Na Mwandishi Maalum
New York
Katika kutambua umuhimu wa raslimali misitu kwa uhai wa mwanadamu na Sayari Dunia,Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, limeutangaza mwaka 2011 kuwa mwaka wa Kimataifa wa Misitu,
Uzinduzi wa kuutangaza mwaka 2011 kuwa mwaka wa kimataifa, umefanyika siku ya jumatano katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali mashuhuri akiwamo mwanaharakati wa mazingira, Profesa Wangari Maathai.
‘ Misitu kwa ajili ya watu” ndio kauli mbiu ya mwaka wa Kimataifa wa misitu. mkazo ukiwa katika kuchagiza na kuhamasisha utuzaji wa misitu, upandaji miti, na matumizi endelevu ya raslimali hiyo muhimu ambayo inatoweka kwa kasi.
Kuzinduliwa kwa Mwaka wa Kimataifa wa Misitu kumetanguliwa na mkutano wa wiki mbili ambapo wataalamu wa misitu wakiwamo mawaziri, kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, walikutana na kujadiliana pamoja na mambo mengine maendeleo endelevu ya misitu na umuhimu wake kwa maendeleo ya kiuchumi kwa mamilioni ya watu ambao maisha yao hutegemea raslimali hiyo.
Tanzania ilishiriki katika Mkutano huo kwa kuwakilishwa na Bw. Juma Mgao Mkurugenzi Msaidizi, kitengo cha Maendeleo ya Misitu na Bi Gladnes Mkamba ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi kitengo cha Ufugaji Nyuki.
Akizungumza kwa njia ya Video, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amesema kwa kuutangaza mwaka 2011 kuwa mwaka wa kimataifa wa misitu, UN imetengeneza platform ya kuielimisha jamii kuhusu thamani ya misitu na hasara kubwa ya kijamii, ya kiuchumi na kimazingira itakayotokana na upotejaji wa misitu.
Naye Rais wa Balaza Kuu la Umoja wa Mataifa, Bw. Joseph Deis, ambaye ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa uzinduzi huo.Akielezea umhimu wa misitu, anasema raslimali hiyo inamchango mkubwa sana kwa maisha ya mwanadamu.
Akasisitiza kuwa misitu pia imekuwa na uhusiano mkubwa na mila , desturi tamaduni , na dini za mataifa mbalimbali.
“ Misitu inatupatia makazi, chakula, nishati, dawa na mambo mengine mengi. Mamilioni ya watu na hasa katika nchi zinazoendelea maisha yao ya kila siku yanategemea sana misitu. Misitu inatuhamasisha, na kuwapa watu mahali pa kumpumzika na kupumua, ni dhahiri kuwa misitu ni mapafu ya sayari dunia” anasisitiza Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Lakini. Anasema Deis. “ Pamoja na kuyatambua yote hayo, kila dakika tunayoitumia kupumua katika sayari dunia, ekari 25 za misitu hutoweka kwa sababu mbalimbali”.
Akaongeza kwa kusema, matumizi ya kupita kiasi ya raslimali hiyo na matumizi mabaya, yanaathari kubwa katika vita dhidi ya umaskini,vita dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi na majanga ya asili.
Kwa upande wake, Profesa Wangari Maathai alipopata fursa ya kuzungumza, alieleza kuwa, mwanadamu kwa hulka yake na kutokana na huduma anazozipata kupitia misitu, siyo tu kwamba anajisahau lakini anaamini kuwa raslimali hiyo inataendelea kuwapo daima dumu, ili hali ukweli ni kinyume na hayo,misitu inatoweka.
Akaongeza kuwa kwa kuufanya mwaka 2011 kuwa mwaka wa kimataifa wa misitu. Kumbe basi mwanadamu anapata fursa nyingine ya kutambua na kuthamini umuhimu wa miti, misitu na mazingira yake.
Katika maadhimisho ya mwaka wa kimataifa wa misitu, kila nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa, inatakiwa kuadhimisha kwa kuwa na program zinazolenga kuwaelimisha na kuhamasisha wananchi kupitia mbinu mbalimbali kuhusu umuhimu na haja ya kupanda miti kwa wingi, kuilinda na kuihifadhi.
Takwimu zinazonyea kuwa angalau watu 1.6 bilion maisha yao ya kila siku yanategema sana uwapo wa misitu na raslimali nyingine zitokanazo na misitu.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...