wake hauwezi kutekelezwa katika nchi husika, hadi hapo mdai(Mfano Dowans) asajili hukumu iliyotolewa katika mahakama ya Tanzania.
    Iwapo mhakama ya Tanzania itaridhia kusajili hukumu hiyo ambayo tayari ilishatolewa na mahakama hiyo ya kimataifa basi hukumu hiyo itakuwa halali kutekelezeka nchini Tanzania, ni kwa maana hiyo basi Tanzania ambayo ni mdaiwa itabidi ilipe hilo dai(Bilioni 94).
    Lakini kwa mujibu wa Taratibu madaiwa anapewa nafasi ya kuikilizwa iwapo ana pingamizi lolote, kuhusu kusajiliwa kwa Tuzo hiyo.
    Hii ni hatari sana sana jamani wabongo, yaani tulipe bilioni 94??? Ni pesa nyingi kupita kiasi ambapo itaacha nchi katika umasikini wa hali ya juu duniani.

    LAWAMA:
    Tukumbuke kujiuliza swali, kwanini tumefikia hapa tulipo hadi kupelekwa mahakama ya kimataifa? Ni wazi kuna vigogo inapaswa kuwajibika kuiingiza nchi katika mgogoro huu unaoligharimu Taifa mabilioni.
    Walioiingiza nchi katika mikataba ya kipuuzi na makampuni ya kipuuzi kama Dowans, wameisaliti nchi, haya ni yale yale kama ya kina Richmond.
    Hivi kweli watanzania kwanini hatuna uzalendo? Tutafika wapi kwa namna hii? Tuangalie nchi za Wenzetu, China, UK, USA, viongozi wako pale kulinda maslahi ya Taifa na wananchi, na wanajivunia iwapo wataleta mabadiliko, ya maendeleo ya nchi, ila kwetu bongo wanasisasa wako kidilidili, kiwiziwizi, kwa maslahi yao binafsi.
    Nchi hii haitabadilika iwapo sisi wenyewe hatutaamka na kusema, sasa tumechoka, we have had enough!!!!

    ReplyDelete
  9. Wenye kujua sheria fungueni kesi ya kupinga na tuwashinde kwa kutaka kujua mmliliki halali wa Richmonds kwanza na alipe fidai ya kutulaza gizani then tujue hukumu hiyo mpya itakuwa kama sio deni lake kwa watazania.Rais anaongea kila mwezi mbona amefunga mdomo kwenye hili?anamuachia waziri mwenye wizara husika ambaye alikuwepo toka mwanzo na hakuna jipya atatufanyia watanzania.Jasmine revolution inanukia bongo kwa kasi,wakilipwa hawa nasema vijana hakuna kuogopa mwendo mdundo tu

    ReplyDelete
  10. Madai ya usajili wa tuzo ni kuwa kwa kuwa kesi ilisikiliziwa nje ya Tanzania na ushindi ulitolewa nje ya Tanzania Dowans wanahitaji kusajili ushindi wao kwenye mahakama ya kitanzania ili wapate malipo yao. Kwa hiyo huu ni mwanzo wa wao kulipwa hizo hela zao Billion 94.

    ReplyDelete
  11. Kwanza, Dowans ni kampuni ya kitapeli! Huo ndio ukweli. Ndiyo maana hata uki-google Dowans International inatokea Tanzania tu na si kwingineno duniani? Pili, Iweje kampuni yenye thamani ya mabilioni haijawahi kufanya biashara kokote duniani? Tatu, Wamiliki wake pia utata mtupu. Kama huamini jaribu ku google majina yao na contacts zao.Nne, nani aliwashika mkono kuwaleta Tanzania? Mbona hatajwi? Iweje kampuni ifunguliwe TZ bila mwenyeji? Tano, Nani aliiwakilisha TZ kwenye kesi hiyo? Hatajwi??!! Waliosaini mkataba huo TZ ni kina nani? Hatua gani zinachukuliwa dhidi yao? Mwisho, Fedha za kulipa, kama tukishindwa ku-appeal zinatoka wapi? bajeti hiyo ilipitishwa na Bunge lipi? Ilweje kampuni feki ya Richmond izae kampuni halali ya Dowans?

    Mdau Lilly

    ReplyDelete
  12. MASWALI MENGI MAJIBU HAKUNA. NIMEAMUA KULIA TU AU TUWAFANYIE KISOMO MSIKITINI NA MAOMBI KANISANI WALAANIWE AO WEZI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...