Sauti ya Vijana Tanzania (SAVITA) na Philosophy Club za Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam, vinawakaribisha sana kwenye Kongamano la Kuadhimisha Miaka 44 ya Azimio la Arusha.

Kongamano litafanyika siku ya Jumamosi tarehe

05/02/2011 kuanzia saa 3:30 Asubuhi mpaka saa 8:00 Mchana, kwenye ukumbi
wa Nkrumah. Kongamano litakuwa katika lugha ya Kiswahili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hivi azimio la Arusha bado lipo? Lilikua ni nini? Madhumuni yake hayajawa out date kweli nakumbuka tulisoma sana hii tukiwa primary school na tulikwnda kuutembelea mnara wa azimio pale....

    Hemu mutukumbushe azimio la arusha lilikua ninini?

    ReplyDelete
  2. Haya maazimio yalikua ni kufunga watu macho tu kama raisi wa Egypt anavyotaka kufanya. Ilikua watu wakifurukuta na kudai haki zao basi linaundwa hiki mara kile mara kushuffle cabinets ili kupooza watu. Lakini waafrica wameamka...leo kaskazini kesho kusini keshokutwa Kaskazini na isye twaja soon...

    No freedom of speech at all and we need to be heard...but love the social network...They can't mute that. So just they know....

    ReplyDelete
  3. Seth Benjamin Day.

    Hao ndugu wanaouliza kama Azimo la Arusha ni nini, ni kielelezo kinachoonyesha jinsi historia ya nchi yetu inavyopuuzwa.

    ReplyDelete
  4. Kwa asiyejua maudhui ya Azimio la Arusha namshauri akasome kitabu cha Mwalim J.K. Nyerere kiitwacho Ujamaa: Essays on Socialism, nadhani kuna toleo la kiswahili pia. Ukisoma kitabu kile utaelewa kwanini leo hali imekua mbaya kama ilivyo, na hutahitaji kuuliza kwanini leo matokeo ya shule za serilaki yamekua mabaya pengine kuliko kipindi kingine chochote katika historia ya Tanganyika na Tanzania. Mawazo yalikua mle ni ya msingi sana sema tu kwamba watu hatujipi muda wa kusoma na tumekua watu wa kuendeshwa na propaganda na kuchukia Azimio la Aarusha wakati kiukweli wengi wetu tusingekua hapa tulipo leo kaam si baadhi ya mambo yaliyokuwemo kwenye azimio la arusha.
    Binafsi nawapongeza watu waliotisha hili Kongamano kwani linatukumbusha fursa nzuri tuliyopoteza ya kuwa na taifa lenye maadili hasa kwa viongozi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...