
Mimi ni mdau wa mkubwa wa Globu ya Jamii najulikana kama Florian Malunde wa hapa Makumbusho DSM. Naomba kuwasilisha picha hii ili wadau wenye data watupe msaada tutani wa kupata majina ya wachezaji hawa wa zamani wa timu ya Pamba 'TP Lindanda' iliyokuwa gumzo mwishoni mwa miaka ya 80. Mie hapo namkumbuka wa kwanza kulia waliosimama ni kipa Paul Rwechungula.
Wasalaam
Florian
Wasalaam
Florian
Ninaowakumbuka (tafadhali nisahihishe kama nimekosea):
ReplyDeleteWatatu kutoka kulia waliosimama ni Fumo Felician, watano kutoka kulia waliosimama ni Nteze John, wa kwanza waliokaa kulia ni Nico Bambaga (R.I.P).
Nico Bambaga kashafariki? Rest in eternal peace
ReplyDeleteWakiosimama: Wanne toka shoto ni Nteze John, akifuatiwa na Kitwana Selemani,Fumo Felician, na mwisho ni kipa Rwechungura
ReplyDeleteWaliokaa: Shoto ni Beya Simba, Halfan Ngassa, Ally Bushiri, watano ni Maonwa Mkami na wa mwisho ni Nico Bambaga.
Wengine siwakumbuki.
Waliosimama kulia ni rwechungura, pascal mayala, fumo felician, kitwana seleman, nteze john lungu, namba 13 nimemsahau,namba 2 nimemsahau,madata libigisa. Waliokaa kulia Marehemu nico bambaga, juma amiri, wa tano kwa waliokaa ni Alfonce modest, wa saba waliokaa kutoka kulia ni Marehemu dan mhoja na George gole. Nadhani nitakuwa nimekusaidia kiasi fulani. kweli wakati huo pamba ilikuwa inatisha
ReplyDeleteMadata Lubigisa. Msoma Rajab,Beya Simba, Beya simba, Nteze John, Kitwana Suleiman,Paschal Mayala, Rwechungura Paul,George Gole, halfan Ngassa, Ali Bushiri,Alphonse Modest, Maonwa Mkami, Thabeet, Juma Jurgen, na Marehemu Nico Bambaga
ReplyDeleteWaliosimama toka kushoto ni Madata Lubigisa, Rajab Msoma, Beya simba, Nteze John, Kitwana Suleiman,Fumo Felician, Pascal Mayala,Paul Rwechungura.
ReplyDeleteWaliokaa toka kushoto, George Gole,Khalfan Ngassa,Ali Bushiri,alphonse modest, Maonwa Mkami, Thabit, Juma Amir, na Marehemu Nico Bambaga(RIP). Tupwisa mazembe Lindanda, wana wa kawekamo
Mnatutia UCHUNGU SANA Kwa kuweka picha za dhahabu hizi za Mpira. Nahisi hakuna kizazi au Viongozi wakutoa dhahabu hizi tena.
ReplyDeleteHakika Pamba ya wakati ule ilikuwa bonge ya timu. Nakumbuka sikuwahi kuiona live lakini alipokuwa anatangaza mpira yule mtangazaji Chilambo Dominic, ilikuwa kama unawaona live. Mtangazaji yule (nafikiri ni R.I.P)alikuwa ananogesha sana wana TP Lindanda, alikuwa kama mchezaji wao wa 12. It was a great entertainment kumsikiliza Pamba wakiwa wanacheza.
ReplyDeleteRIP Rajab Msoma (no 2)
ReplyDeleteEnzi za mpira hizo sio za hashuo na kujinesha kwa wanawake mitaani na kusuka nywele. Wapi mpira Tanzania? Enzi hizo ilikuwa Pamba pamba ya Mwanza, Simba na Yanga zilikuwa ulimi puani hapa lakini wapi? A msitukumbushe kilio matangani.
ReplyDeleteAliyekaa mbele ya Kitwana(15) ni David Mwakalebela.
ReplyDeleteNa hapa walikuwa bado hawajawapata akina Hussein Aman Marsha na George Masatu.
Nimekulia Mwanza na ilikuwa raha tupu kwenda CCM Kirumba kuwaangalia wana TP Lindanda.
Soka enzi hizo ilikuwa tamu. Ndio, Simba na Yanga zilikuwa majina makubwa lakini sio kama sasa. Kulikuwa na timu kama Pilsner(au Plisna),Sigara bila kuwasahau Mecco ya Mbeya(waliwazushia wanatumia madawa ya kuongeza nguvu).
hii ndio Tout Pouissant lindanda wana kawekamo
ReplyDeleteKULIA NI GOAL KEEPER PAUL RWECHUNGURA.
ReplyDeleteHUYU ANAPATIKANA FACEBOOK FULL TIME ONLINE.
These were the moments of best parformance in Tanzanian soccer, Simba na yanga zilikuwa zinasalim amri kwa hawa wana tout pouisssant mazembe lindanda. Kwa mbali nasikia kumbukumbu zikinijia kichwani. Na sasa tunawapeleka kiwanja cha CCM kirummba mwanza kusikia mambo yanaendeleaje huko " Dominic Chilambo" (RIP) tupe mambo huko, eee eeeh hayawi hayawi yamekuwa pamba wanapata bao la pili yanga bila, alikuwa ni FF fumo Felician baada ya kupata pasi maridadi toka kwa maonwa Mkami ball dancer akamwangalia kipa wa yanga amekaa vipi na kumpeleka upande wa pili wa goli, " Pamba mbili yanga bila na hizo kelele unazozisikia ni mshangiliaji mahiri wa pamba Bwana Mang'ombe akiendesha baiskeli kwa style yake kuuuzunguka huu uwanja wa Ccm... ni hoi hoi , cheleko cheleko ndelemo ndlemo na vifijo, na kurudisha huko Pugu road ili uweze kuendelea na matangazo ya kawaida. Hapa waswahili husema mbwa alikuwa anakula karanga, maana kila team ilikuwa ikikanyaga CCM kirumba imeumia
ReplyDeleteHivi Tanzania mpaka leo hatujawapata kina Nteze John,Fumo Felician na Mohamed Hussein wapya
ReplyDeleteToka kushoto waliosimama Madata Lubigisa, Rajab Msoma, Beya Simba, Nteze John, Kitwana Selemani, Fumo Felician,Pascal Mayala, Paul Rwechungura.
ReplyDeleteWaliokaa kitako toka shoto George Gole, Khalfani Ngassa, Ally Bushiri, Alphonce Modest, Mao Mkami, Thabit, Juma Amiri Maftah na Nico Bambaga. Kwa watu wa mpira (soka) Michuzi umetukumbusha mbali saana enzi ya vipaji vya ukweli katika soka letu, leo hii timu ya taifa tunamtegemea Jerry Tegete, Machupa na Mrisho Ngassa!!! enzi hizo hata huyo Kitwana na Fumo Felician wanasubiri kwanza Innocent Haule na Kina Zamoyoni Mogella waumie ndio watie mguu Timu ya Taifa!! Eeeh Mwenyezi Mungu tunakuomba uturejeshee vipaji vingine kama hivi ili mioyo yetu isiendelee kusonononeka kwa vipigo vya 5 - 1! ahsante ndimi mdau shark_ham@yahoo.co.uk
Anonymous Tue Jan 18, 02:12:00 PM 2011 umeua mwana. Hahaha! Dominic Chilambo umempatia yaani kama ulimrekodi! Asante sana kwa kumbukumbu. Nakumbuka enzi hizo wenye kipato kidogo tulikuwa tunaweka betri juani, jioni zinawekwa kwenye redio, tunapand gola (mlima wa kitangiri) kuangalia mpira. Watu wote tunamzunguka mtu yoyote mwenye redio ili tumsikie Dominic maanake kule juu bila binoculars..mmmh, hujui nani kafunga goli.
ReplyDeletenawashukuru sana wadau walionielekeza kumpata mzee Mohamed Ibun Saleh. Nimefanikiwa kumpata.
ReplyDelete