Chama cha maendeleo na demokrasia nchini (CHADEMA) leo kimefanya maandamano ya amani katika jiji la Mwanza kupinga kupinga mchakato wa uchaguzi na matokeo ya Meya wa Jiji la Arusha, kuunga mkono maandamano yaliyofanywa na chama hicho mkoani Arusha Januari 5, mwaka huu na kupinga zoezi la serikali kulipa deni la Dowans.
Mabango yenye ujumbe mbalimbali yalibebwa
Juu na chini ni maandamano hayo makubw ambayo yalianza na kumalizika kw amani huku yakisindikizwa na polisi
Chanzo na kwa picha zaidi
mtembelee mdau G. Sengo

BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. sasa mbona mambo yameenda vizuri hakuna fujo wala nini!!!muwe na akili saa nyingine sio kutumia virungu tu siku zote alaaa

    ReplyDelete
  2. nyie chadema acheni kudanganya watu eti mnafanya maandamano ya
    amani. kwani nyie hamna kazi za kufanya. kila kukicha
    mnaandamana kupinga hili au lile. sasa mnaanza kuonekana kuwa ni
    watu wa fujo. hao wabunge wa chadema kwanini wasi wasilishe hayo
    matatizo bungeni waka yajadili huko badala ya kuwachochea watu
    na kuwafanya waache shughuli zao na kwenda kuandamana.

    ReplyDelete
  3. tihih hih hii. hapo sisiemu wamechukia na kununa kwa kuwa hakuuwa na fujo. siku zote tunasema kuwa fujo huanzishwa na wanaintelijenzia wa sisiyeem ili kupaka matope upinzani.

    polisi limewajaa shingoni, tihih hih hiii!! abali ndo iyo.

    ReplyDelete
  4. Wee hapo juu unayepinga maandamano inelekea umeneemeka na huguswi na machungu ya dunia hii. Ndio nyie wale wa Egypt kila siku mlikua mnalumba wale waliokua wanaandamana.."mnaandamanan ninii", "hamna kazi na hamna cha kufanya" sasa hivi wamekaa kimya hata huwasikii tena...Acheni watu wanaoipenda nchi waseme ukweli...Nyie mafisadi msioguswa na unchungu wa nchi hameni si mnahela za kupaa kila mpendavyo? Siye hatuna hata ya kutoka nje ya mji kwa hiyo kwetu hapa hapa ..

    ReplyDelete
  5. Patrick NhigulaFebruary 25, 2011

    "Mtoto akipewa elimu atakuwa mwanadamu mwenye taaluma na ujuzi"; Watanzania walipewa elimu na Mwalimu bali viongozi wachache waliomfuata wamesahau nchi ilikotoka. Demokrasia Tanzania inakuwa na mwananchi wanaanza kuelewa umuhimu wa demokrasia.

    ReplyDelete
  6. Waacheni waandamane huko bungeni wamebanwa pumzi kila upande wakijaribu kusema wananyamazishwa, Nchi inahitaji ukombozi na wakombozi ni sisi wenyewe. Wewe hapo juu unayepinga bora upae nje ya nchi kama ulivyoshauriwa na mchangiaji wa awali, huu ni mwanzo tu.

    ReplyDelete
  7. Wewe any, hapo juu unasema wawakilishe matatizo bungeni? Hivi hujaona bunge lililopita eeh, yule mama kila wanaloongea chadema analiweka kapuni, sasa unafikiri wataongelea wapi maoni yao kama si kwa njia ya mikutano.
    Hii nadhani watu wamejifunza kitu na kupata majibu ya nani anayesababisha fujo wakati wa maandamano. Kuna usemi usemao aliyeshiba hajui mwenye njaa, tafakari.

    ReplyDelete
  8. AIGIPI,VIPI INTELIJINSIA ILIFANYA KAZI HAPA ROCK CITY? HONGERA SIMON SIRO PAMOJA NA VIJANA WAKO. NAJUA HAPA SISIEMU NA IGP WATAKUCHUKIA KWA SABABU HUKUANZISHA FUJO, ASANTE KWA BUSARA ZAKO NAFIKILI HATA YULE MALAFYALE ANDENDE ATAIGA KUTOKA KWAKO HATA AKINA KOVU SIJUI KOVA WAIGE PIA.

    ReplyDelete
  9. Chadema tupo pamoja na naamini Mungu atasikia kilio chetu. Hongereni sana na kazi nzuri ya kutetea WADANGANYIKA na sio WATANGANYIKA. Mshikamano pamoja nategemea siku moja tutapata mabadiliko ya kweli. CHADEMA JUU JUU JUU zaidi.

    ReplyDelete
  10. kabisa wewe hapo juu unaesema wasiandamane we kaa tuu, acha watu wanaojua uchungu wa nchi waandamane,hv kwenye akili yako unaona swala la DOWANS ni zuri sana????? kila kitu kimepanda vyakula ndio usiseme,maji ya shida bill ikija mwisho wa mwezi unaweza kulia maana sasa maji mara moja kwa wiki mara bill iyo,jaman watanzania sio wale wazamani kabisaaaa tumeamka kutoka usingizini hatudanganyiki na DOWANS,EPA,RICH MOND tumechokaaaa mafisadi ndio wanakula sie masikini kutwa kulia shida tutaandamana mpaka we haikuhusu.

    ReplyDelete
  11. sasa hulo bango linalosema mmiliki wa dowans akamatwe,yeye ndio anaidai nchi harafu tena eti serikali imkamate kwa kifungu gani? inaweza kukataa kulipa au kupunguziwa deni hapo sawa, jamani kuweni na akili!!!!!

    ReplyDelete
  12. mbona sio full shangwe!!! nilidhani barabara zingejaa sana watu, bila ya kuona viraka. Ukifanya sampling, unaweza kukusia watu wangapi katika maandamano haya?
    Mdau, Pemba

    ReplyDelete
  13. chadema wachokozi kweli sio kwamba wamefurahi hakuna fujo hawa jamaa ni attention seekers, nilikua nawafagilia sana hawa jamaa lkn sasa sina mpango nao bora hata wangeandamana kupinga malipo ya dowans hawa wanapenda madaraka sana na tukiwapa nchi tumekwisha, leo hii wao hata habari ya Gongo la Mboto hawana wamen'gan'gana na umeya wa Ausha wakati wenzao wamepoteza familia na huku nchi imegubikwa na shida ya umeme na majanga mfululizo.

    ReplyDelete
  14. Na leo na kesho na keshokutwa waendelee kuandamana hapo hapo Mwanza, kila siku waandamane tu hapo hapo sehemu moja, kama ni kazi rahisi kuiga iga tu wakati watoto wanataka ugali!

    ReplyDelete
  15. Hongera sana Chadema at least umewawezesha wananchi wa mwanza kutoa dukuduku zao sisi hapa Dar ni waoga sana hata kumpiga picha tu anayejiita mwekezaji wa Dowans tunaogopa sembuse kuandamana,tunaugulia tu kimya kimya ukweli tunaumia mno .Mgao wa umeme,sukari imepanda,foleni za magari,ugumu wa maisha na mengine mengi.Hongera Chadema.

    ReplyDelete
  16. wameshau nchi inaomboleza janga la Gongo la mboto wao wanadai madaraka kazi kweli.

    ReplyDelete
  17. Hongera chadema wembe ni ule ule hakuna kurudi nyuma, tutaandamana mpaka palipoandikwa basi wanaoona maandamano ni kupoteza muda wamechelewa!

    ReplyDelete
  18. kaazi kweli kweli eti mmiliki wa dowans akamatwe hivi watu wanaoandika mabango kama hayo wameenda shule kweli? mmiliki wa dowans ana hela chafu sana anaweza hata kununua nusu ya mji wa daresalam

    ikiwa serikali ilishindwa kuwakamata mafisadi wake wa hapo nchini na kuwafungulia kesi itaweza kumkamata tajiri kama huyo wa dowans ambae ana hela chafu vibaya sana

    mtu alikuwa na nia ya kutukomboa katika janga la kiza na sasa mambo hayakufanikiwa leo hii tunamuona adui hivi sisi wadanganyika tumelogwa au vp? mbona hatujui maana ya maendeleo tunachokijuwa sisi ni kufagilia mafisadi na sio kufagilia wanaotuletea maendeleo.


    raisi mtarajiwa wa tanzania 2020.wakati makamo wake akiwa ankal mzee wa libeneke.ikulu oyeeee hehe ankal

    ReplyDelete
  19. Rudi nyuma:

    Ni %-age ngapi ya wa-Tanzania watumiao umeme!

    Wa-Tanzania wengi hawajawahi kutumia umeme! Na hao ndio wengelengwa katika maandamano hayo.

    Tuachane na tabia ya kupalilia apartheid Tanzania ...na huku wengine wakijigamba kuwa maandamo hayo ni "nguvu ya umma"!

    "Nguvu ya umma"; over my dead body!

    ReplyDelete
  20. Andamaneni mchana mpaka usiku, wapuuzi wakubwa, kama kweli mnajali si mngeenda Gongolamboto kutoa damu na kuhamasisha wapenzi mashabiki wenu (kama wa timu za mpira vile) waende wakatoe msaada Gongolamboto. Kwanza Ndesamburo ana majumba mpaka Ulaya na ana pesa kama hana akili nzuri sijamuona kutoa msaada. Na tungewaona wa maana kama mngesema posho yenu ya wabunge wa Chadema ya wiki nzima mpeleke Gongolamboto.

    Hivi hamjijui wenzenu wamekwishawadharau ndio maana wamewaruhusu muandamane, na mtaandamana wee mpaka mtachoka wenyewe mtakaa kitako! Haya mmeandamana mmepata nini sasa? Nyie mna pesa za Illuminate ndio maana mna muda wa kuandamana, sie tunaosotea ugali kwa mikono yetu utapata wapi muda wa kupoteza kwa maandamano?

    Endeleeni kuota hivyo hivyo kuwa yule triple 6 wenu atatawala tena hapa kwetu hatupati ng'oo, watu wanafanya maombi ya nguvu na hizo fujo zake zitaishia huko huko alikozianzisha maana anapenda sana kunywa damu za watu

    ReplyDelete
  21. USHAULI WANGU KWA MUHESHIMIWA KIKWETE ANGALIA WANANCHI WAKO WANACHOHITAJI NINI UWAFANYIE C.C.M ISIJE KUPOROMOKA MIKONONI MWAKO ANGALIA BARABARA ZISIVYOJENGWA KWA UBORA..TAZAMA KIPANDE CHA KUTOKA AIR PORT KWENDA GONGOLAMBOTO KINAVYOCHUKUA MUDA MREFU KINACHOFANYIKA HAKUNA...ANGALIA UMEME KWA NINI HICHI KIANGAZI WATU WASITOE MATOPE KATIKA MABWAWA NA UJENGE JINGINE KUBWA ILI UVUNE MAJI KIPINDI CHA MASIKA AU HAIWEZEKANI????ANGALIA WATU WANVYOVUNJIWA NYUMBA ZAO KWA MRADI WA MTU MMOJA JE HAYO MABASI YAENDAYO MWENDO KASI MTAYAWEZA??BARABARA ZENYEWE ZIKO WAPI AU SERIKALI INAKURUPUKA TU????HIVI HUONI WANANCHI WAKO WANAVYOISHI KWENYE NYUMBA ZA MIAKA 47????HUONI KIJIJINI WANANCHI WANAVYOTEMBEA BILA NGUO NA VIATU????HV HOUNI WANAFUNZI WANAVYOKOSA HATA MADAWATI YA KUKALIA???????HIZO PESA MNAZOCHANGISHA WAKATI WA KAMPENI KWA NINI MSIZIFANYIE KAZI WAKATI HUU??NA HILI DENI LA DOWANS LINA UMUHIMU GANI KULIPWA??NA MADINI YETU YANAENDA WATU KODI ZETU ZINAENDA WAPI???HV UTAWAFUMBIA MACHO HAWA MAFISADI MPAKA LINI WANAKUCHAFUA HAO ANGALIA 2005 ULIVYOPITA KWA KISHINDO LAKINI ANGALIA SASA WANANCHI WANAZIDI KUPOTEZA IMANI...AMKA IKIWEZEKANA FUATILIA MWENYEWE UPUNGUZE SAFARI ZA NJE ILI WANANCHI WARUDISHE IMANI NA SERIKALI YAKO

    ReplyDelete
  22. Anony Fri Feb 25, 09:45:00 PM 2011 ungemalizia maoni yako kwa maneno, "CCM oyee!!!"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...