Mashabiki wakifurahia kupanda daraja kwa JKT Oljoro leo
Timu ya soka ya JKT Oljoro ikiwasili uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo wakitokea mkoani Tanga ambapo imefanikiwa kupanda daraja na kufikia kushiriki ligi kuu ya Vodacom.
Nahodha wa timu ya JKT Oljoro akimkabithi kombe katibu wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Arusha (ARFA)Adamu Brown mara tu baada ya timu hiyo kuwasili uwanjani hapo
Katibu wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Arusha akiongea na wachezaji wa jkt oljoro huku akiwapongeza kwa kufanikiwa kupanda daraja na kuipa sifa mkoa wa Arusha. Picha zote na Woinde shizza wa Globu ya Jamii,Arusha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. duh. vijana mnanikumbusha operesheni 'programu ya chama' intake june 15, 1989 - june 14, 1990. Mambo ya kule kwa 'fini', duka la mbao, mizabibuni, vitofa, afande tyetyetye, co karubi, efukoy, embakassi, dunia, kilima shabaha, shimo la mungu ... so many good memories.

    nakumbuka siku moja, jkt oljoro ilikuwa icheze mechi muhimu ya daraja la nne dhidi ya AICC. marehemu method mogella alikuwa amesajiriwa na kuichezea AICC. at the same taim, alikuwa ni kuruta wa jkt oljoro kwa mujibu wa sheria, hivyo jkt kudai kuwa method ni mchezaji wake halali, kivumbi hapooo. guess nini kilitokea? he hee, ... method aliswekwa rumande (kwotagadi) kuepusha madhara.

    nakumbuka makuruta wenzangu wakati huo, ... ulomi eliofoo upo wapi mwana? Fundi Sangia, uko wapii? Ankonaay Hhawwuu Hhaybee mu-Iraqw upo wapi mwalimuu? Fundi chochi kijana mtanashati wa wana, semaa nikusikiee? Mkaxi-man wa E-koi sema mwanangu, ... nakumbuka zile siku tulipojongo saa nane usiku na kuelekea A-town huku tukipigana vikumbo na fisi? Unakumbuka ile siku tulijibebesha bonge ya mawe huku tukiruka na kuimba (up, up, up, ... kama vile tulipewa adhabu), kumbe ilikuwa ni njia ya kujongo saa tisa mchana kweupee, kuelekea A-town?! nawasalyuti kikosi chote cha ujenzi amacho baadaye kilikuwa dispatched kumalizia mkataba kule mabogini moshi.

    pongezi timu ya jkt oljoro, wadau wa kambi (833kj kama sikosei) pia tuko nyuma yenu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...