
Leo tunapoadhimisha kumbukumbu ya mapinduzi ya zanzibar ya tarehe 12 january 1964 kuna haja ya dhati kabisa kujihoji usahihi wa historia ya mapinduzi hayo kwa maana ya nani alihusika, nani alikuwa kiongozi wa mapinduzi hayo ili mwishowe tupate historia kamili ya visiwa hivyo vya karafuu kuliko hivi sasa ambapo historia ya mapinduzi hayo ina utata mkubwa ambao umepelekea kuandikwa vitabu mbalimbali na wanahistoria mbalimbali huku mjadala mkuu ukiwa ni nani hasa shujaa wa mapinduzi hayo kati ya professa Abdurlhaman Babu, Karume na John Okello.
Baadhi ya vitabu vya historia vinamtaja rais wa kwanza wa Zanzibar na aliyekuwa makamu wa kwanza wa rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kuwa ndiye hasa kinara wa mapinduzi hayo ya januari 12
Pia kuna baadhi ya vitabu vya wanahistoria wengine wanaodai kuwa mganda John Okello kuwa ndiye hasa aliyeongoza mapinduzi hayo huku mwenyewe wafuasi wake wakimpachika jina la Field Marshal Okello kutokana na ukakamavu wake, tena wanahistoria hawa wanatumia ushahidi wa picha iliyopigwa siku ya mapinduzi ambayo inamwonyesha Okello ndiye pekee aliyevaa kiaskari kuonyesha kuwa yeye ndiye kiongozi.
Lakini hiyo haitoshi kuonyesha kuwa kuna msuguano wa kihistoria kwenye visiwa hivyo ambavyo ni maarufu kwa zao la karafuu
kuna vitabu vinamtaja professor Abdurlhaman Mohamed Babu aliyekuwa kiongozi wa chama cha Umma party ndiye hasa kinara wa mapinduzi hayo
Lakini bora ingekuwa hivi tu ingevumilika lakini sasa mwaka 2010 tumeshuhudia kuchapwa kwa kitabu cha Kwaheri ukoloni kwa heri uhuru , huku kikituacha hoi wapenda historia wengi kwa jinsi mwandishi wa kitabu hiki Dr kassan alivyoweza kuibua hoja nzito za kihistoria ambazo bila shaka zimetuonyesha kwa kiasi gani tunahitaji historia sahihi ya visiwa hivyo ili tuwarithishe watoto na wajukuu zetu kuliko hivi sasa ambapo ni kama tunaficha ukweli au tunapotosha historia makusudi.
Akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Redio Desutchwelle Dr Kassan alisisitiza kuwa kwa takribani nusu karne historia ya Zanzibar imepotoshwa kwa makusudi na watawala huku akisisitiza kuwa kitabu chake hiko ni kwaajili ya kuandika historia ya kweli ya visiwa hivyo akaenda mbali zaidi kwa kutaka jamii isimchukulie kama amekuja kufukua makaburi bali amekuja kuweka maua juu ya makaburi.Haya ni baadhi tu ya mambo ya msingi kabisa yanayoonyesha kuna ulazima tena wa haraka wa kuandika upya historia ya mapinduzi ya zanzibar. Hivyo tunaposherehekea mapinduzi ya Zanzibar siku ya leo ni muhimu pia tukakumbuka jukumu letu la kuwa na historia sahihi ya mapinduzi hayo ambayo itakuwa ni kumbukumbu muhimu kwa vizazi vijavyo.
Nova Kambota
Mzumbe university Morogoro
0717 709618 au 0766 730256
novakambota@gmail.com
novadream.blog.com
Inasikitisha kuona mpaka leo msomi kama wewe unaamini vitabu!! Kitabu hakina "peer review" na ni dhaifu kunukuu. Mtu yeyote anaweza kuandika kitabu. Mwandishi wa kitabu anaandika kwa malengo yake. Kwani aliyeongoza vita vya Kagera alichukua uraisi Uganda? Kamanda wa majeshi anapewa amri tu ya kupigana vita na kusimamisha vita. Unafikiri Hitler alichukua bunduki kupigana katika vita kuu ya pili ya dunia? Si kila dereva wa gari analimiliki hilo gari baba.
ReplyDeleteMr. Nova Kambota umenikosha mazee, kweli wewe ni msomi uliyotukuka na sio kama wasomi wengine wababaishaji!
ReplyDeleteYou are really mzalendo wa kweli na unapenda historia ya kweli bila ya propaganda. Na kwanini basi huyu Okello akawa mmoja wa mapinduzi, alitumwa na nani?
Kwanza napenda kukupa pongezi za dhati kwa kuwasilisha mada hii, lakini pili nahisi umetuacha kwenye mataa ulipotaja historia iliyoandikwa kwenye kitabu cha Kwaheri ukoloni, kwaheri uhuru cha Dr kassan kawni wengi wetu hatujui kuna nini kwenye kitabu hicho,ninachopenda kuongezea nahisi suala la kuelezwa kwa uwazi kwenye historia sio nani shujaa wa mapinduzi, bali nani alipinduliwa na kwa sababu gaini, kwani baadhi ya historia zinaeleza kwamba waliponiduliwa ni wa Zanzibari tena weusi kama mimi na wewe. Mwisho naungana nawe kudai histria ya mapinduzi iandikwe upya.
ReplyDeletekmohd@live.com
mtoa maoni kmohd@live.com kwanini unataka historia ambayo haijatimia? iweje tutajiwa/tufafanuliwe ni nani alipinduliwa bila kumtaja aliyepindua? ahsante mtandao manake unafichua mengi. viva john okello.
ReplyDeleteNi mada nzuri sana. Watanzania waliosoma nchini, walisona somo la siasa na somo la historia zilizopikwa na kupikika na makada wa chama tawala kuwaelimisha watanzania watakavyo wao ili kulinda sera na itikadi tawala. Ni kama mtoto aliyedanganjwa utotoni sasa kawa mkubwa, kaelimika na anaona mambo mwenyewe, anataka kujua ukweli na baba anatahamaki. Tufunguke upeo na mawazo watanzania, tuwe huru kutoa maoni, Wengine jinsi tulivyopumbazwa akili zetu miaka na miaka basi hata tukiona mwenzako anatoa maoni yake kuhusu jambo basi unaona huyu vipi au unafikiri ni mkorofi, la hasha ndio haki za binadamu hizo. AlexBura Dar
ReplyDeleteHaaa, umenikumbusha mbali sana kuhusu haya mambo ya historia. Tunapenda sana kurukia mambo ya karibu na ya kiswahili na kutaka kuyarekebisha kwa nguvu zote. Mambo yaliyowekwa na Mjerumani au Muingereza hata kugusa hatugusi. Mfano angalia historia na vitabu vyake dunia nzima vinasema mtu wa kwanza kuona mlima kilimanjaro duniani ni johannes Rebman, je kuna ukweli hapo. Ukiangalia kwa dhana ya mwandishi wa historia hiyo ni kweli maana aliandika kwa mtizamo wa kuona kwake bila kujali wachagga walioishi hapo miaka nenda rudi.
ReplyDeleteHilo pia na sawa kwa wanaondika historia, hufuata dhana ya mwandishi, na kusema Karume, au Okello, au Othman walikuwa kinara cha mapinduzi kwa vitabu tofauti vya kihistoria ni sawa. Kuna watu wanahistoria wanaamini kabisa kwamba kinara mkuu ukitaka kusema wa ukweli juu ya mapinduzi ya Zanzibar ni Mwalimu nyerere aliamrisha mapinduzi haya kwa kuhofiaa Zanzibar ikiwa huru itakuwa sehemu ya Kenya kama hapo awali waingereza walivyoifanya kuwa chini ya serikali ya kifadhihina ya Mombasa, Kenya. Angalia sana historia kwani kila mmoja huandika kwa upande wake.
Huu mjadala ni upumbavu mtupu...kwa kuwa hautusaidii kupunguza inflation au mgawo wa umeme.
ReplyDeleteplease tunaomba mada endelevu si hizi za kujadili yaliyopita na ambayo hayatusaidii kwa maisha yetu ya leo.
Mdau UK
ni Dr Harith Ghassany ingia www.kwaherikwaheri.com,kuna mambo mengi ya kutafakarisha na maswali ni mengi!
ReplyDelete