Bendi kongwe nchini Mlimani Park Orchestra ikitumbuiza usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Break Point (ya mjini) jijini Dar ambapo kila Ijumaa wako hapo wakiwasha moto wa Sikinde. kuwasiliana nao piga +255 784 567 750

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Ankal! michuzi! tunakupigia Saluti!
    Hii ya Leo ya Sikinde,ni baab kubwa,
    maana hili ni somo,kwetu sote,kuwa
    wakongwe hawa mziki wao umepangiliwa
    kwanidhamu ya hali ya juu,tena ni mziki
    wenye mtindo wa dansi halisi la Kitanzania.
    TUnashukuru sana kwa Raha na somo hili la leo,
    Wadau
    FFU Ughaibuni
    (askari wasio na nidhamu)

    ReplyDelete
  2. Sikinde mko juu sanaaaaa. Ila, tofauti na msondo ngoma ambao wana damu changa kila kukicha, nyie mmejiandaaje endapo wakongwe Shaaban Dede na Bitchuka wakistaafu? Jamani wekeni vijana wawarithi. saa haigandi - Ushauri wa bure huo... ohooooo

    ReplyDelete
  3. FFU Ughaibuni mmenena! Ankal anatisha! yaani hadi sasa sijaona bloga wa kumfikia. hii ya kuweka video live ni kiboko. Ankal oyeeeeee!!!!

    ReplyDelete
  4. Kwanza pongezi Mlimani Park kwa kuelewa somo kuwa kutengeneza video na kuitundika YOUTUBE siyo 'issue' kubwa na huitaji gharama yoyote kubwa.

    Pili muziki wa hii clip ni kama FM Stereo, ila tu labda mpigaji video awe na taa ya kutosha kumulika au jukwaa la muziki liwe na mwanga wa kutosha kuongeza ubora.

    Tatu, YOUTUBE ni njia bora ya kuhamashisha vijana wa kizazi kipya kuelewa muziki wa dansi pia una nafasi kubwa ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania.

    Kazi kwenu wazee wazima wa muziki wa dansi, Sikinde wameonyesha njia ya kujitangaza kwa teknohama kupitia YOUTUBE, sasa Msondo Ngoma Music Band, Kilimanjaro Band(Njenje), Inafrika Band, Bana Maquiz, Wazee Sugu (King Kikii) n.k tunataka kuwaona kazi zenu ndani ya YOUTUBE.

    Ankal, tunashukuru kwa kutufungulia milango, huku Marekani ya Kati kama Mexico na Marekani ya Kusini kama Colombia,Venezuela n.k muziki wa Mlimani Park, Orch. Makassy na Matimila unapendwa vibaya sana.

    Mdau
    Jijini Gualadajara,
    Mexico.

    ReplyDelete
  5. Nginde iko juu sana kwa sasa kwa Bendi kongwe.Unapata ladha halisi ya muziki wa kitanzania. Hongera sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...