NA JONATHAN TITO
MSHINDI wa dunia taji la Miss Progress International Julieth William, leo ametembelea watu wenye ulemavu wa ngozi Mkoani Shinyanga.
Julieth alitembelea watu hao na watoto wenye ulemavu huo wa ngozi kwa lengo la kutaka kufahamu mahitaji yao kabla ya kuweza kuwasaidia.
Ziara hiyo iliyoandaliwa na kampuni ya One Touch Solutions inayoandaa shindano la Miss Progress Tanzania ilimedhaminiwa na Precision Air na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
Mlimbwende huyo aliyetwaa taji hilo mwaka jana nchini Italia alianza kwa kutembelea shule ya Buhangija, ambayo inatunza watoto wenye ulemavu huo.
Akiwa katika shule hiyo alipata fursa ya kutanzama mazingira ya shule hiyo pamoja na kuzungumza na watoto hao kwa muda wa dakika 30.
Katika moja ya mahitaji waliyotaka watoto hao ni kumaliziwa kwa moja ya bweni lao ambalo halijamalizika ili kuweza kupata nafasi nzuri ya kulala kutokana na lile wanalotumia kuwa dogo, jambo linalowafanya walale kitanda kimoja watu watatu.
Baadaye alitembelea ofisi za mkoa za Chama cha Maalbino (TAS) na kuweza kuzungumza na watu wazima ili nao kutaja mahitaji yao.
Katika kikao hicho watu hao wenye ulemavu walitaja mahitaji yao ikiwaa ni pamoja na kutaka kupewa elimu ya ujasiliamali ili waweze kuendesha maisha yao na kuondokana na utegemezi.
Pia alikutana na Ofisa Elimu wa mkoa wa Shinyanga, Eva Lopa, Ofisa Ustawi wa Jamii, Jesca Kagunila. Leo Julieth atakuwa mkoani Mwanza kabla kuelekea Arusha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...