Yusuph Bernad akionyesha umahiri wake wa kupuliza mdomo wa bata wakati bendi ya Sikinde Ngoma ya Ukae ilipotumbuiza katika mkesha wa mwaka mpya kwenye ukumbi wa Break Point uliopo Posta Mpya jijini Dar es Salaam.
Mwimbaji mahiri wa bendi ya Sikinde Ngoma ya Ukae, Abdalah Hemba akiimba kwa hisia wakati wa onyesho la mkesha wa mwaka mpy lililofanyika kwenye ukumbi wa klabu ya Break Point uliopo Mtaa wa Simu Posta Mpya jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo. (Picha na Francis Dande wa Blogu ya Jamii)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Changamoto kwa 'maseneta' wa Sikinde na Msondo Ngoma kama kima Michuzi, Papaa Msoffe, Papaa Amos Makala na mapedeshee(PDG) wote kuwa mwaka huu 2011 lazima mpakuwe vitu ndani ya YOUTUBE.

    Maana Sikinde-Mlimani Park na Msondo Ngoma Music band ndiyo T.P OK Jazz ya Tanzania na Afrika Mashariki. Sasa inakuwaje hamjiamini na kuendelea kuutangaza muziki wa dansi duniani kwa teknohama?!

    Kufanya shooting ya video na kuzipakuwa ktk youtube ni kazi ndogo tu, changamkeni mtangaze bendi zenu ndani na nje ya mipaka, si ajabu kupitia kampeni hiyo bendi zetu zinaweza kualikwa nje ya nchi na kupata mikataba minono ya wadhamini wakubwa duniani.

    Mdau
    Mpenzi wa Muziki wa dansi.

    ReplyDelete
  2. Poleni sana kaka zangu wa Sikinde kwa kuondokewa na mwanamuziki mwenzetu mkongwe John Ngosha,Tuko pamoja nanyi kuomboleza msiba huu.Tutamkumbuka sana huyu mkali katika miondoko ya bass Tanzania,kiungo muhimu na ni mmoja kati ya wanamuziki ambao walikubalika hata na wakongwe kama akina Kanda Bongo Man nk.Kwa mara ya mwisho tulionana na Ngosha Feb.2010,pale ddc Kariakoo,hii ilikuwa kama kuagana masikini Ngosha,Kalale mahali pema peponi.
    Abbu Omar,prof.Jnr(Mwanamuziki Japan)

    ReplyDelete
  3. Poleni sana kaka zangu wa Sikinde kwa kuondokewa na mwanamuziki mwenzetu mkongwe John Ngosha,Tuko pamoja nanyi kuomboleza msiba huu.Tutamkumbuka sana huyu mkali katika miondoko ya bass Tanzania,kiungo muhimu na ni mmoja kati ya wanamuziki ambao walikubalika hata na wakongwe kama akina Kanda Bongo Man nk.Kwa mara ya mwisho tulionana na Ngosha Feb.2010,pale ddc Kariakoo,hii ilikuwa kama kuagana masikini Ngosha,Kalale mahali pema peponi.
    Abbu Omar,prof.Jnr(Mwanamuziki Japan)

    ReplyDelete
  4. Hadj Drogba "mwana chelsea"January 03, 2011

    MICHU MBONA PICHA ZA ONYESHO LA PAMOJA MSONDO NA SIKINDE JUZI TAREHE 30/12/2010 PALE MZALENDO PUB UWANJA WA NYUMBANI WA LADY JUDY NA MACHOZI BAND YAKE HUJAZIWEKA KWA WALIOMBALI WAPATE UHONDO?ILIKUA SAFI ILE MBAYA,NILIFURAHI BINAFSI KUMUONA MZEE MZIMA MAX BUSHOKE AKIIMBA JUKWAANI NA DEDE NA BITCHUKA,ILA DEDE ALITAKA KUHARIBU SHOW ILE NZURI KWA MANENO YAKE YA OVYO OVYO!TUNAMUOMBA MTU MZIMA YULE ABADILIKE ILI VIJANA KAMA EDDO SANGA,JUMA KATUNDU,DJ na wengine wapate cha kujifunza kutoka kwa mwanamuziki mkubwa kama yeye ambae vijana hao toka wadogo wamekua wamkisikiliza,na wala hawawezi kushindana nae zaidi zaidi wanaweza kujifunza kutoka kwake.Sio siri nimemtapika Dede kwa kauli zake za kijinga stejini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...