Mwanamziki wa bendi ya msondo ngoma,Hamisi Maliki 'Super Maliki' pichani amefaliki Dunia. mwanamziki huyo aliyekuwa akiimba sauti ya kwanza amefaliki katika hospital ya Agrikan Malapa jijini Dar es salaam alfajiri ya kuamkia leo.

Marehemu Maliki alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa limonia ambao ndio umpelekea kupoteza maisha.mipango ya mazishi inafanya na tutaendelea kufahamishana kadri taarifa zitakavyokuwa zikitufikia.

Globu ya Jamii inatoa pole kwa Bendi ya Msondo Ngoma kwa kumpoteza kipenzi chao pamoja na ndugu,jamaa na marafiki wa Marehemu.

Mungu ailaze pema peponi roho ya Marehemi.
-Amein.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Poleni Sana! Msondo ngoma pamoja na ndugu wa marehemu,
    Tumepokea taarifa hii kwa majonzi makubwa,
    mwenyezi mungu amlaze pema peponi marehemu,
    Wadau
    ngoma Africa Band aka FFU

    ReplyDelete
  2. poleni kwa msiba,na huu mwaka unaonekana sio mwepesi kwa wanamuziki,mwenyezi mungu atupe mwisho mzuri
    Mdau istanbul

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...