Ankali Mithupu hivyo ndiyo hali halisi ya jinsi ya matokeo ya kidato cha nne mwaka 2010. Mkuu wa NECTA hakulitoa kwa asilimia ambazo huwa watu wengi hatuwezi kuzing’amua kwa urahisi.

Ila hayo ndo maafa yaliyotukumba Tanzania kama Taifa,maana huu ni msiba wa kitaifa na ni janga kwa Nchi yetu kutoa 0(division Zero) 174,193 ndani ya mwaka mmoja.
Wadau wanao husika na sekta hii muhimu wito kwenu tufanye kazi kwa bidii kuonoda aibu hii. Napenda kuwasilisha.
Mdau wa Elimu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Kuna graphs hapa ambazo zitakufanya uhoji zaidi:

    http://vijana.fm/2011/01/28/elimu-ya-sekondari/

    ReplyDelete
  2. Namba ime-balance, Div 1 hadi Div IV jumla wapo 177,021, hao wote watachaguliwa kujiunga na kidato cha V kwenye shule za serikali.
    Waliopata Div 0 nao wapo 177,021 nao watagombania nafasi kwenye shule za binafsi na wasiokuwa na uwezo serikali itawajaziajazia kwenye shule zao. Hapo hakuna chenji, kila mwanafunzi atapata shule.

    Matari, Galloway OHIO

    ReplyDelete
  3. Waziri aliyekuwa na dhamana ni PROFESSOR na aliyepo sasa hivi ni DOCTOR na wote ni MAKADA wa CCM.
    Hebu na tujaribu kuomba msaada wa upande wa upinzani hasa yule kijana wa CHADEMA, John Mnyika.

    Abiola Jr.

    ReplyDelete
  4. na Mdau umesahau kuwa division four officially is failure kwa hiyo idadi ya ambao hawakufaulu ni 313,654 na waiopasi ni 40,388 ambayo ni sawa na asilimia 12.8,hiki ni kiwango cha kibovu ambacho kama sio waziri wa elimu basi maofisa wa wizara husika wanatakiwa wastaafu,serikali inawaharibia vijana future zao bila ya hata kuwa responsible,kati ya hao 80% waliofeli ni 30% ndio watakaoweza kwenda private na 50% iliyobakia tumeshaipoteza,halafu tunategemea tucompete na kenya na uganda katika free market,wache tu waje kutuongoza,watanzania inabidi tuanze utamaduni wa kuhoji viongozi wetu majukumu yao,maneno mengi hayajengi ...
    Mdau Istanbul

    ReplyDelete
  5. hao walio pata vichwa vya kuku , ndo wanapewa office kesho!!

    mdau china

    ReplyDelete
  6. katka hili kuna kila jitahada za serikali kuliangalia upya suala la mfumo mzima wa elimu kwa mazingira kama haya tunaona huyu mwanafunzi aliyepata div 0 km amepoteza miaka yake minne (4) bure bora angefanya kazi nyingine angekuwa walau na ujuzi wa kazi hiyo, pia serikali iwajali walimu ili wawe na moli na khari ya kuipenda kazi yao, upande wa pili ni kipengere cha mmomonyoko wa maadili kwa wanafunzi wenyewe ziro nyingi ni za wacheza viduku,wavaa vi bajaji na washamba wachangamfu

    ReplyDelete
  7. Sina uhakika kama number hizi zipo sawa. Naomba ufafanuzi. Yaani Division I-IV jumla wapo 177,021 na wenye division 0 (zero) wapo 177,021. Je hizi namba zimefanana kibahati tu au kuna makosa kwenye kuwasilisha. Mdau naomba ufafanuzi.

    ReplyDelete
  8. Tatizo liko wapi hapa? waliofeli kama ni watoto wa walala hoi hilo sio tatizo wanajua the drill, ikiwa waliofeli ni watoto wa vigogo na matajiri shule za ng'ambo zimejaa tele, watasafirishwa kwenda kusoma nje bila tatizo lolote!!!!

    ReplyDelete
  9. Kazi kwelikweli, shule za kata, binafsi,za serikali zote zimefanya vibaya tuu, tatizo hapa ni mfumo mzima wa elimu tulionao na wanafunzi wa nyakati hizi nao bomu tu hawajitumi kazi kutegemea mitihani ilivuja.


    Mdau DSM TZ

    ReplyDelete
  10. Inawezekana tatizo ni mtihani wa kuwapima, wala sio wapimwaji.

    ReplyDelete
  11. sasa takwimu zimekuwa sasa
    division I HADI IV ni 177,021
    division 0 ni 174,193.
    Hii inabidi mtihani wa kidato cha pili kurudi.
    Maana hali ni mbaya sana kwa watoto na vijana wetu.

    ReplyDelete
  12. 1.Waalimu hawako motiveted, JK anajitahidi kuongeza idadi ya shule, na kuongeza idadi ya waalimu, bila kuongeza idadi na kwalite ya fasilitiiz huko mashuleni na motivesheni kwa waalimu so, Workdone = 0
    2.Shule zimekuwa nyingi sana, kwa nini tusifaulishe nyingine tuwarudishie mashirika ya dini yaendeshe? Ona kwa muda mfupi sana tumefaulisha Forodhani sec school kwa kanisa katoliki, mmeona matokeo yake?.
    3.Waalimu wanapata wanachostahili kweli? Tujiangalie.
    4.Utandawazi jamani....... Mwanafunzi anatokea kwa mume kwenda shule, kisa kwao ni mbali na shule, shule hazina usafiri wala hosteli, kadanganya kwao amepanga chumba mjini, kumbe yuko kinyumba hana uwezo wa kujitegeme.
    5.Shule za kata ni mradi uliyofeli, wanaoingia form one toka darasa la saba, wengine hawajui hata kusoma wala kuandika, kisa wajaze tuu hizo shule tuonekane tumeboresha mazingira ya kusoma.
    6.na mengine meengi uwiiiiiiiii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...