WABUNGE wa Chadema wakiongozwa na mwenyekiti wao, Freeman Mbowe jana walichafua hali ya hewa bungeni pale walipotoka tena nje ya Ukumbi ya Bunge kupinga azimio la kuondoa utata wa tafsiri ya Kanuni ya Bunge inayotoa fursa kwa chama chenye asilimia 12.5 ya wabunge wote kuunda kambi rasmi ya upinzani.

Tukio hilo linalofanana na lile la Novemba 18, mwaka jana, Rais Kikwete alipozindua Bunge lilifanywa na Chadema baada ya Mbowe ambaye pia ni mbunge wa Hai mkoani Kilimanjaro kuchangia mjadala wa huo akiwa mchangiaji wa mwisho.

"Madamu Bunge limeona busara kuleta hoja hii, na vijembe vile, kwa masikitiko nasema hatutashiriki kumalizia hoja hii, naomba kutoa hoja," alimalizia maelezo yake Mbowe na kuanza kutoka nje akifuatiwa na wabunge wa chama hicho. Kwa habari kamili tembelea Mwananchi..
BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Hiyo kutoka nje ya kikao ni pia sehemu ya demokrasia.

    Nchi zingine kama Uingereza wabunge badala ya kutoka nje wao huzomea hoja za wabunge wenzao ndani ya ukumbi, jambo ambalo kwa Tanzania nadhani siyo vizuri, ni bora kutoka nje kwa muda.

    Pia kanuni za bunge la muungano kwa sasa halizuii wabunge wa chama fulani kutoka nje wakiona mjadala unataka kuwabinya CHADEMA kutokana na mbinu za kisiasa za chama chenye wabunge wengi kama CCM.

    Hivyo kidogo kidogo ndiyo sasa Watanzania tunaelewa mbinu za kisiasa ktk kuwakilisha hisia za chama fulani kupinga hoja yoyote bungeni na hasahasa kama kuna chama chenye wabunge wengi kutumia wingi wao wa kupitisha miswada bungeni kishabiki zaidi bila kuangalia ubora wa hoja/ muswada unaotaka kubadili sheria na kanuni za vikao vya bunge.

    Mimi nawaunga mkono CHADEMA kwa kutumia njia inayokubalika kisheria kama kutoka nje ni dalili za kupinga hoja kiungwana hasahasa ikizingatiwa CCM inataka ku-'bully'(a.k.a kuonea) vyama vingine.

    ReplyDelete
  2. Haya ni mambo ya ajabu sana, hata kama Michuzi hutaweka hii posti yangu lakini nasema hata ukiisoma wewe pia inatosha unaweza kuijadili peke yako rohoni mwako. Kwani asiyejua kuwa CUF ni chama tawala ni nani? itakuwaje chama tawala walazimishwe kuungana na chama cha upinzani? hii sio kweli kabisa, ingependeza sana CCMCUF iwaachie wapinzani waendelee kukosoa madhaifu yaliyopo kuliko kufanya maamuzi ya lazima ya kuunganisha watu ambao sera zao ni tofauti ambayo si halali hata kidogo.

    ReplyDelete
  3. Hawajachafua hali ya hewa bali hawataki kuburuzwa ebu tafuta ile clip ya bunge la kenya ndo utajua demokrasia inavyotetewa, nimeona huko kwenye blog ya u turn clip ya bunge la wanageria kwa kweli ni kama maigizo watu wanachapana hadi kuchaniana nguo, na hii ndio dawa ya ccm manake wanajifaya wababe sana mabavu hadi kwa waheshimiwa wenzao...... haaaaaaaaaaata hiyo si kweli dereva wacha vitukooooo!!!!

    ReplyDelete
  4. nawaunga mkono CHadema haswaaa,pia kitu kingine wabubge mliobaki kule jana tumeona kama vile mnatoa vijembe haipendezi,jaribuni kuongelea swala la umeme imekuwa kero sana sasa tunapata umeme kwa wiki mara 2 inasikitisha sana sana,tunaelekea wapi acheni mafumbo teteeni haki kuna mbunge 1 jana katoa maneno kweli kweli wanatakiwa wajadiliane kwanini vitu vimepanda je wafanye nini wananchi wapate maisha bora, sio kupeana vijembe

    ReplyDelete
  5. Mnazungumzia CCM NA CUF ndio wenye hila. Sasa NCCR, UDP nk. sio upinzani. Chadema mmeshindwa kujenga kambi ya upinzani kutokana na uchu wa madaraka na upeo wenu mdogo. Sasa acheni kulia lia hapa. Ndio demokrasia ata kama uamuzi hampendi ndio hivyo teh teh teh

    Chadema wanataka kujifanya wao ndio wanauchungu na nchi hii kuliko vyama vingine :)!?

    ReplyDelete
  6. Chadema Ovyo!!!! nafasi yakuunda kambi ya upinzani na kuunganisha nguvu mlikua nayo, sasa msimtafute mchawi

    ReplyDelete
  7. Chadema walitaka kuunda kambi ya pamoja ya upinzani wenzao wakaleta nyodo. Leo waliposikia bila kuungana hawatapata uenyeviti wa kamati za bunge ndio wanajifanya umoja ni nguvu.
    Ukiona CCM wanaunga mkono suala la wapinzani kuungana ujue mwananchi wa kawaida unatengenezewa maumivu. CCM wanataka kuipandikiza CCM-B ndani ya umoja wa wapinzani. Habari ndio hiyo.

    ReplyDelete
  8. Chadema hawana jipya kwenye Siasa. Ni wao ndio wenye ubabe na umwamba hata kwenye maamuzi ambayo hayahitaji kutumia ubabe. Sijui tunaelekea wapi.

    Hakafu Ankal kuna coments hazipostiwi. kuna coment nimeiandika siioni. Hawa Chadema inatakiwa waambiwe ukweli wa mambo, manake naona vichwa vyao vibovu kuanzia viongozi wao hadi mashabiki wao.

    Nilishawaambia kuwa Mtu anapotokota hata kama ni wako mwambie ukweli kwa nia ya kumjenga. Watakaa wanasusia bunge hadi lini? Kutoka kwao hakutengui uhalali wa maazimio yanayopitishwa. So it doesn't help. Watakaa wanatoka nakurudi hadi watu watawaona wendawazimu. Hawajapelekwa na wananchi kugimea vikao.

    Wakipewa nchi hawa watatuangamiza kwa staili hii, kwani hata wasipofikia muafaka na wananchi watakuwa wanatususa hivyohivyo, kwamba kama hamtaki shauriyenu. Sasa ni uongozi huo?

    Ninaloliona mimi ni Ubinafsi na uroho wa madaraka. Kwani kuwamo CUF na vyama vingine ndani ya kambi ya upinzani hakuwaondolei wao nguvu ya kufanya maamuzi ndani ya kambi ya upinza, kwa bado kura zao ni nyingi ukilinganisha na idadi ya hivyo vyama wanavyovikataa.

    Madhara ya hiyo mitafarukuku ni kuendelea kupigana vijembe wao kwa wao CCM anaendelea kupeta. Ndiyo kanuni ya dhambi ya ubaguzi. Kama hawalioni hilo, haya tuendelee hivyohivyo. Wakishindwa wanakimbilia kwenye maandamano yasiyokuwa na msingi wowote na kuleta vurugu.

    ReplyDelete
  9. ki ukweli na uhalisia CUF HAIWEZI KUWA NDANI YA KAMBI YA UPINZANI KWANI WAO TAYARI WAMEUNDA SERIKALI NA CCM
    HATA KWA MTOTO MDOGO HUWEZI KUMDANGANYA UKAWA SERIKALI AT THE SAME TIME UKAWA MPINZANI WA SERIKALI HAIWEZEKANI
    HUWEZI KUWA MCHEZAJI WA SIMBA AT SAME TIME YANGA

    ReplyDelete
  10. Siku hizi democrasia inaitwa kuchafua hewa? Michuzi usituletee hapa.. na comments acha kubania..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...