Rais Barack Obama ametoa wito wa kuwepo na kipindi cha mpito kitakachopelekea kundwa serikali itakayo sikiliza matakwa ya wananchi. Viongozi wa Ulaya kwa upande wao wametoa wito wa kuwepo na uchaguzi wa huru na haki katika taifa hilo la Kiarabu lenye wakazi wengi.
White House ilieleza Jumapili kwamba rais Obama alizungumza na viongozi wa Uingereza, Uturuki, Israel na Saudi Arabia mnamo siku mbili zilizopita. Alirudia nia ya serikali yake ya kuwepo hali ya kustahmiliana wakati inaunga mkono haki za kidemokrasia kwa wananchi wa Misiri ikiwa pamoja na haki ya kukusanyika pamoja kwa amani na haki ya kujieleza.
Mhadhiri wa chuo kikuu cha Florida Charels Bwenge anasema Marekani inajikuta katika hali nzito, kwa upande haiwezi kumtupa rafiki yake wa muda mrefu katika utaratibu wa amani na wakati huo huo inaunga mkono mabadiliko ya kidemokrasia kwa wamisri.
Habari kamili tembelea VOA
Hosni is as old as Mugababe. Kwasababu tu ni kibaraka wa Marekani na Uingereza hawajambatiza kama DICTATOR! Maslahi kwanza demokrasia baadae.
ReplyDelete