Spika wa Bunge la Tanzania Mhe Anne Makinda akiwa pamoja na Maspika wenzake kutoka katika mabunge ya nchi 9 wanachama wa Jumuiya ya Madola ambao wanaunda Kamati Tendaji. Maspika hawa wanakutana katika kisiwa cha Isle of Man kilichoko chini ya utawala wa Malkia Elizabeth II wa Uingereza kuandaa mkutano wa wanachama wote utakaojadili mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kupanda kwa bei za vyakula ulimwenguni. Kikao hicho kilichoanza tarehe 12 kitakamilika tarehe 15 Januari 2011. Spika Makinda atarejea nyumbani tarehe 16 Jan. 2011. Hapa maspika wako kwenye tafrija iliyoandaliwa kwa heshima yao.
Spika Makinda akiwa na Spika wa India
Mhe. Meira Kumar (kati) katika mkutano huo

Maspika wakitembelea maeneo mbalimbali
ya kihisoria katika Kisiwa cha Isle of Man
.
Picha zote na Prosper Minja wa Bunge

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. naamini ushauri wa mavazi ulimfikia. Good looking.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...