Bw. Yusuf Manji akiwa na wakili wake Mh. Mabele Marando wakati alipoingia kwenye Chumba cha mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa ushahidi na kuwasilisha vielelezo vya kesi yake dhidi ya Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Bw. Reginald Mengi. Picha na Mussa Mateja

UPANDE wa mashitaka katika kesi ya kashfa ya madai inayomkabili Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd, Reginald Mengi, dhidi ya mlamikaji Yusuf Manji, jana umepinga kuwasilishwa kwa nyaraka za upande wa uetetezi kwa kuwa hazijatimiza matakwa ya Mahakama.

Wakili wa Manji Mabere Marando alitoa madai hayo mbele ya Hakimu Mkazi Aloyce Katemana wa Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu jijini Dar es Salaam.

Alidai nyaraka hizo si halisi wakati sheria inakataa nyaraka kivuli kuwasilishwa mahakamani kama kielelezo cha ushahidi.

“Sheria inakataa nyaraka kivuli ila iko sheria ya kuomba kuwasilisha hicho kivuli ambayo walitakiwa kuwasilisha kabla ya kusikiliza shauri hilo, kama ni nyaraka za serikali inatakiwa kuwa na tangazo la ofisa aliyetoa nyaraka hiyo ambayo pia inatakiwa ilipiwe.

“Wao hawakuomba hilo tangazo kwa hizo nyaraka ambazo zinaonyesha zimetoka serikalini na hazijatimiza masharti ya Mahakama, kwa hiyo hazifai na zinatakiwa ziondolewe kwani zinatupotezea muda, kwani hata hivyo shauri lililopo mbele yetu linahusu mtu na mtu na si kampuni na mtu, kwa hiyo nyaraka hizo pia hazimhusu mteja wangu” alidai Marando.

Upande wa utetezi ukiwakilishwa na Wakili wa Mengi Michael Ngalo uliiomba Mahakama wapewe muda aweze kuwasiliana na mteja wake ambaye yuko safari mkoani Arusha na pia waweze kujipanga kujibu hoja hizo zilizotolewa na upande wa mashitaka.

Shauri hilo limeahirishwa hadi Februari 17, mwaka huu litakapokuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa.

Katika kesi hiyo Manji anamdai Mengi na kituo cha televisheni cha ITV amlipe fidia ya Sh moja kwa kumkashifu kwa kumuita ‘Fisadi Papa’ na kwamba mmoja wa watu wanaopora rasilimali za Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Marando ???????????????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. Marando Njaa Itakuua

    ReplyDelete
  3. Unafiki wa viongozi wa upinzani Tanzania...kukashifu "mafisadi" majukwaani, kuwatetea mbele ya sheria.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...