Mama Christina Innocent , jina la Usanii ni Mama Bishanga (kushoto) na kulia ni mwanae Hendrick Nambira, jina la Usanii Kenny akizungumza na Waandishi wa Habari ambao hawapo kwenye picha na kutoa ushauri kwa Wasanii wa Tanzania jinsi Filamu zinavyoendeshwa nchi nyingine,na kuwapongeza jinsi Watanzania walivyoendelea kwenye majukwa ya usanii, kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam leo. Picha na Anna Itenda -Maelezo.

Mama Bishanga ameongelea
mambo makuu matatu:


1. Umuhimu wa wasanii wa filamu na watendaji (wapiga picha, waongozaji, watu wa taa nk.) wafanye juu chini wasomee fani hiyo badala ya kutegemea uzoefu tu kwani bila weledi fani hio itadoda. Ameitaka serikali itoe kipaumbele mafunzo ya sanaa ya filamu kama zilivyo fani zinginezo.

2. Amesisitiza umuhimu wa uhalisia ambao unakosekana sana katika filamu za Tanzania kiasi nyingi zionaonekena kama maigizo yasiyo na mvuto. Amesisitiza umuhimu wa kuheshimu maadili ya nchi na kukataza kabisa waigizaji kucheza michezo ya ngono nje nje kwani hio si utamaduni wa mtanzania. Kuhusu filamu ya 'Shoga' inayozi9nduliwa wiki hii amesema ushoga si desturi ya Kitanzania na bila shaka filamu itapendwa kwani inatoa tahadhari ya tabia hio chafu. Ila amesema si vyema watu wakambeza mchezaji mkuu wa filamu hio kwa kudhani yeye ni shoga kweli, na kwamba huo sio ustaarabu kwani hata yeye aliwahi kusemwa mitaani na wenye uelewa mdogo kuwa ni mama mkatili baada ya kucheza kama mama mkwe mkatili.

3. Amewataka wasanii na wadau wa tasnia ya filamu kuendeleza libeneke kwani kazi zao zinaonekana na kuheshimika sana na kwamba wakiongezea weledi wa kwenda shule hakuna wa kuwagusa. Alimfagilia sana JK kwa kujituma kuendeleza michezo na sanaa, na kusema wasanii na wanamichezo wamuenzi Rais wetu kwa kujituma na kufanya vyema


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Mama Bishanga ushauri wako ni mzuri hata mimi nasapoti sana maoni yako,cha kuongezea tu ni swala la hawa wasanii,wapiga picha,mafundi nk.kujitahidi kuweza kijiendeleza kwa masomo yahusuyo fani hii ili kuweza kufikia angalau level ya juu na hata kimataifa.Tunaona ktk magazeti yetu kila kukicha habari za wasanii wetu ambazo siyo nzuri,yaani kila siku wako kwenye vilabu,ni ulevi,kupigana,ngono nk.nadhani hata muda wa kutulia na kujisomea au kujifunza zaidi hawana.Unaweza kumsoma msanii kwa wiki anahusika ktk kashfa nyingi na siku zote ni "Mango garden,Billicanas,Sigara club,leaders club nk.nadhani maisha yao yanakuwa humo humo vilabuni na kashfa tele,Mimi kama mpenzi wa filamu zetu za bongo nashauri hawa wasanii wajirekebishe na watumie muda wao kwa kujiendeleza ili wajenge heshama zaidi ktk tasnia hii ya filam.ni ushauri wa bure.
    mtoa maoni Washington Dc,Usa.

    ReplyDelete
  2. Kumbe mama Bishanga anaishi Marekani siku hizi. Woow ndio maana alipotea. Sasa inabidi aungane na Chemi Chemponda watoe filamu hukohuko majuu!

    ReplyDelete
  3. Hapo umenena mama filamu za Tanzania ni kama maigizo ya shule za msingi kuanzia mwanzo hadi mwisho watu wako sebuleni na chumbani tu!

    ReplyDelete
  4. Mama Bishanga umetoa ushauri mzuri sana. Natumaini wasanii waTanzania watakusikia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...