WWW.TUNES100.COM ni website kwa ajili ya Wasanii (Wanamuziki) na watu wanaopenda Muziki Tanzania.

Tunes100.com inawezesha wasanii wa Tanzania kusambaza na kutangaza nyimbo,albamu na vilevile videos kwa watu wengi wanaopenda Muziki.

Wanamuziki wanaweza kupromote nyimbo zao na watu wanaweza kupata nyimbo zao.

Tunes100.com ipo kwenye simu yako kama unapata huduma ya internet kwenye simu.

Unaweza kupata nyimbo poa BURE kutoka Tanzania au Marekani kwa kutumia simu yako.

Website ina lugha ya Kiswahili vilevile. Bonyeza bendera ya Tanzania kwenye website kubadilisha lugha kuwa kiswahili.

Wasanii wanaweza -

  1. Kuweka (Upload) albums,nyimbo na picha ili watu wote wazipate Tanzania mpaka Ulaya

  2. Dj's wanaweza kuweka (Upload) mixtapes zao na kujitangaza.

  3. Wasanii wanaweza kushindana na kupata downloads reports.

  4. Watu wanaweza kuingia na kupata music downloads latest kutoka Marekani (Chris Brown, Gucci, Rick Ross and more)

  5. Tunes100.com kuna Taarabu mpaka Bongo Flava kwahiyo tunaomba wasanii na wanamuziki wote Tanzania watumie website hii kuonyesha miziki yao.

  6. Wanamuziki wanaweza kuuza au kutoa bure (Promotion songs) ili wapenda muziki wajue miziki yao.

  7. Wanafilamu wanaweza kuweka filamu na videos pia.

  8. Watu wote watapata muziki na vilevile kuweza kutoa maoni kuhusu nyimbo za wasanii hao.

Malengo ya www.tunes100.com ni kuwezesha wanamuziki wa Tanzania,Kenya na Uganda kutangaza nyimbo zao na vilevile kupata pesa moja kwa moja (Direct) kutoka kwenye Muziki yao bila kutumia gharama za kutengeneza cd au kuuza haki za miziki kwa makampuni au mdhamini.

WWW.TUNES100.COM haimiliki na haichukui Haki au Copyrights za Muziki au albums. Wasanii ndio wanamiliki na sisi ni wasambazaji tu.

Kwa wanamuziki wanaotaka kuongea zaidi kuhusu malipo au kitu chochote, naomba watume email juliustemu@gmail.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. wanaziki wanahitaji faida ktk kazi zao unapoweka mp3 mtandaoni,
    basi lazima msikilizaji atakae download alipe japo vijisenti,
    lakini kwa mradi na mtaji huu,wasanii msikubali kuweka mtandaoni nyimbo zenu bure ...kwa kuambiwa ni poromotion.
    tumeona tovoti moja www.rusumo.com imeweka nyimbo za wasanii bila ya ridhaa yao wenyewe

    ReplyDelete
  2. kwa mwanzo si mbaya keweka buer kwa kuwavutia members baadae ikipata member wengi nadhani ndio muda muhafaka kuweka kwa pesa

    ReplyDelete
  3. HATA KWENYE RADIO HAPO TANZANIA HATULIPWI.
    Yaani kuna wivu wakuua mtu kwa mdau wa kwanza. Nafikiri kwenye huu mtandao wasanii wanalipwa. Ukisoma kuna email kuhusu mambo ya malipo.
    Marekani, Ulaya na sehemu nyingi wasanii wanatoa nyimbo nyingi sana za promotion na ni bure kabisa. Nafikiri kuna wasanii wengi tanzania hawapati nafasi radioni kabisa. Mtandao kama huu lazima uwepo kutusaidia.. MIMI NI MSANII HAPA TANZANIA NA NIMEWEKA NYIMBO ZANGU KWENYE HUU MTANDAO.
    INASIKITISHA WASANII WENGI HAWAJULIKANI TANZANIA. NYIMBO ZAO ZINAPIGWA RADIONI LAKINI WAO MASIKINI NA HAWAJULIKANI HATA KWA PICHA. MIMI KAMA MSANII NASEMA NI ANGALAU NIJULIKANE NA VILEVILE WATU WAJUA ALBUM YANGU.
    Naweza kutoa album nyingi kama msanii.. Hii nafanya kila siku.

    SIO KILA MSANII NI ALI KIBA AU LADY JAY DEE.

    Kwa sasa hakuna mtandao wowote kwa wasanii tanzania na haswa wa kiswahili. Kwahiyo mimi nasema hii maendeleo..

    Mimi ni msanii mkubwa tanzania na najulikana sana.. NA KWENYE RADIO HATULIPWI KABISA
    NIKIUZA ALBUM YANGU KWA MUHINDI NI HELA NDOGO SANA. KWAHIYO NAFIKIRI NI VIZURI NI NIWEKE NYIMBO NA NIFANYE SHOO. COPYRIGHTS NAMILIKI MWENYEWE.. POA KABISA.

    ReplyDelete
  4. Mimi ni msanii hapa Dar. yaani hii website ndio tunahitaji. Jamani wahindi wamekuwa wanatunyanyasa sana kwenye fani zetu. Hakuna anaetuangalia. Kuna wakati niliuza album yangu zima kwa milion 3. Na hiyo inajumuisha hati na kila kitu. Wakati mwingine wanachukua albumu zetu halafu wanasema watalipa lakini hawalipi. Kwenye mtandao huu naweza kuweka demo tu. Kwahiyo kuna nyimbo nitaweka samples alafu nitaweka link ya website yangu ili watu waende kununua.

    ReplyDelete
  5. Mimi naona huu mtandao ni poa sana. Kwanza kuna siri yake nimegundua. Sisi ndio tunafungua profile kama wasanii. Ushauri wangu ni hivi.. Ukiandia profile information yako.. weka pia maduka ambayo watu wanaweza kununua cd yako. Vilevile tumia mtandao kupima nyimbo zako. watu watakupa maoni na utajua kweli hii ni nyimbo kali au no.
    Ushauri wangu wa mwisho.. weka namba yako ya simu na email ili watu wa show waweza kukupigia direct. Kwakweli hii ni mara ya kwanza mtandao kama huu ambao ni wa kiswahili na ni sisi wasanii tunakontrol..

    Mimi ni msanii maarufu sana tanzania.. mpaka ulaya..
    Unanijua tayari. Naimba na ninatunga karibia nyimbo 5 au 6 kwa siku.
    Wapi nitapima kama sio hapa.
    Uzuri wake naweza kuweka na kutoa wakati wowote. Haki na mmiliki mimi.
    Mtu wa kigoma , mwanza au iringa anaweza kunipa maoni sasa hivi.
    AK

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...