Kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha Thobias Andengenye akiongea leo. Shoto ni Naibu DCI Kamishna wa Polisi Peter Kivuyo
Kamishna wa Operesheni na mafunzo ya jeshi la polisi Afande Paul Chagonja


Na Woinde Shizza, Arusha
Jeshi la polisi mkoani hapa limesema kuwa halijafanya kosa kuvuruga maandamano na mkutano CHADEMA majuzi likidai kuwa yangeachwa yaendelee yangeleta madhara makubwa zaidi ya yaliyotokea.


Kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha Thobias Andengenye amesema mchana huu wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake kwamba jeshi hilo limetenda haki kabisa kuvuruga maandamano hayo na mkutano huo kwani iwapo vingefanyika kungeweza kutokea madhara makubwa zaidi ambayo yangewapata wananchi na mali zao.


Alisema kuwa mpaka sasa vurugu hizo zimesababisha vifo vya watu watatu baada ya leo kuongezeka ameongezeka mtu mmoja ambaye alijeruhiwa siku hiyo na kusababisha idadi ya watu waliokufa katika vurugu hizo kufikia watatu.
Kamanda Andengenye alimtaja mtu huyo kuwa ni Ismail Omari (37) mkazi wa Unga limited ambaye yeye alijeruhiwa kwa risasi tumboni katika fujo hizo. Amesema marehemu alifariki leo asubuhi katika hospitali ya mkoa ya Mounti Meru na mwili wake umeifadhiwa katika chumba cha kuifadhia maiti cha hospitali hiyo.


Naye Kamishna wa Operesheni na mafunzo ya jeshi la polisi Afande Paul Changonja amesema katika mkutano huo kwamba viongozi wa CHADEMA walikuwa wameachwa kwa dhamana baada ya kusomewa mashitaka kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sheria na sio kwa kufuata shinikizo la mtu yeyote.

Afande Chagonja kasema jeshi la polisi linamshangaa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Kabwe kwa kujifanya kutoa amri viongozi wa chadema watolewe na kutopewa mashariti yeyote, akisisitiza kuwa hicho ni kitu ambacho hakutegemea kabisa mtu kama yeye angeweza kuongea.

"Namshangaa sana Zitto kuzungumza maneno kama haya. Anazungumza maneno bila ya kufikiria kweli, na wakati CHADEMA ndio wamesababisha haya yote. Wasilikwepe hili na wala wasitafute njia ya kulikwepa kabisa "alisema Chagonja.

Alimalizia kwa kuwapa pole wale wote waliopata mazara na kusema kuwa kwa sasa wasiwe na wasiwasi kwani hali ya mji wa arusha imerudi sehemu yake na kutakuwa na fujo tena

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 34 mpaka sasa

  1. KWELI SASA NAZIDI KUAMI POLISI WETU HAWANA UPEO WA KUFIKIRI NA WANAONA WATANZANIA KUA NIWAJINGA KAMA WAO, WATU WOTE WAMEKUFA NA KUJERUHIWA KWA RISASI, NA WALIO KUA NABUNDUKI NI POLISI NA WALIO FYATUA RISASI NI POLISI. SASA MAAFA YANGEKUA MAKUBWA VP KAMA WAO WASINGETUMIA RISASI AU WATU WANGENYONGANA KWA MIKONO MSITUFANYE SISI HATUNA AKILI KAMA NYINYI NAWAOMBA MSOME THEN MKISHAKUA NA UWEZO WA KUFIKIRIA NDIO MUITISHE WAANDISHI WA HABARI MUWAELEZE MAMBO YENU. MNATIA HASIRA KWELI POLISI

    ReplyDelete
  2. Watu wazima ovyoo. mmeshindwa nini kutumia risasi za mpira badala ya za moto. Hatuitaji kibali kuitoka kwa watawala-kuandamana ni haki yetu ya msingi. Ni wakati sasa wa kupata Uhuru kutoka klwa mkoloni mweusi. Miaka 49 mliotutawala inatosha.

    ReplyDelete
  3. LAZIMA MJITETEE, KWAKUWA YAMESHATOKEA YALIYOTOKEA MNADAI MSINGEINGILIA YANGEKUWA MAKUBWA ZAIDI YA HAYO? WAPI UMESHAWAHI KUSIKIA MAANDAMANO BONGO WATU WAMEUWAWA? NYIE MNAKWEPA LAWAMA TU NA HAYA MAUAJI YAMEFANYWA NA WATU WENYE SILAHA ZA MOTO (AMBAO NI POLISI). MSINGEKUWEPO NANI ANGEKUFA NA KIVIPI? MBONA HAMTAKI KUTOA MAELEZO YAKE KUWA WATU WANGEKUFA VIPI AU MADHARA GANI WANGEPATA? JE ULIZNI WA MALI ZA WATU (KAMA MSEMAVYO NYIE) NA MAISHA YA WATU KIPI CHA MUHIMU? MNAONA NI BORA MLINDE MALI ZA WATU HUKU MKIWA TAYARI WATU WAFE JUST KWA SABABU MNATAKA MALI ZIWE SALAMA? KWELI HII NI KAULI YA KIONGOZI WA POLISI??

    KWENYE MAANDAMANO YA DAR, CUF WALIJARIBU KUWAPIGA CHENGA POLISI, NA UZURI POLIS HAWAKUTUMIA NGUVU KAMA KAWAIDA YAO, JE KUNA ALIEKUFA? HII NI KUTHIBITISHA TU KUWA POLISI MKIWEPO LAZIMA WATU WAFE MAANA MNATUMIA NGUVU BILA AKILI.SIJUI SHULE ZENU MLISOMA WAPI NYIE.

    SHAME ON YOU POLICE NA SERIKALI YAO. SHAME ON YOU ALL.....INATIA HASIRA KABISA. HUKU MNAWALIPA DOWANS KWA HELA ZA WANANCHI,LEO MNADAI UPANDAJI UMEME HAUNA UHUSIANO, HAMJAMALIZANA NA EPA, RICHMOND,RADAR, HII SERIKALI INATIA HASIRA SANA.

    ReplyDelete
  4. Huyu RPC mbona anazungumza kama mtu asiye na busara? CHADEMA hawakupiga risasi hao watu,ni jeshi la polisi lililofanya hivyo.

    Hata kama waliandamana bila kibali, jeshi la polisi halikutakiwa kutumia risasi. Wandugu hivi kweli punishment ya kuua mtu inalingana na kosa la kuandamana bila kibali ?

    ReplyDelete
  5. Mafisadi ndiyo wamekuwa Amiri Jeshi wa Tanzania. Uliona wapi Jeshi linaua raia wasio na silaha wala mafunzo ya kijeshi.

    Ukiangalia uso wa Kamanda wa Arusha unaona Ujinga na Unyama combined

    ReplyDelete
  6. Asante sana kwakunionyesha sura za hao wakubwa. Tutajifunza accountability na ku-take responsibilities taratibu.

    ReplyDelete
  7. Polisi hawataki maandamano kwa sababu ya kuhofia fujo sasa kazi yao ni nini mamae zao kama siku ile wao si ndio waliosababisha fujo na kuleta mauaji sasa walikua wanaepusha nini? Sisi tunakatwa kodi nyingi ili kuwalisha wao washibe walinde vizuri wao wanatumika kunyamazisha harakati za kudai haki si watuambie tu kwamba wao ni jeshi la kuilinda CCM

    ReplyDelete
  8. hayo yote yasingetokea kama hao voingozi wange fuata agizo lililotolewa kusitisha maandamano,they got what they wanted na wala wasilalamike.

    ReplyDelete
  9. jamani tuige mifano ya nchi zilizoendelea.uingereza wanafunzi waliandamana na walifunja kioo cha gari la prince charles na hakufa mtu.ingekuwa bongo sijui ingekuwaje.kweli bongo si tambarare hata kidogo.hao mapolisi wanatetea makosa yao.shame on u Polisss

    ReplyDelete
  10. Chagonja anamshangaa nini Kabwe?

    Ajui kabwe ni mbunge na anawakilisha malalamiko ya wananchi! ama mpaka kila mwananchi akitoa tamko ndio ataelewa kwamba unyanyasaji umekithiri?

    Nami natoa tamko langu-
    POLICE ACHENI UNYANYASAJI NA WALISHITAKIWA WAFUTIWE MASHITAKA MARA MOJA.

    Najua police ni vibaraka wa chama tawala kama walivo UVCCM walivolaani maandamano ya kudai haki na wazee wa CCM walivo laumu madai ya KATIBA MPYA. wote mnalinda maslahi yenu kama vile mafisadi wanavolinda maslahi yao kwa kuzuia mabadiliko ya Katiba mpya na na kurudishwa kwa Tanganyika

    Taka msitake wapinzani tutaingia ikulu 2015 na demekrasia ya kweli itadumishwa

    ReplyDelete
  11. kweli nimeamini jeshi la polisi ni la ccm kwani hayo maelezo aliyetoa mkuu wa polisi wa arusha amepewa na chama cha mapinduzi asome hana alakujitetea,na ccm ndiyo waliokuwa wanajua kwamba maandamano hayo yangefanyika yalikuwa yanazidi kukinyima nafasi mwaka 2015!!na bado wamechemka kwani wanazidi kukitia kitu
    mbua mchanga kwahiyo wajiandae kuangukia pua!!na kweli polisi wetu ni waogo sana watu waliokufa ni tano na wengi majeruhi!!

    ReplyDelete
  12. Japokuwa mimi ni mwana CCM damu na nampenda sana Rais wetu (Mkatoliki na ni Mchagga), ila nimesikitishwa sana na mauwaji yaliyotokea Arusha. Ni vyema kutumia "rubber bullet" kama jirani zetu wa Kenya kuliko risasi za moto. Poleni sana mliopatwa na janga hili.

    ReplyDelete
  13. HIVI MPAKA UNAMPIGA MTU RISASI YA TUMBO HAWA WANA AKILI KWELI? NAMUUNGA MDAU WA HAPO JUU ALIYEGUSIA WASINGETUMIA BULLET YA MOTO.HAWAKUWA NA NIA YA KUAMUA KWA AMANI..WAJIFUNZE KWA WENZAO WA MAGHARIBI.
    HII HAITAJI KUWA NA AKILI AU USOME SANA. SASA WANADHANI WATANYAMAZISHA TAIFA KWA HAYO YALIYOFANYA.HUU NAAMINI UNAVUNJA AMANI KATI YA ASKARI JESHI NA RAIA WAKE WEMA. NA SIO VINGINE.

    ReplyDelete
  14. This is a beginning of a change...Tanzanians are tired of corrupt leaders and now they will come out in public to voice their frustrations. However, I wonder why did people continue to vote for CCM despite it's corrupt leaders??? When will that change??

    ReplyDelete
  15. Jambo hili naliangalia kwa mtizamo tofauti kidogo. Nataka nilijadili kwa kuangalia hasa ni kwa nini askari wetu walifikia hatua ya kufyatua risasi za moto. Nasema hivi kwa sababu, risasi za mto hutolewa pale askari wanapoenda doria au lindo ambalo linatarajia kuhusisha arushianaji risasi (Majambazi). Kwa maandamano kawaida askari hutakiwa kuwa equipped na anti riot gears. Katika hizo gears (vifaa) hakuna risasi za moto. Na kwa kuthibitisha hilo juzi tu jeshi letu limepata vifaa bora kweli vya kupambana na ghasia ikiwemo magari ya maji ya kuwasha. Hilo la kwanza, la pili ni namna maandalizi ya mapambano yanavyofanywa. Hii mara zote huongozwa na rules of engagement, sijui polisi wetu wanaongozwa na rules of engagement gani. (Polisi nadhani wana orders zao, kwamba, unapokwenda kutuliza ghasia hizi ndizo taratibu za kufuata hadi kufikia matumizi ya nguvu ya mwisho iliyoandaliwa. Sidhani kama matumizi ya risasi za moto ni moja ya option na kama hawa polisi walifuata huo utaratibu. tatu Maandalizi pamoja na aina ya askari. Kwa taarifa nasoma walitumiwa vijana wa CCP. Well, sijui hasa viwango vyao vya mafunzo. Lakini kama kweli walitumia wanafunzi hili litakuwa ni tatizo kwa polisi. Kwa hali kama hii huwezi kutumia mwanafunzi kwa sababu bado hajawa polisi au bado hajathibitishwa. Lakini kama ilikuwa ni kujaza askari basi hawa wanafunzi wangeishia kupewa virungu na kuambiwa wawalinde wazoefu sina uhakika. Nne, je ni mob saikolojia gani wanayoiangalia wanapo deal na hali kama hizi? wanawaona hao wanaoandamana na viongozi wao wa kitaifa (Kama vile mwenyekiti wa CCM na Katibu wake) kama vile ni wahuni na wanaweza kuamrisha kufanyika fujo?? au watu kama Slaa wanawaona hivyo?. Naamini katika mafunzo yao hufundishwa saikolojia ya ku deal na hali kama hizi. je tathmini yao kweli inawaonyesha yale maandamano yangesababisha fujo?. La mwisho, nini historia na mtiririko wa tukio. Fujo ilianza mara moja au baada ya watu kukaa na kutafakari na kushindwa kuvumilia?

    Ushauri wangu kwa viongozi wa polisi na sertikali. Siku zote mismanagement ya hali kama hizi ni hatari sana. Wawe waangalifu sana katika kushughulikia hali kama hizi. Siku zote lazima kuwepo na win win options, ukilazimisha siku zote win - loose siku moja inaweza kukataa na ndipo unaishia kutumia nguvu zisizo hitajika kwa kuwa hukutegemea na tunakuwa kwenye front pages za news kote duniani. Nadhani hatuhitaji kufika huko.

    ReplyDelete
  16. Hey Wadau?
    MIMI NINA SWALI KWANI? TANZANIA HAKUNA SHERIA YA KULISHITAKI JESHI LA POLICE IN COURT?? KWA UTUMIAJI NGUVU KUPITA KIASI??? HAPA KWA WENZETU MAREKANI NIMEONA PALE POLICE INAPOTUMIA EXCESSIVE FORCE VICTIMS WANALISHITAKI JESHI LA POLICE NA MARA NYINGI NIMESHAONA POLICE AU GOV WANALIPA FIDIA MADOLA YA FEDHA. SASA HAPA TANZANIA KWANI HAKUNA SHERIA KAMA HIZO JAMANI???? VICTIMS MARA NYINGI TANZANIA SIONE HATA KWENDA MAHAKAMANI HATA KAMA NI MAKOSA YA POLICE KULISHITAKI JESHI LAPOLICE HIVI WATU HAPO HAWAELEWI SHERIA NA HAKI ZAO??? WANASHERIA NAO HAPO BONGO NAONA SIJUI KWANINI HAWATUMII HIYO OPPOTUNITY TO OPEN THE CASE??? WAKO WAPI THIS IS THE OPPORTUNITY TO SCREW THE POLICE FORCE NA GOV ILI NEXT TIME WANAPOAMBIWA KULIPA VICTIM FIDIA WATAKUWA NA TAHADHARI YA KUFANYA MAMBO YAO SI KAMA WALIVYOFANYA ARUSHA MAANA HAKUNA INCENTIVE YOYOTE WAUE AU WASIUE DONT CHANGE ANYTHING. JESHI LA POLICE LIPO KWA AJILI YA KULINDA AMANI YA WANANCHI SIO KUVIOLATE THE PEACE.
    mdau USA.

    ReplyDelete
  17. Wananchi tumechoka na fujo na vurugu za CHADEMA kila kukicha, SAFI SANA POLISI ARUSHA HONGERA ANDENGENYE UMETOA MFANO KWA MAKAMANDA WENGINE WAACHE KUFUMBIA MACHOI AU KUWAONEA AIBU WATU WANAOTAKA KUVURUGA TAIFA.

    ReplyDelete
  18. Tusipoziba ufa tusubiri kujenga ukuta, Polisi Arusha wamefanya la maana kwani tayari kuna vyama vilishajisahau na kujiona viko juu ya sheria na vinaweza kufanya lolote vitakavyo, sasa siasa zitakua za heshima na ustarabu kama hawasikii dawa ni kama hii, washughulikiwe bila huruma

    ReplyDelete
  19. Tusipoziba ufa tusubiri kujenga ukuta, Polisi Arusha wamefanya la maana kwani tayari kuna vyama vilishajisahau na kujiona viko juu ya sheria na vinaweza kufanya lolote vitakavyo, sasa siasa zitakua za heshima na ustarabu kama hawasikii dawa ni kama hii, washughulikiwe bila huruma

    ReplyDelete
  20. Kwa nini serekali isitumie uwezo wake wa ki-intelinjisia na kukamata mafisadi, badala ya kutumia uwezo huo kuua waandamanaji? Hata kama waandamanaji walikuwa na makosa, adhabu yao isinge kuwa kifo jamani. Mbona wakati wa uchaguzi kulikuwa na matukio mabaya kuliko ya AR lakini jeshi la polisi lili weza kuhimili matukio yote bila kumwaga damu? MNYONGE MNYONGENI LAKINI HAKI YAKE SI KIFO.

    ReplyDelete
  21. Virungu za juzi!! kweli kiswahili is not richabo.

    ReplyDelete
  22. jamani ndugu zangu watanzania mliowengi msiokuwa na upeo kwa nn msifanye mamboyenu kukaa tu mnashabikia mambo ya siasa?du hamna shughuli nyie kuumiza vichwa vyenu kwa ujinga?hongera sana jishi la polisi kwa kazi nzuri mlio ifanya ukweli mimi binafsi chadema nilikuwa nawakubali lakini sasa nimegundua wanachama wao na viongozi wao wote ni wehu tu hamna kitu kichwani wanaendeleza chuki ya nini uchaguzi uliisha kwisha?wajipange tu 2015 siombali kwanini kila siku tuwasikie wenyewe tu mara mboe mara slaa au huyo zito hee tumechoka kwakweli hasa sisi ambao tupo nje ya nchi wanatu boa tu hawana lolote tumechoshwa na hao watu siwakae tu na nduguzao nini tatizo?hongera sana RPC mkoa wa ARUSHA umefanyakazi nzuri tunakupongeza sana

    ReplyDelete
  23. Toka lini mahandamano yanaitaji vibali vya polisi hata kama ni vibali ni vya aina gani nacho kijua ni kwamba polisi upewa tahalifa na siku mahandamano yatakapo tokea sio vibali na hakuna kua polisi wanaweza kuzuia mahandamano no no hangalia Bush nchi zote halizo kwenda kulikua na mahandamano ya kumpinga na kila mkutano wa UN INAPOFANYIKA NJE ya un kunakua na mahandamano kwa siku zaidi ya 7 polisi awazuhii watu labda ukifanya fujo ndio ushikwa na polisi kwa kosa la kusababisha fujo na nikupewa ticket yako na kuachiwa sasa nchi yetu TANZANIA VIONGOZI MNA NINI MNACHO FICHA RAIA WASIJUE NDIO MAHANA MNATAKA KUWEPO NA VIBALI NEVER KUSIKIA KITU KAMA HICHO KWENYE NCHI YA DEMOCRASIA

    ReplyDelete
  24. I cant believe that up today there are people who are conjured up to speak LIE, all who support what the Police Force did i think their SLAVE OF MIND, Why do we want to make ourselves colonised? I know it was the heads order but WHY only to FREE MIND people like CHADEMA?
    Where is the forces into KAGODA, EPA, DOWNS, RADAR, KIWIRA{Big shame to all mafisadi na ndugu zenu, coz hamna Mungu ndan ya MIOYO yenu wala damu ya UTANZANIA, Mtavuna tu moto hamtauzima}
    I wonder where is the goverment of people for the people?
    Wap wazalendo kama Slaa, Nyerere, Shivji, ni ufisad na uchakachuaji ndo umejaa.
    Aibu mnayo 2015.

    ReplyDelete
  25. hivi mtoto wako akikukosea unachukua kisu unamchoma afe, unamfinya au unamchapa viboko asirudie tena? tafakari then chukua hatua.

    ReplyDelete
  26. NDIO WAMEENDAMANA .TOKA LINI MAANDAMANO YA WATU WASIO KUWA NA SILAHA POLISI KUUA RAIA, HAKUNA HAKI ZA BINADAMU?
    MAANA POLISI ARUSHA INAKIWA KUFUNGULIWA KESI KWA MAUAJI YA RAIA. SASA HIVI DUNIA NZIMA INAONGELEA KUWA POLISI ARUSHA WAMEUA MNATUHARIBIA JINA LA MKOA WETU MNATAKA KUFANYA KUWA SOMALIA?

    ReplyDelete
  27. Mimi nadhani hizo risasi zilitoka kwa bahati mbaya,kwasababu sidhani kama kweli polisi anaweza kudhamilia kuua raia ambaye ameshika hanjifu mkononi,waliteleza kwa bahati mbaya.

    ReplyDelete
  28. Kuna vitu vya msingi vinavyohitaji majibu kuhusiana na tukio hili. Kwa waliokufa, autopsy ifanyike kwa umakini mkubwa ili tujue umbali kati ya marehemu na askari ili tujue kama marehemu aliuawa makusudi. Pia idadi ya risasi kwa kila mwili. Askari wote aliohusika wachukuliwe hatua kali maana inaonekana dhahiri kwamba walitumia nguvu kupita kiasi kitu ambacho ni kosa kwa mjibu wa kanuni za jeshi la polisi. Mfano kuna kijana mwenye umri wa miaka 15 aliepigwa risasi ya paja na mchumba wa Dr. Slaa aliepigwa marungu ya kichwa, hawa hawakuwa na silaha yoyote.

    Askari wetu wana mapungufu makubwa inapokuja kwenye suala la kutumia nguvu kiasi. Tunakumbuka vifo vya wafanyabiashara wa morogoro(kesi ya zombe)?, watuhumiwa kufia vituo vya polisi? Hili linaweza kumkuta mtu yeyote (maana kuna wengine hawashiriki mambo ya siasa)iwapo polisi hawatashinikizwa kufuata sheria na kanuni walizosomea. Kuna haja gani ya mafunzo ya polisi? Kwanini wasichukue majambazi wanaojua vizuri kulenga shabaha wawe askari?

    ReplyDelete
  29. sad sad sad

    ReplyDelete
  30. Wacheni kuzunguka mbuyu, viongozi wa chadema wamewatumia watu kwa ajili ya malengo yao.

    Kibali walichopewa sio cha kuandamana, wanajua wamevunja sheria na siku zote ni mwananchi wa kawaida ndio aliyeponzwa na kuingia kwenye matatizo.

    Viongozi wa chadema wana makosa, kutofata sheria na kusababisha vifo!!!!

    ReplyDelete
  31. lakini hao chadema si waliruhusiwa kufanya mkutano na sio kuandamana? sasa kwa nini waliandamana? huo ndo mshahara wao. Mambo mengine tuwe tunayafuatilia na kayapima si kulaumu serikali kila siku.

    ReplyDelete
  32. Kweli mimi si mchangiaji wala si mwanasiasa lakini jambo hili limenisikitisha sana, wengine watadai maandamano yalizuiliwa ila wakaruhusiwa mkutano. Jamani tujiulize mahubiri tu ya jangwani hayana maandamano lakini utakutana na msururu wa watu kutoka kagera hadi jangwani wakienda kuhuduhuria mahubiri tusema nayo hayo ni maandamano??? kwa hiyo kwa vyovyote vile maadam mkutano uliruhusiwa lazima watu wangekuwa wengi njiani kwenda kwenye mkutano hivyo polisi kutumia silaha za moto kidogo inavunja amani na kuacha maswali mengi kichwani mwa watanzania wapenda amani. Kumbuka kipindi cha kampeni pindi akihutubia Dr. Slaa wala usingejua watu wanatoka wapi kuja kusikiliza lakini kwa Dr. Kikwete magari yalizunguka mitaani kukusanya watu.


    Nyuma ya pazia kuna nini?? tunachofichwa????

    ReplyDelete
  33. anonymous sun Jan 09 08:26:00 AM 2011
    Mdau heshima yako...
    kwa hiyo unachosema ni kuwa polisi waliowaua wananchi hawana kosa ila ni "viongozi wa chadema wamevunja sheria na kusababisha vifo"? Who actually fired the bullets??? Nani muuaji, polisi au viongozi wa chadema? fikiria jibu lako in terms of percentage... kwa akili ndogo tu ni asilimia ngapi utawapa polisi kwa kosa la kuua watu unnecessarily? unatetea ujinga... polisi wangetumia hata maji yenye pilipili! Regardless of kibali or not, watu hawakupaswa kuuawa. Huku ndo kunaitwa kuua nzi kwa bunduki... mtoto anaiba sukari unamchapa na fimbo na kumkataka makalio na kisu.

    Tatizo polisi wetu hawana kazi wanasubiri maandamano ndo wajionyeshe umwamba wao! Kazi yao kubambikizia watu kesi na kula rushwa kutoka kwa mlalamikaji na mlalamikiwa!

    ReplyDelete
  34. Kwa ukweli hali hii inanisikitisha sana.pande zote mbili zinasikitisha.Nikianza na upande wa polisi kweli nguvu hapo si sahihi hamjaona wenzenu wa UN huko Ivory cost,Rwanda na nchi zote zilizowahi kufanya vurugu?Kawaida kikosi cha kulinda amani kinatakiwa kikae intact mpaka pale inapobidi tena kwa kupewa ruhusa!!je ruhusa ilitoka kwa nani?Kwa interest gani?
    Je nyie viongozi wa chadema wa Hai,wa Moshi na Rombo je mmefanya ninimpaka sasa kwenye majimbo yenu?nyie mnaenda kutoa kafara walalahoi hiyo ndo kuwapa maendeleo mliyokuwa mnahubiri huko majukwaani miezi mitatu?Kama mna nguvu za kumobilise watu kiasi hicho kwa nini msimobilise vijana na hao wanaowaunga mkono kutengeneza mashule zahanati hata vikundi vya biashara wapate pesa za kujikimu? Hii ndio kura yangu niliyoipangia mstari nikidhani napigia chama cha maendeleo?Tamaa hizi zinatutia aibu mwishowe mnakosa kila kitu.Zito Mwenzenu yupo Kigoma anapanga maendeleo ya jimbo lake sana anapiga simu nyie mnatafuta nini huko kama sio tamaa na ufinyu wa kufikiri?Mzee wangu Ndesamburo na umri huo mahakamani kufanya nini au mnataka kuwa kama Mandela?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...