Nilisoma kwenye Globu hii ya Jamii na kwenye magazeti na kuona kwenye TV juu ya uamuzi wa Naibu Waziri Nyalandu kuwafukuza Machinga wageni sokoni Kariakoo.
Binafsi nautazama huu uamuzi kwa pande ya pili na kuona kama si sawa.
Kipindi hichi ambapo uchumi wetu ni wa soko Huria Mteja ndio ana nafasi ya kuamua nini anunue, anunue kwa nani na bei gani.
Bado kuna challenge kubwa sana ya ubora na soko la bidhaa la Tanzania kutumika kama Jalala la bidhaa duni hasa toka mashariki ya Mbali.
Ambacho nilidhani Mheshimiwa Naibu Waziri alitakiwa kukivalia njuga ni ubora wa bidhaa zilizoko sokoni si kuangalia nani anafanya biashara hiyo.
Hawa wachina ambao wako Kariakoo wanalipa
*Kodi ya Mapato
*Wanalipa Kodi ya Pango
*Wanatoa ajira kwa wazawa
*Wanaongeza chachu ya ushindani
wa kibiashara sokoni.
Hata tukisema tuwafukuze eti wananwanyima wazawa nafasi za kufanya biashara kwani mitaji yao watapewa hawa wazawa.
NINI KIFANYIKE
Kuna vitu viwili ambavyo mi naona Serikali kupitia Wizara husika wangefanya
1. Kuhakikisha Wazawa wanawezeshwa kiuchumi kuwa na nguvu katika dunia hii ya ushindani wa kibiashara. Vijana wengi ambao wananguvu za kufanya biashara hawana mitaji na hawajui wataipataje mitaji hii.
Kuna Program nyingi zimeanzishwa ambazo vijana wanaishia kusoma kwenye magazeti tuu. Mkukuta ambao ulipigiwa kelele sana watu wengi hawajui mpango huu unafanyaje kazi na upo kwa ajili ya nani.
Elimu ya Biashara, Uwezo wa Kijasiriamali, Moyo wa Kuthubutu na mitaji duni ndio kinachotushinda sisi na kutaka kuwafukuza hawa wachina mitaani leo.
2. Ubora wa Bidhaa
Kama nilivyosema hapo juu, Wizara ilitakiwa kuhakikisha Ubora wa Bidhaa zinazoingizwa nchini ili kufanya soko la bidhaa liwe na bidhaa ambazo zina ubora wa kimataifa. Kuna Bidhaa nyingi ambazo nchi nyingi hazikubaliki lakini kwetu zinamwagwa kama njugu, watu wanatafuta pesa kwa taabu matokeo yake vitu wanavyonunua vinakaa kwa muda mfupi havidumu na kuwarudisha kwenye umasikini.
Changamoto tuliyonayo si hawa wanaouza maua au viatu Kariakoo, ni watanzania waache uoga wa Kibiashara na kukubali ushindani hata wa kukaanga Chipsi na huo utakuwa ushindani wa maendeleo. Maamuzi kama haya ndio yanatufanya watanzania kuwa legelege. Leo mtakimbiza Wachina kesho mtaanza oooh na Wakenya wanaofanya biashara waondoke. Kwani maduka ya Kompyuta yaliyojaa mjini na kumilikiwa na Wahindi inamaana watanzania hawawezi kufanya biashara hizo?
Unamsaidiaje mtanzania mjasiriamali anapopambana kwenye Tender na makampuni ya kigeni?. Kuna maamuzi mengine ni ya kisiasa zaidi na Bahati mbaya tunayashabikia kisiasa lakini swali bado Nani atachukua nafasi ya hawa tunaowafukuza? nani atafaidika na kuondoka kwao?
Mdau wa Michuzi Blog
na Mwana Blogu pia.
Nawakilisha.
Binafsi nautazama huu uamuzi kwa pande ya pili na kuona kama si sawa.
Kipindi hichi ambapo uchumi wetu ni wa soko Huria Mteja ndio ana nafasi ya kuamua nini anunue, anunue kwa nani na bei gani.
Bado kuna challenge kubwa sana ya ubora na soko la bidhaa la Tanzania kutumika kama Jalala la bidhaa duni hasa toka mashariki ya Mbali.
Ambacho nilidhani Mheshimiwa Naibu Waziri alitakiwa kukivalia njuga ni ubora wa bidhaa zilizoko sokoni si kuangalia nani anafanya biashara hiyo.
Hawa wachina ambao wako Kariakoo wanalipa
*Kodi ya Mapato
*Wanalipa Kodi ya Pango
*Wanatoa ajira kwa wazawa
*Wanaongeza chachu ya ushindani
wa kibiashara sokoni.
Hata tukisema tuwafukuze eti wananwanyima wazawa nafasi za kufanya biashara kwani mitaji yao watapewa hawa wazawa.
NINI KIFANYIKE
Kuna vitu viwili ambavyo mi naona Serikali kupitia Wizara husika wangefanya
1. Kuhakikisha Wazawa wanawezeshwa kiuchumi kuwa na nguvu katika dunia hii ya ushindani wa kibiashara. Vijana wengi ambao wananguvu za kufanya biashara hawana mitaji na hawajui wataipataje mitaji hii.
Kuna Program nyingi zimeanzishwa ambazo vijana wanaishia kusoma kwenye magazeti tuu. Mkukuta ambao ulipigiwa kelele sana watu wengi hawajui mpango huu unafanyaje kazi na upo kwa ajili ya nani.
Elimu ya Biashara, Uwezo wa Kijasiriamali, Moyo wa Kuthubutu na mitaji duni ndio kinachotushinda sisi na kutaka kuwafukuza hawa wachina mitaani leo.
2. Ubora wa Bidhaa
Kama nilivyosema hapo juu, Wizara ilitakiwa kuhakikisha Ubora wa Bidhaa zinazoingizwa nchini ili kufanya soko la bidhaa liwe na bidhaa ambazo zina ubora wa kimataifa. Kuna Bidhaa nyingi ambazo nchi nyingi hazikubaliki lakini kwetu zinamwagwa kama njugu, watu wanatafuta pesa kwa taabu matokeo yake vitu wanavyonunua vinakaa kwa muda mfupi havidumu na kuwarudisha kwenye umasikini.
Changamoto tuliyonayo si hawa wanaouza maua au viatu Kariakoo, ni watanzania waache uoga wa Kibiashara na kukubali ushindani hata wa kukaanga Chipsi na huo utakuwa ushindani wa maendeleo. Maamuzi kama haya ndio yanatufanya watanzania kuwa legelege. Leo mtakimbiza Wachina kesho mtaanza oooh na Wakenya wanaofanya biashara waondoke. Kwani maduka ya Kompyuta yaliyojaa mjini na kumilikiwa na Wahindi inamaana watanzania hawawezi kufanya biashara hizo?
Unamsaidiaje mtanzania mjasiriamali anapopambana kwenye Tender na makampuni ya kigeni?. Kuna maamuzi mengine ni ya kisiasa zaidi na Bahati mbaya tunayashabikia kisiasa lakini swali bado Nani atachukua nafasi ya hawa tunaowafukuza? nani atafaidika na kuondoka kwao?
Mdau wa Michuzi Blog
na Mwana Blogu pia.
Nawakilisha.
Hawa ndio viongozi wasiotakiwa katika karne hii.
ReplyDeleteBadala ya kumsomesha mtanzania ashindane kwenye nyanja kama kujenga majengo makubwa na kutengeneza barabara et tunagombea kuuza viatu na maua kariakoo. huyo waziri ajiulize kwanini ma engineer wetu hawapewi kazi sio kwenda kariakoo kugombea kuuza karanga. hata watanzania wamejazana nchi za watu.
Kuwafukuza Wachina sio kuwalemaza mazawa kiu-jasiliamali, tatizo ni kuwa hawa Wachina waliopo Kariakoo walikuja sio kuuza maua, bali walikuja kama wawekezaji katika sekta ya viwanda, kilimo n.k Hivyo, basi hawa Wachina badala ya kushindana na Wahindi, akina Mengi, Dialo, Shirima, Dewji, na ajina Manji katika sekta ya viwanda vidogo, kati na juu, wao wameingia kushindana na kundi tofauti kabisa, mbaya zaidi wakiwa na mtaji mkubwa kuliko hawa wazawa na pia hati zao ukazi ni za wawekezaji na sio kupigwa vumbi Kariakoo. Hilo ndilo tatizo na kiini cha maamuzi ya waziri. Ikumbukwe kuwa sera ya mwekezaji wa kigeni ili aweze kupata hati ya kuishi ya uwekezaji ni lakima uonyesha kiasi cha dolla laki 300,000. Je, hawa ni wa kufanya biashara na wazawa waliokopa SACCOs, FINCA, PRIDE kiasi cha milioni 15? Ndio maana bei ya vyumba kariakoo imepanda kutoka 200,000 mwaka 2005 na sasa sio madafu tena bali ni dolla za kimarekani kuanzia 800 na kuendele. Je, wewe mswahili unanunua kwa dola??? Wachina wanaleta 'property bubble' tu kariakoo ambalo halimsaidii mtanzania wa kawaida.
ReplyDeleteWakenya na Waganda wakiingia kuuza Kariakoo sio tatizo iwapo tu watakuwa wamekuja kwa lengo hilo na leseni za ukazi zikionyesha hivyo, lakini ikiwa nao watakuwa na leseni nyingine tofauti na shughuli watakazo kuwa wanazifanya basi huo utaratibu ndio unaopaswa kuendelea kutumika, timua chinga wa kigeni wote.
swala hapa ni kwamba hicho wanachokifanya sicho kilichowaleta nchini. wew ulishawahi kuwa kwenye nchi za wengine uone wanavyofanya kama unafanya kile ambacho hakikupeleka huko inakuwa ilegal no matter unalipa tax au la isitoshe hata hiyo tax haitusaidii maana fedha zote zinaenda kwa mafisadi.
ReplyDeleteChina ni moja ya nchi tajiri sana duniani. Serikali yao inakalia zaidi ya dola trilioni moja katika benki yake. Sisi Tanzania tumesaidiwa na serikali ya China kujengewa uwanja wa kisasa wa mpira, treni, elimu ya juu katika vyuo vyao na kupewa misaada katika sekta za kijeshi na kadhalika. Kufukuzwa kwa Wachina sio tu itawakosesha kazi wazawa wengi, ila pia haitasaidia Wazawa kwa kuwa hawana uwezo mkumbwa wa kufanya baishara. Pia, nchi masikini kama yetu haina ubavu kugombana na rafiki mkubwa wetu kama China. Leo tunawafukuza, kesho tunataka kwenda kwao kuomba misaada na elimu au matibabu. Mheshimiwa Naibu Waziri kapata pointi za haraka za kisiasa lakini naona binafsi hajafikiria jinsi alivyofanya itaharibu uhusiano mzuri na China na nchi yetu inahitaji China kuliko.
ReplyDeleteSafi sana mtoa hoja. Tatizo watanzania wengi tunapenda shortcut! Tunapenda majibu marahisi kwa maswali magumu. Unaona waziri kaongea..hujiulizi mara mbili mbali maana halisia ya kauli zake. Leo tunasema wachina..kesho ni wakenya na keshokutwa ni nani Mungu anajua.
ReplyDeleteTuache uzalendo wa kijinga. Hatuna budi kuchapa kazi kama inavyotakiwa. Tatizo la Tanzania...watu wanaona kwamba kila serikali inachokifanya ni favour. Tuna safari ndefu sana ya kupambana na kujua wajibu wetu katika kushindana kwenye hili soko huria.
nimesikitishwa sana na hoja hii.
ReplyDelete1. uliyeituma huna nia mbaya ispokuwa huenda uelewa wako ukawa mdogo sio kosa lako.
mgeni popote duniani anapoenda ktk nchi ya kigeni huwa haruhusiwi kwenda kuwa mchuuzi(machinga)na kama hana mtaji akae kwao afanye uchuuzi wake.
kwa mfano ukiomba visa ya UK kama mfanya biashara wanamasharti yao wameweka ili wakuaamini kuwa wewe ni mfanya biashara lazima uwe na mtaji wa kuanzia £2000,000. isiwe chini ya hapo.
sasa basi hawa wa china machinga wameingiaje na wamewapa nini wizara ya uhamiaji mpaka wao wawe wachuuzi je mzawa nae atafanya nini
lazima mjuwe pia sheria za uhamiaji zinasema nini na ktk nchi za wengine pia ili msiigeuze nchi kuwa jarara.
Weweeeeeeeeeeee man u mwaka wetu huuuuuuuuu halo halo ya bwawaaaaa... maji kwisha kauka!!
ReplyDeletecompetetion ambayo unajuwa utashindwa ni kuwaruhusu hawa watu watutawale.
ReplyDeletewaarabu wahindi sasa wachina,
nendeni india, china,uarabuni, ulaya, marekani tata kwa majirani zetu uganda na kenya muone kama wageni wanakaribishwa.
hatuwataki hawa wachina ni waarifu wakubwa kama wasomali.
wachina waje na maviwanda ya kutengeneza magari, computer na sio umachinga sasa wale wananchi wetu wa HALI YA CHINI WATAFANYA NINI.
TANZANIA TUMESINZIA KWELI TUJIFUNZE KWA WENZETU WAKENYA UGANDA NA RWANDA.
TATIZO LIKO KWA SERIKALI WAKO TAYARI KUUZA NCHI ILIMRADI MAMBO YAO YATIMIZWE NA HAO WACHINA WEZI.
MTOA MAADA INAONEKANA HUJUI DUNIA YA LEO IKOJE.
TEMBELEA KENYA WEEK MBILI TU UONE JINSI UTAKAVYO JISIKIA MGENI NA KUNYANYASWA.
KWANINI TUWAKUMBATIE HAWA WATU AMBAO WANAKUJA KUTUTAWALA.
MIMI NASEMA HIVI, MH WAZIRI HAKUKOSEA HATA KIDOGO NA NAUNGANA MOJA KWA MOJA NA WALE WOTE WENYE UFAHAMU WA KUTOSHA KUWEZA KUTAMBUA KWAMBA LILILOFANYIKA NI SAHIHI.
ReplyDeleteTAZAMA GEREJI ZOTE ZA USWAHILINI NI ZA WACHINA SIKU HIZI.JE MAFUNDI WETU WANAOHITIMU KILA SIKU WAISHIE KUAJIRIWA NA MCHINA KWA KUTWA WALIPWE SH 3500??
WACHINA MOJA YA MIKAKATI YAO KWA SASA NI KUICHOTA AFRICA KABLA YA NCHI ZA MAGHARIBI.WAMEJAA KOTE HUKO ILA BONGO TU NDIO TUMEWAPISHA MPAKA VYUMBANI MWETU.
SI WATU WEMA HAWA. WANA ROHO MBAYA MNO. KWAO MTU MWEUSI HANA THAMANI.
MM NAWAFAHAMU SANA
BWANA MTOA HOJAINAONEKANA UELEWA WAKO NI ZIRO KANA TARATIBU NASHERIA ZA NCHI KWA WAGENI KUFANYA KAZI AU IWE BIASHARA,WAGENI WANAWATUMIA VIBARAKA WAZAWA KUPATA LESENI ZA KUFANYA UMACHINGA,KWA KUWA SHERIA ZA NCHI HAZIRUHUSU,NA SIO KWA TANZANIA TU NCHI ZOTE DUNIANI ZINATARATIBU ZAKE KAKA,UWEZI KUMPANDISHA ULINGONI MATUMLA NA TYSONI,TUKIRUHUSU WAGENI WAFANYE BIASHARA HOLELA UNAYAJUA MADHARA YAKE?KAMA UNAMUDA WA KUTUNDIKIA HOJA KAMA HIZI TUMIA MUDA HUO KUCHAMBUA ON LINE HOJA USIKA SHERIA ZAKE KISHA ANGALIA NA NCHI ZILIZO ENDELEA SHERIA ZAO ZINA SEMAJE,NA NDUGU MICHUZI KUNA HOJA ZINGINE SIO LAZIMA UTULETEE HUYU MTANA WAJADI ANAJIPIGIA NGOMA KUTUPAGIA SHERIA.HEBU NENDA CHINA,JAPANI,USA PANGA VINYAGO KIOLELA SKONI UNE MOTO WAKE.
ReplyDeleteHivi mdau uliyeandika hii hoja uko Bongo au Mtoni? maana una mapointi ya kufa mtu. Lazima waswahili tuelewe kuwa wakati tunatafuta solution ya issue kompliketedi sio kuwa na jazba la sivyo hatutasolvu chochote. Kawa wageni wanakiuka masharti ya vibali vyao, basi hilo liwe addressed but kuna mtu kala rushwa kutoa vibali kiholela na usikute hajafungwa bado!! Lakini picha ya maelfu ya Wachina wanapanda ndege wamefukuzwa Tanzania inanikumbusha sana Uganda ilivyotimua Waasia na kwa masuala ya PR it would be a disaster!!Wanasiasa bwana ni kama kinadada poa mradi waonekane wanafanya kazi hata kama kesho madhara ni makubwa. Sasa leo unawafukuza Wachina kesho wanafuta skolashipu za vijana wetu, nani kaluzi? Vichwa kama vya huyu mshikaji aliyejenga hoja hii tunavihitaji sana Bongo... Asante kaka kwa kuwa na vision swali ni je, utasikilizwa?
ReplyDeleteMdau Akilimali wa Mtoni tena Kijichi.
ndugu mtoa maoni inaonekana umeajiriwa na wachina kufatana utafiti wangu na shule hujaenda kabisaaaaaaaaaa kama umenda basi umehudhuria tu na kushindikiza wenzako kwa mtu mwenye busara na elimu ambayo ndio mwanga mkubwa asingeweza kutoa wazo kama hilo sisi tupo nje ya nchi nani anatuthamini huku mpaka tupewe sehemu ya kufanya biashara ndogondogo kama wanazo fanya wachina huko kwao?mimi nimesoma china digree ya kwanza hao watu ni wabaguzi na wababaishaji hela yote wanayoipata hapo nyumbani inaingia ktk serikali ya china wachina sio wajinga kutapakaa afrika nzima bila manufaa ya nchi yao acha ukichaa ww kama wamekuajiri basi huo ndio mwisho wa ajira yako
ReplyDeleteKuna maana sana kama wazawa watafanya wenyewe hizi biashara,kuanzia za umachinga hadi za tenda kwenye ofisi na miradi ya serikali,kwa hali hii ndio tutapata maendeleo ya kweli,msingi wa kuitaji hali hii ni kuhakikisha mzunguko wa fedha ambao ndio uchumi wenyewe unabaki miongoni mwetu na sii kama sasa watu wanakuja kufanya uchuuzi na kuondoka na pesa zote na wala hawawekezi kitu cha msingi.Wazawa wakipata nguvu za kiuchumi wataweza kuleta maendeleo kuanzia ngazi ya familia mpaka taifa.Mfano mzuri angalia wakinga wa kariakoo wameweza kuwekeza kwenye majengo na wameweza leo hii kuwasomesha watoto wao kwenye shule nzuri....tuna walilia wachina bila ya kuelewa adhari kubwa wanyotuletea kiuchumi kuanzia kwenye bidhaa zao zenye ubora mdogo mpaka kuuminya mzunguko wetu wa kiuchumi.Tusione aibu tuige wenzetu wa Botswana,Ghana na hata jirani zetu Rwanda ambao wanazingatia haswa wazawa kushika nguvu za kiuchumi,sio zambi kuwajali wazawa ,hawa hawana nchi nyingine zaidi ya hii....wapi kwao?Nenda kwa hao wachina na mataifa mengine uone ni jinsi gani ilivyokuwa ni kazi sana mgeni kufanya biashara,.
ReplyDeleteTUAMKE IANZE KWENYE UMACHINGA MPAKA KWENYE TENDA...UPENDELEO NI LAZIMA NA MUHIMU KWA AJILI YA KUTULINDA SISI WENYEWE.NCHI YETU NI TAJIRI SANA WENYE NCHI NIMASIKINI SANA,ILA WAGENI NDIO WANAOFAIDI MALIASILI ZETU.
Naibu waziri hajasema kwamba anawafukuza ila amewataka wafuate kanuni na taratibu zilizopo mjomba!!we kama Mtanzania lazima uwe tofauti na mwekezaji!!
ReplyDeleteTembea kwenye nchi zao ndo utaona kweli naibu ana nia nzuri maana naona una mpinga!!huku UK kupata visa tu ni issue.We unataka hao wachina wako watajirike afu wewe usifaidi hata mapato yao?
Kuna watu wengi wapuuzi hapa tanzania wanapewa ela na hao wageni hili watoe maoni yao ya kijinga. Tanzania ni nchi kama nchi nyingine, mgeni yeyote lazima afanye kilichomleta au mpleka katika nchi aliyoenda. Swala la wageni kuja tanzania na kufanya shughuli tofauti na visa zao ni kosa kubwa. Nampongeza waziri, maoni yote yanayowatetea hawa wageni yanatolewa na hao wageni ili kuvuruga sheria za nchi yetu.
ReplyDeleteHI KAKA MITHUPU,
ReplyDeleteNAONA HUU MJADALA UMEKUWA MKALI MNO, ILA NAMI NINAMACHACHE YA KUCHANGI. HV SISI WASWAHILI TUNA UHAKIKA GANI KAMA WACHINA WOTE WALIOPALE KARIAKOO WALIINGIA NCHINI KAMA WAWEKEZAJI?, AU NDIOI MAMBO YA UOGA WA USHINDANI. UNAJUA SISI WASWAHILI NI WAVIVU SANA NA MALA ZOTE HUWA TUNAPENDA TUPATE PESA BILA YA KUIFANYIA KAZI, EITHER TUIPATE KWA RUSHWA, KUIBA AU MAMBO YA KIJINGA KIJINGA TU, ALAFU TWENDE BAR TUKANYWE BIA AU TWENDE KWENYE BENDI ETI TUKAJIDAI MAPEDEJEE, TUWE TUNAGAWA PESA BURE UKU TUNASISIFIWA ETI TUNAPESA NYINGI SANA LKN UKIULIZA BIASHARA TUNAZOFANYA ILI TUPATE PESA HIZO TUNAZOGAWA OVYO HATA HAZIJULIKANI. SASA KAMA WEWE NI MFANYABIASHARA MAKINI NA MCHAPAKAZI MCHINI PALE KARIAKOO AU ALIYEFUNGUA GARAGE SINZA WEWE ANAKUZUIA NINI KAMA NI KWELI WEWE NI MCHAPAKAZI, KWAKUWA KAMA KWELI WEWE GAREJI YAKO INATOA HUDUMA BORA SISI TUTALETA TU MAGARI YETU, LKN KAMA GAREJI YAKO INACHAKAHUA NI BORA TUKALIPE BEI KUBWA KWA WACHINA KAMA TUFANYAVYO SASA KULIKO KUMPELEKEA GARI FUNDI MWIZI ALAFU AANZE KUNIBADILISHIA ENGINE.
WAZIRI PALE KACHEMKA, HAKUTAKIWA KULICHUKULIA SUHALA ILI KISIASA NA KUKURUPUKA ALIPASWA KUFUATILIA KWA KINA KISHA KU ACT KAMA NI KWELI JAMAA WAKO NCHINI KINYUME CHA SHERIA NA WANAFANYA KAZI KINYUME CHA SHERIA PIA.
JAMANI WASWAHILI TUACHE UVIVU TUPIGE PESA, MBONA SISI WENGINE TUNAPIGA PESA NA TUNA MAISHA MAZURI NDANI YA NCHI HII HII AMBAYO NYIE MSIOFANYA KAZI MNAISHIA KULALAMIKA TU.
MUDDY NICE
Yaani hata mimi nashangaa hawa viongozi wetu sidhani kama wanafanya utafiti kabla ya kutoa maamuzi,hivi jamani angalieni bidhaa zetu zilivyokuwa kabla ya hawa wageni na zilivyo sasa hivi baada ya hawa wageni kuingia, kwa kweli at some point zimekuwa improved kidogo na hii ni kwasababu ya competition iliyokuwepo kwenye market na wageni wameleta ujuzi hapa kwetu na hata creativity pia imeongozeka kidogo,kwa hiyo soulution sio kuwafukuza kama issue ni kuwa hazijasajiliwa basi wazisajili ili wawe wanalipa kodi na Tanzania iweze kupata revenue. Hivi hao wahusika hawaoni kama kuwafukuzani ni kupotezea serikali pato? Lakini nafikiri hizi wizara husika huwa hazishirikiani especially wizara ya fedha na uchumi ambayo inahusika katika kukusanya kodi, wizara ya viwanda na masoko ambayo kwa mtazamo wangu naona inajaribu kulinda viwanda vya ndani hatupingi kuvilinda ili viweze kukua lakini juhudi zinazofanywa na wizara hii ili kuviwezesha viwanda hivi viwe competitive na bidhaa za viwanda hivi ziweze kuuzika katika masoko ya ndani na kimataifa bado haziridhishi kwani ukiangalia hata hiyo mikopo na mambo mengine kama hayo yanakwenda kwa watu wenye makampuni makubwa au wafanya biashara wakubwa tu na sio wale wauza bidhaa ndogo ndogo kule sokoni kariakoo na pia wizara ya mambo ya nje na wizara ya mambo ya ndani ziko wapi kwani kuna sheria ambazo mtu anapoingia ndani ya nchi fulani anapewa permission ya kufanya kazi, kufanya biashara na shughuli zozote hapa nchini kuna sheria zipo mtu gani anaruhusiwa kufanya nini, hizi wizara zote zinatakiwa zishirikiane katika kujadili issues na kutoa maamuzi ambayo yanakuwa yana maana kwa nchi yetu.
ReplyDeleteNimefurahishwa na maoni ya mdau hapo juu. Lakini lazima wananchi tuelewe kuwa tuna makubaliano ya ujirani sijui kitu gani unaweza kuelezea kuhusu sisi na wachina.kwamba tuna ile kitu free movemnet ya maingiliano,so vikwazo vya uhamiajiu baina ya nchi zetu (tanzania na china) vimepunguzwa,hivyo mchina anakuja bongo kama mtu wa sumbawanga tu akiamua kupanda basi aje ndo inakuwa hivyo,hiyo ya kusema eti wanakuja kama wawekezaji wa viwanda,nani kasema? Hiyo ni politics tuuu,kwani si lazima mtu aoneshe mtaji wa hicho anachoenda fanya,au unapewa tu kibali cha kuishi kwa kusema eti naenda kufanya kazi fulani? Sitaki kuamini hilo.
ReplyDelete