Ndugu Michuzi, kupitia mtandao huu wa jamii napenda kuwajulisha wanajumuia wote wa hapa DALLAS-TEXAS na sehemu zingine juu ya kifo cha mzee EDWARD KIMBE SAILALE ambaye ni baba mzazi wa ndugu NICHOLUS SAILALE ambae tunaishi naye hapa Dallas.
Kifo cha mzee Sailale kimetokea huko nyumbani Arusha baada ya kusumbuliwa na tatizo la moyo. Ili kufanikisha gharama za shuguli nzima ya mazishi tunaomba ushirkiano wa watanzania na marafiki popote pale walipo. Imefunguliwa account maalumu katika Benki ya Wells Fargo kwa ajili ya ukusanyaji wa michango.
Kifo cha mzee Sailale kimetokea huko nyumbani Arusha baada ya kusumbuliwa na tatizo la moyo. Ili kufanikisha gharama za shuguli nzima ya mazishi tunaomba ushirkiano wa watanzania na marafiki popote pale walipo. Imefunguliwa account maalumu katika Benki ya Wells Fargo kwa ajili ya ukusanyaji wa michango.
Jina la account:
Nicholaus S. Chove
Account #: 9687778754
Kesho kutakuwepo na ibada maalumu (MEMORIAL SERVICE) katika kanisa la Umoja -Dallas (Meeting at King of Glory Lutheran Church)
Anwani: 6411 LBJ Freeway, Dallas TX 75240
Mawasiliano kwa simu: 214 554 7381, 817 875 4764, 469 279 1762
Kuwafariji wafiwa:
Mr.Nicholaus (Cell) 682-552 6402
Mrs Nicholaus (Cell) 682-203 2850
Pastor Absalom Nasua
-Umoja Church
-Umoja Church
Poleni wafiwa.
ReplyDeletepoleni sana wafiwa kwa kuondokewa na baba Mungu amlaze mahali pema.
ReplyDeleteNajua ni wakati wamajonzi ila sioni sababu ya kufungua account ya kufanikisha mazishi wakati msiba upo nyumbani sidhani kama unahitaji gharama kubwa kiasi hiki kama ni nauli ya mwanae kwenda tanzania na matumizi madogomadogo hata marafiki wa karibu wanaweza kutatua hili.
Mi nafikiri wa walio nje ya nje isiwe kama fashion kuchangishha fedha bila kuangalia uzito maana kuna vifo viwili ambavyo vimetokea huko wanahitaji kuleta miili Tanzania hiyo ni gharama kubwa wangepewa kipaumbele hao kuliko kuchangisha kwa mtu ambaye tayari yupo Tanzania.
Maana hata tuliopo huku sasa tukifiwa tutatoa matangazo ya kuomba michango
Ni mawazo yangu tu
Pole sana ndugu mfiwa. Watu tunaokufahamu tutakuja kukuona na kukufariji.
ReplyDeleteIla sasa tunaelekea pabaya Watanzania. Mi pia nipo hapa Dallas na nakubaliana kabisa na maoni ya mtu hapo juu. Kweli kuna sababu ya kuchangisha pesa toka kwenye General public kwa ajili ya mazishi nyumbani? Kufiwa kusigeuzwe miradi. Hii inatutia aibu wote tulio hapa Marekani!!
Ni sawa kabisa watoa maoni hapo juu, kwani tusipoangalia hata watu wanaofia nje watashindwa kuridishwa nyumbani kama ndio huko tunaelekea.
ReplyDeletekufiwa siku hizi imeshakuwa dili yaani msiba upo tz mchango unaombwa dallas...hii kiboko
ReplyDeleteYaani ukitoa maoni sasa ndo yanaitika moja kwa moja?? Testing, testing
ReplyDeleteNATOA POLE ZANGU NYINGI KWA WAFIWA, MUNGU AWAJAZE NEEMA ZAKE, AWAFARIJI NA KUWATIA NGUVU KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU CHA KUONDOKEWA NA MPENDWA WENU MZEE NICHOLOUS SAILALE
ReplyDeleteLakini kama wachangia mada waliopita bado siafiki kuchangisha kwa hili. Mie nipo Dar es Salaam tofauti na wachangiaji wa mwanzo lakini bado naona kuchangisha watanzania wa USA kwa mtu aliefia Bongo ni kuumizana. Jamani nafasi ya kuchangishana iachwe kwa wale watakaofia huko na ama kuhitaji safirishwa kuja Bongo or kuzikwa huko. Kwa waliofia Bongo, watu watoe wakijisikia na siyo kuitisha michango. Maisha ni magumu ndugu zanguni, nipo Bongo lakini nafahamu sana jinsi gani mlio ugaibuni mnahenyea hizo ndururu za huko.
Kwa mwendo huu itafika mahali watu watachoka na kujitolea kutakuwa kugumu sana. Waambieni watu waende mpa pole na company mfiwa wakati akijiandaa kuja mzika mzee inatosha.
Poleni sana wafiwa,
ReplyDeleteIla sasa "Blaza Mithupu" naona Blog inageuka kuwa ya matangazo ya vifo naomba liangalie hili maana haipiti siku bila kuwa tangazo la kifo wakati mwingine hata mawili au matatu kwa siku na michango inahitajika.
Maoni yangu tu msinihukumu
Pole sana ndugu zangu mliopatwa na msiba. Ni msiba mkubwa, Mungu awafariji. sasa tukirudi kwenye suala la michango, ndugu zetu mlioko nje ya nchi ninapenda kushauri kuanzishwa kwa umoja wa kusaidiana. Huko mtengeneze katiba yenu kuwaongoza kila kukiwa na tukio, mfano mtu kafia nje, kiasi gani umoja utoe kusaidia, kafiwa nyumbani anatakiwa kusafiri, kiasi gani mfuko utoe. Vile vile na watu tuwe tayari maana misiba haipigi hodi. Tujiwekee akiba ya kusubiri dharura za jinsi hiyo, ili kwamba hatutegemei msaada kwa kila jambo. Jambo lingine kwa wanaofia nje, basi hukuna udongo usiozika, zikeni huko, leteni video nyumbani watu watatazama na wataelewa kwamba kweli mwenzetu alikwenda. sasa hivi dunia imekuwa kama kijiji kwa hivyo tuache kujisumbua na mambo haya kama uwezo hatuna, kama uwezo upo, ruksa kufanya unachotaka.
ReplyDeletePoleni sana wafiwa kwa kupatwa na janga hili ila naungana na wenzangu kusema kuwa mchango kwa mtu aliyefia ar sio dili jamani
ReplyDelete