Ahmad Michuzi Jnr leo anasherehekea hepi besdei yake ya kuzaliwa akisisitiza ni vyema kumshukuru Mungu kwa kila jambo atendalo kwetu sisi waja wake, kwa maana yeye ndiye mwingi wa rehema siku zote katika maisha yetu. Globu ya Jamii inampa hongera kwa kuzaliwa leo na kumtakia maisha mema yeye na familia yake huku akiendelea libeneke katika kijiwe chake cha Jiachie ambacho anakukaribisha mdau yeyote popote ulipo.
BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Nakutakia Mwaka wenye mafanikio sana na Mungu akubariki. Mimi nafurahia sera za blog yako na misimamo huru isiyovutia upande wowote. Ninaomba blog yako ya JIACHIE izidi kupata umaarufu.

    Mdau, USA

    ReplyDelete
  2. Happy Birthday dear brother wa libeneke. Me and my family tunakutakia maisha marefu yenye mafanikio na afya tele. Tunamwomba Mwenyezi Mungu akulinde na kukuepusha na mabaya yote uingiapo na utokapo.
    Tunakutakia mwaka wenye kheri na utuletee habari zaidi katika picha za sehemu mbalimbali nchini kwetu. Kwa kweli umetufanya tuione dunia kuwa ndogo kwani Tanzania yote tunaiona kwenye screen! Unafanya kazi nzuri sana na tunakushukuru kwa hilo.
    Mwenyezi Mungu azidi kukubariki.
    MDAU WA DAMU USA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...