Gharama za chakula kama ngano, mahindi, sukari na mafuta ya kupikia imekuwa ya juu kuliko wakati mwingine wowote. FAO inasema bei zimekuwa zikipanda kwa miezi saba iliyopita na inaonekana itaendelea katika miezi ijayo.
Ngano, mahindi, sukari na bidhaa za maziwa imepanda kwa asilimia kati ya 3 na 6 kwa mwezi Januari mwaka huu wa 2011. Hali hii imesababisha kufanyika kongamano la kimataifa mjini Geneva Uswis kuhusu kupanda kwa bei ya chakula, athari zake na njia za kukabiliana na tatizo hilo. Kongamano hilo limeandaliwa na shirika la Umoja wa mataifa la masuala ya bidhaa na biashara UNCTAD na kuhusisha FAO, shirika la mpango wa chakula duniani WFP na wadau wengine.
Miongoni mwa waliohudhuria ni balozi Ali Mchumo ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa mfuko wa pamoja wa masuala ya bidhaa wa UNCTAD. Amezungumza nwa mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva Patrick Maigua na kuanza kumueleza nini sababu kubwa ya kupanda kwa bei ya mazao duniani.
Kwa kina bonyeza links hizi kusikiliza
au http://www.facebook.com/
au http://twitter.com/redioyaum
au moja kwa moja kwenye taarifa yenyewe
http://www.unmultimedia.org/
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...