Tamasha la SIKU YA UTAMADUNI WA MTANZANIA litafanyika katika kijiji cha Makumbusho Dar es Salaam kwa siku tatu tangu tarehe 21 Januari, 2011. Kwa mwaka huu kabila la Wanyambo kutoka mkoa wa Kagera watakuwa wenyeji wa tamasha hilo.

Siku ya Utamaduni wa Mtanzania ni utaratibu uliobuniwa na Bodi ya Makumbusho ya Taifa ilipokuwa chini ya Wizara ya Elimu na Utamaduni mwaka 1994 ili kutoa fursa kwa jamii mbali mbali hapa nchini kuonyesha tamaduni zao katika Kijiji cha Makumbusho.

Hadi sasa jamii zifuatazo zimeshashiriki katika maonyesho hayo: Wagogo (Julai 1994), Wazaramo (Julai 1995), Wangoni (Julai 1996), Wachaga (Julai 1996), Wahaya / Wanyambo (Machi 1998) na Wamasai (Novemba 1998).

Wengine ni Wanyakyusa (Novemba 1999), Wamakua/Wayao (Desemba 1999), Waha (Julai 2000), Wasambaa/Wadigo/Wasegeju/Wazigua (Machi 2001), Wasukuma (Septemba 2001), Wakwere /Wadoe (Oktoba 2002), Wamwera (Desemba 2003), Wabena (Agosti 2004), Wairaqw (Desemba 2004), Wakerewe (2008), Wahangaza na Washubi (2009).

Malengo ya kuwa na Siku ya Utamaduni wa Mtanzania ni:

· Kutoa nafasi kwa jamii moja baada ya nyingine kati ya jamii nyingi tulizo nazo kuonyesha mila, desturi na mienendo yao mbali mbali ya jadi ili jamii nyingine ziweze kuelewa na kuthamini utamaduni wa Watanzania wenzao. Hii ni njia mojawapo nzuri ya kukuza uelewano wa kitaifa.

· Kujifunza na kufahamu aina mbali mbali za mila na desturi zinazofaa kudumishwa, kuboreshwa na kurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kama Utamaduni wa Taifa.

· Kupafanya Kijiji cha Makumbusho kuwa kielelezo halisi cha maisha ya Watanzania.

Shirika la Makumbusho ya Taifa linazo program mbali mbali za kuwahamasisha wananchi katika kuthamini, kukuza na kuendeleza utamaduni wa Taifa letu. Miongoni mwa programu hizo ni pamoja na siku hii, Historia Simulizi na Programu ya Watoto wenye mahitaji maalum.

Wananchi wote wanakaribishwa kushiriki katika tamasha hilo ili kufahamu mila na destri za kabila la Wanyambo pamoja na kuburudika na ngoma zao za utamaduni.

Dkt. Ladislaus Komba

KATIBU MKUU

WIZARA YA MALIASILI NA UTALI


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nakuomba Michuzi ukiweza tuwekee picha na video za siku hiyo! Ahsante

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...